• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Shirika kuu la Utangazaji la China CMG latangaza habari kumi kubwa za kimataifa kwa mwaka 2019

  (GMT+08:00) 2019-12-31 09:44:29

  2. Ukuaji wa uchumi wa dunia wadorora, huku ukuaji imara wa uchumi wa China ukichangia zaidi uchumi wa dunia

  Ripoti ya Makadirio ya Uchumi wa Dunia iliyotolewa Oktoba 15 na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF, ilishusha makadirio yake ya ongezeko la uchumi wa dunia hadi kufikia asilimia 3, ambayo ni kiwango cha chini kabisa tangu msukosuko wa kifedha ulipolipuka mwaka 2008.

  Katika mazingira ya kimataifa ambayo kuongezeka kwa sera za kujilinda kibiashara kumekwamisha ukuaji wa uchumi wa dunia, ukuaji wa uchumi wa China ulidumisha mwelekeo mzuri, na kuongoza duniani kwa mchango wake mkubwa kwa uchumi wa dunia. China iliendelea kushikilia sera za mageuzi na kufungua mlango, kulinda kithabiti mfumo wa biashara wa pande nyingi, kujitahidi kusukuma mbele ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja", kuinufaisha dunia nzima kutokana na maendeleo yake na kuleta fursa nyingi kwa nchi mbalimbali duniani. China imekuwa injini muhimu ya ukuaji wa uchumi wa dunia.


  1  2  3  4  5  6  7  8  9  10  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako