• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yazisaidia nchi zinazoathiriwa na Ebola kuanzisha na kuboresha mfumo wa afya ya umma
    Naibu mkurugenzi wa Kamati ya Afya na Uzazi wa Mpango ya China Bw. Ma Xiaowei amesema China inazisaidia nchi zinazoathiriwa na Ebola kudhibiti maambukizi ya ugonjwa huu na kuanzisha na kuboresha mfumo wa afya ya umma wa nchi hizo. Vilevile Bw. Ma amefahamisha kuwa, hakuna tukio la maambukizi ya Ebola, wala watu wanaodhaniwa kuambukizwa virusi vya Ebola nchini China kwa sasa.
    Chanjo ya Ebola yaanza kufanyiwa majaribio nchini Usiwisi wiki hii
    Hatimaye chanjo ya Ebola inayosubiriwa kwa muda mrefu inaanza kufanyiwa majaribio wiki hii nchini Uswisi.
    Wanasayansi wasema Dar iko katika hatari ya kupata mlipuko wa Ebola
    Wanasayansi kutoka chuo kikuu cha Oxford nchini uingereza wameiweka Tanzania katika orodha ya nchi za Afrika ambazo ziko katika hatari kubwa ya kupata mlipuko wa Ebola. Wanasayansi hao pia wameonya kwamba zaidi ya watu milioni 22 barani Afrika wako katika hatari ya kupata maambukizi.
    AU yafanya mkutano wa dharura kuhusu mapambano dhidi ya Ebola
    Kamati ya utekelezaji ya Umoja wa Afrika jana ilifanya mkutano wa dharura kwenye makao makuu yake mjini Addis Ababa, ambapo ilitoa mwito kwa nchi wanachama wa umoja huo kushikamana na kushirikiana kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa wa Ebola, na kuhimiza jumuiya ya kimataifa itoe uungaji mkono zaidi katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo.
    Tunachoweza kujifunza kutoka kwa China ili tujilinde dhidi ya Ebola
    Wakati maambukizi ya Ebola unapoendelea kukithiri katika nchi tatu za Afrika magharibi, na kuingia nchini Jamhuri ya kidemokrasi ya kongo hivi majuzi, wengi wetu tutakuwa tunakumbuka jinsi China ilivyosumbuliwa na homa ya mafua makali SARS, na hata changamoto nyingine za kiafya zilizotokea baada ya hapo, ikiwa ni pamoja homa ya mafua ya ndege.
    Madaktari wa China washirikiana na wa Afrika kupambana na ugonjwa wa Ebola
    Nchi kadhaa za Afrika Magharibi zimekumbwa na ugonjwa wa Ebola. Huu ni mlipuko mkubwa zaidi wa ugonjwa huo kutokea tangu virusi vya Ebola vigunduliwe mwaka 1976. Hivi sasa ugonjwa huo umesababisha vifo vya watu zaidi ya elfu moja. Nchini Sierra Leone, madaktari kutoka China wanashirikiana na wenzao waafrika kupambana na ugonjwa huo.
    China yafanya juhudi kuisaidia Sierra Leone kupambana na Ebola
    Hivi sasa ugonjwa wa Ebola ulioanza mwezi Desemba mwaka jana nchini Guinea, na kutajwa kuwa ni "tukio ghafla la afya ya umma linalofuatiliwa na nchi zote duniani", bado unaendelea kuenea na kutishia usalama wa nchi nyingi za Afrika magharibi, mpaka sasa umesababisha vifo vya watu zaidi ya elfu moja.
    China yatoa misaada ya matibabu yenye ufanisi kwa wakati kwa nchi za Afrika zinazokumbwa na ugonjwa wa Ebola
    Mshauri wa rais wa Nigeria ambaye pia ni chifu mwenye asili ya China Bw. Hu Jiegou, amesema serikali ya China imetoa misaada mingi ya vitu vya kinga na matibabu kwa wakati kwa nchi za Afrika Magharibi zinazokabiliwa na ugonjwa wa Ebola, na vikundi vya wataalamu wa matibabu wa China pia vimefika katika nchi hizo, hatua zinazoonesha kuwa China ni nchi kubwa inayowajibika.
    Wataalamu wa afya wa China waenda Afrika Magharibi kushiriki kwenye mapambano dhidi ya Ebola
    Ugonjwa wa Ebola uliozikumba baadhi ya nchi za Afrika Magharibi unafuatiliwa sana na jumuiya ya kimataifa. Wataalamu wa afya waliotumwa na serikali ya China wameondoka kuelekea Guinea, Liberia na Sierra Leone kusaidia kazi ya kupambana na ugonjwa huo. Hii ni mara ya kwanza kwa China kutuma vikundi vya watalaamu wa afya kupambana na ugonjwa huo. Fadhili Mpunji anatueleza zaidi.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako