China yatangaza ripoti kuhusu hatua na sera za China katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa mwaka 2015 Kamati ya Taifa ya Maendeleo na Mageuzi ya China imetoa ripoti kuhusu hatua zilizochukuliwa na sera za China katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa kwa mwaka huu. Ripoti hiyo inasema, katika miaka mitano iliyopita, China imepata mafanikio makubwa katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa kupitia marekebisho ya mwundo wa viwanda, kubana matumizi ya nishati na kuinua ufanisi wake, kuongeza nishati safi na kupanda miti. Katika mkutano wa hali ya hewa utakaofanyika huko Paris, China iko tayari kushirikiana na pande mbalimbali kuhakikisha mkutano huo unafikia makubaliano yanayotarajiwa kwenye msingi wa haki na kanuni ya "wajibu mmoja majukumu tofauti". |
China yapambana na bidhaa feki ili kulinda sifa ya "Made in China" Baada ya serikali ya China kutoa mpango wa kupambana na bidhaa feki zinazouzwa nje ya nchi, idara mbalimbali za China zimechukua hatua kwa pamoja za kupambana na bidhaa feki ili kulinda sifa ya "Made in China". |
China kukuza utoaji mpya wa soko na msukumo mpya wa uchumi kutokana na mahitaji mapya ya matumizi Kamati ya maendeleo na mageuzi ya China leo imesema, ili kuhimiza mageuzi ya uchumi na kuongeza ufanisi wake, China itaharakisha maendeleo ya sekta ya utoaji huduma, kulingana na mahitaji mapya ya matumizi, ili kuendeleza utoaji mpya sokoni na kukuza msukumo mpya wa uchumi. |
Mitaji ya nje inayowekezwa nchini China yaongezeka kwa utulivu katika miezi 10 iliyopita Katika miezi 10 iliyopita, mitaji ya kigeni inayowekezwa nchini China imeongezeka kwa utulivu, na imetumiwa zaidi kwenye sekta ya huduma za teknolojia ya juu na viwanda. Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, ingawa ongezeko la biashara ya China na nje limepungua, lakini China pia imedumisha nafasi yake ya kwanza kwa ukubwa wa biashara duniani. |
Waziri mkuu wa China afanya mazungumzo na wataalamu na viongozi wa kampuni kubwa kuhusu hali ya uchumi ya sasa Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang Jumatatu wiki hii amekutana na wataalamu na viongozi wa kampuni kubwa za China, na kusikiliza maoni na mapendekezo yao kuhusu hali ya uchumi ya sasa. |
Pendekezo kuhusu kutunga mpango wa miaka mitano ijayo wa maendeleo ya China lajumuisha mambo makuu matatu Chama cha Kikomunisti cha China CPC kimetangaza pendekezo kuhusu kutunga Mpango wa Miaka Mitano Ijayo wa Maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii ya China, lililopitishwa katika kikao cha 5 cha wajumbe wote wa Kamati Kuu ya 18 ya CPC kilichomalizika Oktoba, 29. Mkurugenzi wa Kamati ya Maendeleo na Mageuzi ya Taifa ya China Xu Shaoshi anasema pendekezo hilo lina mambo makuu matatu, na China ina nia na uwezo wa kufanya uchumi wake uongezeke kwa kasi ya kati na hadi kubwa. |
Makampuni ya ndani ya China yaonesha kuwa na imani ya muskabali mzuri katika soko la China Tovuti ya uchumi ya China hivi karibuni ilichapisha makala iliyotolewa na naibu mkurugenzi wa idara ya utafiti wa kampuni ya Kituo cha Utafiti wa Maendeleo cha Baraza la Serikali la China Zhang Yongwei, akielezea kuhusu imani ya makampuni ya China kuhusu mwelekeo wa hali ya soko la China katika mazingira mapya kiuchumi. |
Ujenzi wa jamii yenye maisha bora kwa pande zote wawa matarajio mapya wa wananchi wa China Mkutano wa tano wa wajumbe wote wa Kamati Kuu ya 18 ya Chama cha Kikomunisti cha China umepitisha pendekezo la kutunga mpango kuhusu maendeleo ya uchumi na jamii katika miaka tano ijayo, na kutoa malengo mapya kuhusu kujenga jamii yenye maisha bora kwa pande zote, ambayo yametoa matarajio mapya ya Wachina. |
Wachumi wa nchi za nje na vyombo vya habari vinaona mustakbali mzuri kuhusu mpango mpya wa China wa maendeleo ya miaka mitano Wachumi na vyombo vya habari vya nchi za nje vinaona kuna mustakbali mzuri kuhusu itikadi ya maendeleo iliyomo kwenye mpango mpya wa 13 uliopitishwa na malengo yaliyowekwa kwa maendeleo ya uchumi na jamii ya China katika miaka mitano ijayo. |
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |