Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
 
v Mwongoza wa michezo ya kuigiza wa China, Lin Yihua  2007/12/17
Tokea mwaka 2000 "Kukutana mjini Beijing" ni tamasha la wasanii ambalo linafanyika kila mwaka katika majira ya Spring, mjini Beijing. Kwa bahati mwaka huu tamasha hilo linafanyika wakati China inapoadhimisha miaka mia moja ya mchezo wa kuigiza nchini China.
v Wakulima wajitahidi kustawisha biashara ya utamaduni ili kuondoa umaskini 2007/12/03
Qinghai ni mkoa wenye wakazi wa makabila mengi, raslimali za utamaduni wa kikabila ni nyingi. Katika miaka ya hivi karibuni serikali ya mkoa imekuwa inajaribu kuwawezesha wafugaji kuongeza mapato yao kwa njia ya kustaswisha biashara katika sekta ya utamaduni wa kikabila.
v Tamasha la nane la michezo ya sanaa lachangia ustawi wa utamaduni nchini China 2007/11/26
Tamasha la nane la sanaa la China linalofanyika kwa siku 16, linaendelea mjini Wuhan, mji mkuu wa mkoa wa Hubei. Kaulimbiu ya tamasha hilo ni "kustawisha utamaduni wa kisasa na kujenga jamii yenye masikilizano ya kiutamaduni".
v Mkoa wa Ningxia nchini China wajitahidi kuhifadhi urithi wa utamaduni usioonekana  2007/11/05
Mkoa unaojiendesha wa Ningxia wa Kabila la Wahui, ni moja ya mikoa mitano inayojiendesha ya makabila madogomadogo nchini China. Ingawa mkoa wa Ningxia uko nyuma kiuchumi ikilinganishwa na mikoa ya pwani ya mashariki ya China, lakini mkoa huo una utamaduni wa jadi unaong'ara.
v Mwigizaji nyota wa filamu Li Lianjie (Jet Lee) 2007/10/29
Bw. Li Lianjie anayejulikana kwa wengi kama Jet Lee, mwenye umri wa miaka 44, ni mwigizaji mashuhuri wa filamu za gongfu. Tokea mwaka 1982 alipoigiza filamu yake ya kwanza ya "Hekalu la Shaolin", hadi sasa ameigiza filamu 33 za michezo ya gonfu. Hivi karibuni filamu yake ya "Shujaa Huo Yuanjia" ilioneshwa mjini Beijing.
v Maingiliano ya kiutamaduni ya nchi tatu, China, Japan na Korea ya Kusini yazidi kuimarika 2007/10/15
Huu ni mwaka wa 35 tangu uhusiano wa kibalozi kati ya China na Japan na uanzishwe na ni mwaka wa 15 tangu uhusiano kati ya China na Korea ya Kusini uanzishwe
v Filamu ya katuni ya "Matembezi ya Fu Wa wa Olimpiki" yavutia  2007/10/01
Wanasesere Fu Wa wa kuashiria baraka kwenye michezo ya 29 ya Olimpiki ya Beijing mwaka 2008 wanawavutia sana watu wa China na wa nchi za nje. Tokea tarehe 8 Agosti, filamu ya katuni yenye sehemu 100 inayolenga kueneza elimu ya michezo ya Olimpiki ilianza kuoneshwa katika kituo cha televisheni CCTV nchini China. Filamu hiyo sio tu inawavutia watoto, bali pia inawavutia watu wazima
v Uzuri wa mji wa Kashi wanakoishi Wa-uygur mkoani Xinjiang 2007/09/17
Mji wa Kashi mkoani Xingjiang ni mji wanakoishi na watu wa kabila la Wa-uygur. Huu ni mji uliowekwa chini ya hifadhi ya taifa kutokana kuwa na historia ndefu. Watu husema kama ukitembelea mkoa wa Xinjiang bila kufika mji wa Kashi ni sawa na bure.
v Maeneo ya Shannan?chimbuko la utamaduni wa Tibet 2007/09/03
Maeneo ya Shannan yaliyoko upande wa kusini wa milima ya Tanggula na Gandise na sehemu ya kati na ya mwisho ya mto Yalu Tsangpo ni chimbuko la utamaduni wa kale wa Tibet, mahali hapo palikuwa na utajiri na penye utamaduni mkubwa katika zama za kale. Katika maeneo hayo kuna kasri la kwanza la Yongbulakang na hekalu la kwanza la Changzhusi la dini ya Kibuddha mkoani Tibet.
v Filamu ya kiserikali ya michezo ya Olimpiki ya mwaka 2008 mjini Beijing yaanza kupigwa rasmi 2007/08/20
Michezo ya Olimpiki inayovutia kote duniani itafanyika mwezi Agosti mwaka kesho. Upigaji wa filamu ya kiserikali ya michezo hiyo umezinduliwa? na kuanzia mwezi Machi mwaka kesho filamu hiyo itaingia katika kipindi halisi cha upigaji wake.
v Utamaduni wa kiasili wa Tibet wahifadhiwa vizuri 2007/08/06
Tibet ni mkoa uliopo kusini magharibi mwa China, mkoa huo sio tu unavutia kwa kuwa na milima yenye theluji na maziwa yenye maji maangavu bali pia unavutia kwa utamaduni wake, kasri la Potala, hekalu kubwa la Jokhang na opera ya Kitibet yenye historia ya miaka mingi.
v Ushirikiano katika sekta ya filamu kati ya sehemu ya ndani ya China na Hong Kong waimarika 2007/07/23
Tarehe mosi Julai ilikuwa ni siku ya kuadhimisha miaka 10 tokea Hong Kong irudishwe nchini China. Katika muda wa miaka 10 iliyopita maingiliano kati ya sehemu ya ndani ya China na Hong Kong yamekuwa yakiongezeka siku baada ya siku katika uchumi na utamaduni, na ushirikiano katika sekta ya filamu pia unazidi kuimarika, katika muda huo filamu zilizotengenezwa kwa ushirikiano zimekuwa zaidi ya 200
v Li Yuchun mwanafunzi wa kike aliyejulikana ghafla na kuwa maarufu 2007/07/09
Mwaka 2005 kipindi cha "mashindano ya kuchagua wanafunzi hodari wa kike" kilichotangazwa na kituo cha televisheni cha Mkoa wa Hunan kiliwavutia watu wengi nchini China, na mwanachuo Li Yuchun aliyeshinda kwenye mashindano hayo akapendwa na vijana wengi wa kike na wa kiume nchini China.
v Mwigizaji wa filamu Yu Entai 2007/06/25
Mchezo wenye sehemu 80 wa vichekesho kwenye televisheni "Hadithi za Wanagonfu Hodari wa Zama za Kale Nchini China" ulianza kuoneshwa katika vituo vingi vya televisheni nchini China. Mchezo huo unawafurahisha sana watazamaji, na hasa vijana. Waigizaji katika mchezo huo wamejulikana kutokana na mchezo huo, mmoja kati ya waigizaji ni Bw. Yu Entai.
v Mwongoza michezo ya kuigiza Li Guoxiu 2007/06/11
Katika siku za tamasha la "Kukutana Mjini Beijing" mchezo wa kuigiza wa Shamlet ulioongozwa na Bw. Li Guoxiu aliyetoka kisiwani Taiwan ulitimiza maonesho yake mara 100. Mchezo huo umewapatia watazamaji wa Beijing nafasi adimu ya kuufurahia mchezo wa kuigiza kutoka kisiwa cha Taiwan.
1 2 3 4 5 6 7 8 9