China yatangaza ripoti kuhusu hatua na sera za China katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa mwaka 2015
Kamati ya Taifa ya Maendeleo na Mageuzi ya China imetoa ripoti kuhusu hatua zilizochukuliwa na sera za China katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa kwa mwaka huu. Ripoti hiyo inasema, katika miaka mitano iliyopita, China imepata mafanikio makubwa katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa kupitia marekebisho ya mwundo wa viwanda, kubana matumizi ya nishati na kuinua ufanisi wake, kuongeza nishati safi na kupanda miti. Katika mkutano wa hali ya hewa utakaofanyika huko Paris, China iko tayari kushirikiana na pande mbalimbali kuhakikisha mkutano huo unafikia makubaliano yanayotarajiwa kwenye msingi wa haki na kanuni ya "wajibu mmoja majukumu tofauti".
|
China yapambana na bidhaa feki ili kulinda sifa ya "Made in China" Baada ya serikali ya China kutoa mpango wa kupambana na bidhaa feki zinazouzwa nje ya nchi, idara mbalimbali za China zimechukua hatua kwa pamoja za kupambana na bidhaa feki ili kulinda sifa ya "Made in China".
|
China kukuza utoaji mpya wa soko na msukumo mpya wa uchumi kutokana na mahitaji mapya ya matumizi Kamati ya maendeleo na mageuzi ya China leo imesema, ili kuhimiza mageuzi ya uchumi na kuongeza ufanisi wake, China itaharakisha maendeleo ya sekta ya utoaji huduma, kulingana na mahitaji mapya ya matumizi, ili kuendeleza utoaji mpya sokoni na kukuza msukumo mpya wa uchumi.
|
Mitaji ya nje inayowekezwa nchini China yaongezeka kwa utulivu katika miezi 10 iliyopita Katika miezi 10 iliyopita, mitaji ya kigeni inayowekezwa nchini China imeongezeka kwa utulivu, na imetumiwa zaidi kwenye sekta ya huduma za teknolojia ya juu na viwanda. Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, ingawa ongezeko la biashara ya China na nje limepungua, lakini China pia imedumisha nafasi yake ya kwanza kwa ukubwa wa biashara duniani.
|
Waziri mkuu wa China afanya mazungumzo na wataalamu na viongozi wa kampuni kubwa kuhusu hali ya uchumi ya sasa
Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang Jumatatu wiki hii amekutana na wataalamu na viongozi wa kampuni kubwa za China, na kusikiliza maoni na mapendekezo yao kuhusu hali ya uchumi ya sasa. |
|