• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • • Siku ni ya 13 kwenye mashindano ya olimpiki jijini London,Uingereza.Siku tatu zimesalia kabla kukamilika kwa mashindano hayo.
    Kamati ya kimataifa ya olimpiki(IOC) imesema haitachunguza ushindi wa mwanariadha Taoufik Makhloufi wa Algeria kwenye mbio za mita 1500 licha ya shaka ya kupata kwake nafuu kwa usiku mmoja. Makhloufi mwenye umri wa miaka 24 alishinda mbio hizo saa 24 baada ya kujiondoa chini ya mita 150 kwenye mbio za mchujo za mita 800.Mwanariadha huyo aidha aliondolewa kwenye olimpiki na shirikisho la kimataifa la vyama vya riadha(IAAF) kwa madai ya kutojituma kwenye mbio hizo.
    • Siku ni ya 12 ya mashindano ya olimpiki jijini London,Uingereza
    Maafisa wa timu ya olimpiki ya Cameroon wamesema wanamichezo saba wamepotea wakiwa nchini Uingereza kwa mashindano hayo.Mkuu wa timu hiyo, David Ojong ameongeza kuwa saba hao ambao walitoweka wikendi iliyopita ni pamoja na mabondia watano,muogeleji na mwanasoka wa kike.
    • Siku ya 11 kwenye mashindano ya olimpiki jijini London
    Raia wa nchi ya Greanada iliyoko kwenye visiwa vya Caribbean wameingia kwenye sherehe baada ya mwanariadha wa nchi hiyo,Kirani James kujinyakulia medali ya dhahabu kwenye mbio za mita 400 kwa wanaume.Waziri Mkuu wa nchi hiyo,Tillman Thomas amemtaja mwanariadha huyo kama mfano bora kwa vijana wa Grenada,nchi yenye idadi ya watu laki moja.
    • Siku ya nane ya mashindano ya olimpiki tuangazie yalojiri viwanjani
    Tuanze na riadha,kwenye mbio za mita 10000 kwa wanaume, Mo Farah wa Uingereza alijishindia nishani ya dhahabu, Galen Rupp wa Marekani akajibebea nishani ya fedha nae Bekele Tariku wa Ethiopia akavuna medali ya shaba.Mbio za mita 100 kwa kina dada zilishuhudia Shelly-Ann Fraser-Pryce na Veronica Campbell-Brown wa Jamaica wakijipatia nishani za dhahabu na shaba mtawalia.Aidha Carmelita Jeter wa Marekani akaridhika na nishani ya fedha.
    • Siku ya saba kwenye mashindano ya olimpiki jijini London Uingereza
    Tuanze na riadha ambapo mwanariadha Tirunesh Dibaba wa Ethiopia alijishindia nishani ya dhahabu kwenye mbio za mita 10000 kwa kina dada.Aidha wanariadha Sally Jepkosgei Kipyego na Vivian Jepkemoi Cheruiyot wa Kenya wakalazimishwa kuchukua medali za fedha na shaba mtawalia.
    • Siku ni ya nne kwenye mashindano ya olimpiki jijini London,Uingereza.Tutupe macho yetu viwanjani.
    Tuanze na ushindi mpya wa China kwenye mashindano hayo ambapo Ye Shiwen wa China alitia mkobani nishani yake ya pili ya dhahabu baada ya kushinda uogeleaji mita 200 medley kwa wanawake. Ye alishinda medali yake ya kwanza na kuandikisha rekodi mpya ya dunia kwenye uogeleaji mita 400 medley. Kwenye uogeleaji mita 200 medley,Alicia Coutts wa Australia alijipatia nishani ya fedha nae Caitlin Leverenz wa Marekani akaridhika na nishani ya shaba.
    • Ikiwa leo ni siku ya nne ya mashindano ya olimpiki jijini London,Uingereza
    Bondia Damien Hooper wa Australia hataaadhibiwa kwa kuvalia fulana yenye bendera ya kabila la Aborigin la nchini humo.Hooper alimshinda Marcus Browne wa Marekani;Mmarekani wa kwanza kushindwa kwenye michezo hiyo.Kamati ya kimataifa ya olimpiki(IOC) imesema haitamchukulia hatua bondia huyo ambaye alikashifiwa vikali na kamati ya olimpiki ya nchini mwake(AOC).Bondia huyo ameongeza kuwa hajali kama atawekewa vikwazo kwani anaona fahari kufanya kitendo hicho ambacho ni cha kutangaza mila zake.Aidha kitendo cha Hooper kinaweza kuchukuliwa kwenda kinyume na kanuni za olimpiki zinazowakataza wanamichezo kutoa matamshi ya kisiasa.
    • Uzinduzi wa mashindano ya Olimpiki utakuwa na mambo mengi ya kushangaza
    Siri kubwa ya mashindano ya Olimpiki kwa sasa ni jinsi gani uzinduzi wa mashindano hayo utafanyika, lakini kutokana na taarifa zilizotolewa na mamlaka ya Olimpiki na kwa kiasi fulani kuvujishwa na baadhi ya washiriki wa mashindano hayo, uzinduzi huo unatarajiwa kuwa wa kustaajabisha, huku ukiwa na vionjo vya kuwafurahisha watu kwa mtindo wa Uingereza.
    • Uteuzi wa kikosi cha Kenya kwenye Olimpiki
    Shangwe vifijo na nderemo vilitanda katika uwanja wa kimataifa wa nyayo jijini Nairobi wakati wa mashindano ya riadha ya kuteuliwa kwa kikosi kamili cha wanariadha watakaoiwakilisha Kenya kwenye mapambano ya Olimpiki yatakayoandaliwa London Uingereza kuanzia tarehe 27 Mwezi Juai Mwaka huu. Uteuzi huu uliwalazimu wanariadha wanaotaka kushiriki katika mbio za vitengo tofauti kukabiliana kufa kupona na wenzao kutoka hapa Kenya kabla ya kupata tiketi ya kuelekea Uingereza kwenye olimpiki ambayo ni ndoto ya kila mwanariadha kushiriki.
    • Magwiji wa marathon duniani
    Bendera ya Kenya inatarajiwa kupaa angani wakati wa kinyanganyiro cha mashindano ya olimpiki yatakayoandaliwa jijini la London nchini Uingereza mwezi Julai mwaka huu 2012 katika riadha hususan kwenye mbio za masafa ama Marathon. Hii ni kutokana na uzoefu mkubwa walionao wanariadha wa Kenya katika mashindano ya kimatiafa ya riadha kama vile mbio za Afrika IAAF,World Cross Country, na hata mashindano ya dunia ya Olimpiki yanayoandaliwa kila baada ya miaka 5..
    • Eldoret chimbuko la mabingwa wa wariadha duniani.
    Wanariadha walikimbia mapema asubuhi katika kambi ya riadha ya Iteen jijini Eldoret wakati wa mazoezi ya kujitayarisha kwenye mashindano ya olimpiki yatakayoandaliwa jijini London Uingereza mwaka huu wa 2012. Iten ni kambi ya wanariadha iliopo jijini Eldoret mji uliopata umaarufu mkubwa sana nchini Kenya na dunia nzima kwa kuwa chimbuko la wanariadha maarufu sana wa Kenya wanaotambuliwa ulimwenguni.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako