Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
 
  • China yaunga mkono ujenzi wa mradi wa utoaji wa maji nchini Cameroon
  •  2007/09/14
    Balozi wa China nchini Cameroon Bw. Huang Changqing na waziri wa uchumi na fedha wa Cameroon Bw. Polycarpe Abah, tarehe 30 mwezi Agosti huko Yaoundé walisaini makubaliano kuhusu China kutoa mkopo wa kiserikali wenye riba nafuu wa dola za kimarekani milioni 23 kwa Cameroon, ili kuunga mkono ujenzi wa mradi wa utoaji wa maji mjini Douala.
  • Hatua mbalimbali ilizoahidi China zainufaisha Afrika ya Kusini
  •  2007/08/17
    Mwandishi wetu wa habari hivi karibuni alifahamishwa kuwa, hatua nane ilizoahidi China kwenye mkutano wa wakuu wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika mwezi Novemba mwaka 2006 hapa Beijing zinatekelezwa kwa utaratibu, utekelezaji wa hatua kadhaa umezinufaisha kidhahiri sekta mbalimbali nchini Afrika ya Kusini.
  • Ushirikiano kati ya China na Afrika una manufaa halisi kwa waafrika
  •  2007/08/03
    Kwenye ufunguzi wa mkutano wa wakuu wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika hapa Beijing mwezi Novemba mwaka jana, rais Hu Jintao wa China alitoa hatua nane za kusukuma mbele maendeleo ya uhusiano wa aina mpya wa kiwenzi na kimkakati kati ya China na Afrika.
  • China na Kenya zana fursa nyingi za ushirikiano katik sekta ya nishati ya jua
  •  2007/07/20
    Suala la nishati ni suala linalozingatiwa duniani siku zote. Hivi sasa soko la kimataifa la nishati lina mabadiliko makubwa, mapambano ya kugombea nishati yanazidi kuwa makali, na tatizo la usalama wa nishati limetokea, hivyo kuendeleza matumizi ya nishati endelevu kumekuwa ni sehemu muhimu ya mkakati wa maendeleo kwa nchi nyingi
  • Mkutano wa kwanza wa baraza la "kushirikiana na nchi za Afrika ili kupata maendeleo ya pamoja"
  •  2007/07/06
    Kwenye mkutano wa kwanza wa baraza la "kushirikiana na nchi za Afrika ili kupata maendeleo ya pamoja" uliofanyika tarehe 30 Juni hadi tarehe 1 Julai huko Nanjing, mwandishi wa habari wetu alifanya mahojiano na Bw. Joseph Wolukau, mwanafunzi anayefanya utafiti na kujitahidi kupata shahada ya juu kwenye kituo cha utafiti wa kilimo ya Afrika cha chuo kikuu cha kilimo cha Nanjing mkoani Jiangsu, China, ambaye alikuwa mwalimu wa chuo kikuu cha Egerton cha Kenya.
  • Benki ya China yapata mafanikio barani Afrika
  •  2007/06/29
    Miaka kumi iliyopita, benki ya China ilifungua tawi lake huko Lusaka, mji mkuu wa Zambia, na kuwa tawi la kwanza la benki ya China barani Afrika. Lakini kutokana na shughuli za kiuchumi za Zambia siyo nyingi na kutokuwepo kwa mazingira mazuri ya biashara, kabla ya mwaka 2003 benki hiyo iliendeshwa kwa hasara.
  • "Darasa la matangazo la Confucius" laanzishwa huko Nairobi Kenya
  •  2007/06/15
    "Darasa la matangazo la Confucius" limezinduliwa rasmi asubuhi ya tarehe 8 Juni huko Nairobi, Kenya. Darasa hilo lilianzishwa kwa ushirikiano kati ya Ofisi ya kikundi cha uongozi wa kazi ya uenezaji wa lugha ya Kichina cha taifa la China na Radio China Kimataifa.
  • Wachina barani Afrika
  •  2007/05/25
    Hivi sasa uhusiano kati ya China na Afrika unaendelezwa kwa kasi. Baada ya rais Hu Jintao wa China kufanya ziara barani Afrika mara mbili, na waziri mkuu wa China Bw. Wen Jiabao kufanya ziara barani Afrika mwezi June mwaka jana, tarehe 15 mwezi Aprili mwaka huu, mwenyekiti wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China Bw. Jia Qinglin aliondoka kutoka hapa Beijing na kufanya ziara nchini Tunisia, Ghana, Zimbabwe na Kenya.
  • Wakulima wa China waanzisha shamba la kilimo nchini Sudan
  •  2007/05/11
    Sudan ni nchi iliyoko kaskazini mashariki mwa bara la Afrika, lakini wachina wote wa huko wanaweza kupata mboga za kichina, hali hii inatokana na wakulima wa China waliokwenda Sudan kufanya shughuli za kilimo kuanzia miaka ya 90 ya karne iliyopita. Katika nchi hiyo yenye joto kabisa duniani, wachina hao wanajishughulisha na kilimo kwa juhudi na kuwatosheleza mboga wachina wanaofanya kazi nchini Sudan pamoja na wasudan.
  • Mabasi ya abiria yaliyotengenezwa na China yakaribishwa na Zimbabwe
  •  2007/05/04
    Katika siku za karibuni Zimbabwe ilitangaza kuwa mwaka huu itanunua mabasi ya abiria 245 kutoka China, yakiwemo mabasi kadhaa ya kiwango cha juu yatakayotumika kwa safari ndefu. Hayo ni mabasi mengi zaidi kuliko yale ya mwaka 2005, wakati China ilipoiuzia Zimbabwe mabasi 50 ya abiria.
    1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11