Thamani ya uwekezaji ya China barani Afrika yazidi Dola za kimarekani bilioni moja 2005/09/30 Kwenye ufunguzi wa maonesho ya biashara na uwekezaji kati ya China na Afrika, naibu mkuu anayeshughulikia mageuzi ya kiuchumi wa kamati ya maendeleo na mageuzi ya China Bwana Li Haiyan alisema kuwa, katika miaka ya karibuni makampuni ya China yamewekeza miradi katika nchi 49 za Afrika, ambapo thamani ya uwekezaji huo imezidi dola za kimarekani bilioni moja.
|
Wafanyabiashara binafsi wa China wanaojiendeleza katika nchi za Afrika 2005/09/16 Tangu China ianze kufanya mageuzi na kufungua mlango, maingiliano ya kiuchumi na kibiashara kati yake na nchi za Afrika yanaimarika siku hadi siku. Serikali ya China inawahimiza wanakampuni na wafanyabiashara wa China kuwekeza barani Afrika, ambao pia wanakaribishwa sana na nchi za Afrika kuwekeza vitega uchumi barani humo, ili kuhimiza maendeleo ya uchumi wa huko.
|
China kuchukua hatua kuhimiza kuagiza bidhaa kutoka Kenya 2005/08/26 Katika miaka kumi iliyopita, ushirikiano wa uchumi na biashara kati ya China na Kenya umepata maendeleo makubwa. Lakini kutokana na miundo tofauti ya kiuchumi, hivi sasa bado kuna pengo kubwa la biashara kati ya nchi hizo mbili.
|
Kampuni ya Betri ya Anyang mkoani Henan yaendeleza shughuli zake barani Afrika 2005/07/08 Betri za chapa ya "kifaru" zilizotengenezwa mjini Anyang mkoani Henan, China zimeingia kwenye soko la Kenya na kuhusiana na maisha ya kila siku ya wakenya.
|
Afrika yatumai kuimarisha ushirikiano ya madini kati yake na China 2005/06/03 Afrika ni bara lenye maliasili nyingi, uwingi wake wa madini unachukua nafasi ya kwanza katika mabara yote duniani. Mwezi Februari mwaka 2004, mawaziri wa madini wa nchi 28 za Afrika zikiwemo Afrika Kusini, Ghana, Msumbiji, Sudan, Misri, Namibia, Botswana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kong, walikutana huko Cape Town, kwenye mkutano wa 9 wa uendelezaji wa kazi za madini barani Afrika.
|
Shirika la Kilimo la China kushughukia mashamba nchini Zambia 2005/04/22 Shirika la Kilimo la China ni shirika kubwa linalomilikiwa na taifa la China. Mwaka 1990, shirika hilo lilinunua shamba lake la kwanza nchini Zambia, lililoko kilomita 20 magharibi mwa Lusaka mji muku wa nchi hiyo. Shamba hilo lenye eneo la hekta 667 sasa linajulikana kama Shamba la Urafiki kati ya China na Zambia. Kwa Shirika la Kilimo la China, shamba hilo ni hatua yake ya kwanza katika kuanzisha shughuli nchini Zambia, na uzoefu uliopatikana katika shamba hilo limenufaisha sana shughuli za baadaye.
|
Mashirika ya viatu ya Guangdong kuanzisha shughuli katika nchi za Afrika na mashariki ya kati 2005/04/15 Tarehe 15, Mwezi Machi, mwaka 2005, Shirikisho la Afrika na Sehemu ya Mashariki ya kati la biashara na China na Shirikisho la wafanyabaishara wa viatu la Huizhou mkoani Guangdong yalisaini makubaliano kuhusu "Mradi wa bilioni 10". Kutokana na makubaliano hayo, Shirikisho la Afrika na sehem ya Mashariki ya kati la biashara na China litatoa misaada mbalimbali kwa mashirika ya viatu ya Huidong.
|
Nchi za Asia na Afrika zataka kuanzisha uhusiano wa wenzi wa kimkakati 2005/04/15 Naibu waziri wa mambo ya nje wa Afrika ya Kusini jana alisema kuwa, bara la Afrika ambalo liko nyuma kabisa kiuchumi duniani linataka kuanzisha uhusiano wa wenzi wa kimkakati na bara la Asia ambalo uchumi wake unaendelea haraka, ili kubadilishana uzoefu wa maendeleo na kujenga kwa pamoja siku za usoni zenye wenye utulivu na ustawi.
|
Mawasiliano na ushirikiano kati ya China na Afrika kupata maendeleo mazuri 2005/03/25 Ushirikiano katika kilimo kati ya China na Afrika unachukua nafasi muhimu katika mkakati wa kuhimiza kampuni za China kuanzisha shughuli katika nchi za nje. Tangu yaanzishwe mageuzi na ufunguaji mlango, China imekuwa ikifanya mawasiliano na ushirikiano na nchi za Afrika. Katika miaka ya hivi karibuni, maofisa wa ngazi ya juu wa Wizara ya kilimo ya China na idara za kilimo za Afrika wanawasiliana zaidi.
|
Wafanyabiashara wa China wanaoanzisha kituo cha biashara cha China nchini Afrika kusini. 2005/03/11
Katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na maendeleo ya kasi ya uchumi wa China, serikali ya China inahamasisha makampuni na matajiri wa China kwenda nchi za nje kuwekeza vitega uchumi. Hivyo wachina wanaoanzisha shughuli zao nchi za nje wanaongezeka siku hadi siku.
|