Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
 
  • Watu wengi duniani waendelea kujifunza lugha ya Kichina
  •  2006/07/26
    Katika hali ya kawaida lugha ya kiingereza ni chaguo la kwanza kwa watu wengi wanaotaka kujifunza lugha ya kigeni, na hivi sasa kiingereza bado ni lugha muhimu ya kimaitaifa. Lakini pamoja na kuinuka kwa uchumi na hadhi ya China duniani, watu wengi duniani wameanza kujifunza lugha ya kichina kama lugha ya pili.
  • Idadi ya watu wanaojifunza kichina katika nchi za nje yaongezeka siku hadi siku
  •  2006/07/19
    Confucius alikuwa mwanafalsafa, mwanasiasa na mwelimishaji maarufu wa China. Hadi sasa vyuo vilivyopewa jina la Confucius vimeanzishwa katika nchi na sehemu 36 duniani, na idadi yake imefikia 80. Kwenye Mkutano wa kwanza vya vyuo vya Confucius, wajumbe 400 kutoka nchi na sehemu 38 duniani walijadili kwa pamoja ufundishaji wa lugha ya kichina duniani. Mjumbe wa taifa wa China Bibi Chen Zhili alisema, kadiri China na nchi mbalimbali duniani zinavyozidi kuwasiliana, ndivyo lugha ya kichina inavyozidi kutumiwa na kufuatiliwa zaidi.
  • Kampuni ya Mcmillan nchini Kenya
  •  2006/07/12
    Kampuni ya Mcmillan nchini Kenya ilianza 1971, ikiwa ni kituo cha usambazaji wa vitabu vya kampuni kubwa ya Mcmillan duniani, hivi sasa imekuwa kampuni kubwa ya kitaalamu kwa uchapishaji nchini Kenya.
  • Jamii inapaswa kufanya juhudi kuwaepusha watoto wasiathiriwe na dawa za kulevya
  •  2006/07/05
    Tarehe 26, Juni ni Siku ya 19 ya kupambana na dawa za kulevya duniani, na kauli mbiu ya mwaka huu ni "dawa za kulevya si mchezo wa kujiburudisha kwa watoto". Je, ni kwa nini kauli mwaka huu inafuatilia matumizi ya dawa za kulevya kwa watoto? Je hali ya hivi sasa ya mapambano dhidi ya dawa za kulevya kwenye sehemu ya Asia na Pasifiki ikoje? Mwandishi wetu wa habari alimhoji Bw. Akira Fujino ambaye ni mkuu wa Kituo cha Asia Mashariki na sehemu ya Pasifiki kwenye Ofisi ya udhibiti wa dawa za kulevya na kudhibiti uhalifu ya Umoja wa Mataifa.
  • Ujenzi wa reli ya Qinghai-Tibet
  •  2006/06/28
    Reli ya kutoka mkoa wa Qinghai hadi mkoa wa Tibet iliyojengwa kwenye uwanda wa juu wa Qinghai na Tibet wenye mwinuko mkubwa zaidi kutoka usawa wa bahari duniani itaanza kufanya kazi tarehe 1, Julai mwaka huu. Kutokana na matatizo ya "kuganda kwa udongo", na "upungufu wa oksijeni kwenye uwanda wa juu", wataalamu wa nchi za nje waliona kuwa haiwezekani kujenga reli kwenye uwanda wa juu wa Qinghai-Tibet, lakini wachina waliondoa matatizo mbalimbali na kufanikiwa kujenga reli hiyo kwenye uwanda wa juu wenye mwinuko mkubwa zaidi duniani.
  • bidhaa za teknolojia zaongoza maisha mapya
  •  2006/06/21
    Bila shaka mmewahi kufikiria kuwa wakati michezo ya Olimpiki ya Beijing itakapofanyika mwaka 2008, kabla ya kuondoka nyumbani mnaweza kupata taarifa za moja kwa moja kuhusu mawasiliano barabarani kwenye mtandao wa Internet, na kuchagua njia bora ya kwenda kwenye uwanja fulani wa michezo; katika mapumziko ya adhuhuri, utaweza kupata habari za michezo kwenye simu ya mkononi na kuhifadhi matangazo ya moja kwa moja ya michezo kwenye simu yako?
  • Magari yanayotumia nguvu ya betre yakuwa karibu nasi
  •  2006/06/21
    Endapo unatembelea miji ya China, pengine bas unayopanda, ambayo inaonekana ni ya kawaida, lakini bas hiyo huenda ni bas inayotumia nguvu ya betre, na magari ya aina hiyo yanayotumia nguvu ya betre yanachukuliwa kuwa ni magari ya siku za baadaye.
  • Mahojiano kati ya mwandishi wetu wa habari na Bw. Silverse Anami wa Kenya
  •  2006/06/14
    Kenya ina lengo la kuwahamasisha wakenya wote kulinda utamaduni wetu. Wakoloni walileta utamaduni tofauti, kama dini tofauti, lugha tofauti na mambo mengi tofauti, hivyo ni lazima kwa serikali kurudisha na kulinda vizuri utamaduni wetu wenyewe.
  • Wanafunzi milioni 9.5 washiriki kwenye mitihani ya kujiunga na vyuo vikuu nchini China
  •  2006/06/14
    Wanafunzi milioni 9.5 walishiriki kwenye mitihani ya kujiunga na vyuo vikuu iliyofanyika kuanzia tarehe 7 hadi 9 Juni nchini China, ili kuwania nafasi milioni 5.3 zinazotolewa na vyuo vikuu mbalimbali. Katika siku ya kwanza ya mitihani hiyo, mwandishi wetu wa habari alikwenda kwenye kituo cha mitihani kilichoko kwenye mtaa wa Shijingshan hapa Beijing, ambapo aliona wanafunzi wengi wakiwa wamekusanyika.
  • Mtihani wa kiwango cha lugha ya kichina HSK
  •  2006/05/31
    Hivi sasa, wanafunzi wengi wa nchi za nje wanaosoma nchini China wanafanya juhudi za kuinua kiwango chao cha lugha ya kichina, ili kufanya maandalizi kwa ajili ya HSK---"Mtihani wa kiwango cha lugha ya kichina"  utakaofanyika miezi michache ijayo katika sehemu mbalimbali nchini China. Katika miaka ya hivi karibuni, watu wengi wa nchi za nje wamekuwa wakiufahamu mtihani huo, na baadhi ya watu wanaufahamisha na mtihani wa TOFEL.
    1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16