• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • • fainali iliyochezwa jana jumapili kwa huko Brazil
    Wiki iliyopita katika kipindi hiki cha Jamvi uchambuzi wa timu zinazocheza kombe la dunia nchini Brazil, tulizizungumzia timu za taifa za nchi zilizoingia hatua ya robo fainali na vile vile tukachambua kwa upana mechi za nusu fainali ambapo tulisema tulishuhudia maangamizi makubwa kwa Brazil ilipofungwa na Ujerumani. Pia tuliizungumzia Uholanzi ambayo nayo ilitolewa ingawa kwa taabu na Argentina na kupelekea mechi ya fainali kuvaana miamba miwili kutoka Amerika Kusini Argentina na Ulaya Ujerumani
    • Timu zilizoingia nusu fainali
    Wiki iliyopita katika kipindi hiki cha Jamvi uchambuzi wa timu zinazocheza kombe la dunia nchini Brazil, tulizizungumzia timu za taifa za nchi mbili za Afrika zilizoshiriki michuano hiyo hadi hatua ya mtoano. Timu hizo ni Nigeria na Algeria. Na vile vile tukaona jinsi zilivyofanya kwenye hatua hiyo, ambapo tulisema Algeria ilitolewa lakini ilijikaza kiume baada ya kufungwa na Ujerumani kwa mabao 2-1.
    • Soka labadilisha maisha ya watoto wa mtaani nchini Brazil
    Wakati kombe la dunia la Brazil linapopamba moto na kuingia nusu fainali, mbali na kufuatilia matokeo ya mechi, tuangalie jinsi soka linavyobadilisha maisha ya watu hasa watoto katika nchi hiyo inayojulikana kwa soka.
    • Hatua ya mtoano kwa Algeria na Nigeria
    Wiki iliyopita katika kipindi hiki cha Jamvi uchambuzi wa timu za Afrika zinazocheza kombe la dunia nchini Brazil, tulizizungumzia timu za taifa za nchi zote tano zinazoshiriki michuano hiyo. Na vile vile tukaona nchi gani iliyoingia hatua ya mtoano na ipi iliyofungasha virago baada ya mechi za hatua ya makundi. Jumla ya nchi tatu zilitolewa katika hatua ya awali au ya makundi zikiwemo Ghana, Ivory Coast na Cameroon. Na nchi mbili zilizoendelea mbele katika hatua ya mtoano zilikuwa ni Algeria na Nigeria, sasa leo hii tutazungumzia hatua ya mtoano ilikuwa vipi kwa nchi hizo mbili.
    • Nchi zenye nafasi ya kuendelea mbele kwenye hatua ya mtoano

    Wiki iliyopita katika kipindi hiki cha Jamvi uchambuzi wa timu za Afrika zinazocheza kombe la dunia nchini Brazil, tulizizungumzia timu za taifa za nchi zote tano zinazoshiriki michuano hiyo. Na vile vile tukaona nchi gani iliyofanya vizuri au kujitahidi lakini pia tulizungumzia nchi zile zilizofanya vibaya na ambazo zilikuwa hatarini kufungashwa virago kwenye michuano hii. Na leo hii pia tutaendelea kuzijadili nchi hizo na kujua zipi zenye nafasi ya kuendelea mbele kwenye hatua ya mtoano na zipi zilizofurushwa kwenye michuano hiyo.

    • uchambuzi wa timu nyingine mbalimbali za Afrika zilizocheza wiki nzima
    Wiki iliyopita katika kipindi hiki cha Jamvi uchambuzi wa timu za Afrika zinazocheza kombe la dunia nchini Brazil, tuliizungumzia timu ya taifa ya Brazil na Croatia ambazo zilicheza Alkhamis iliyopita siku ya ufunguzi wa kombe hili ambapo Brazil iliifunga Croatia kwa mabao 3-1. na leo hii tunaendelea na uchambuzi wa timu nyingine mbalimbali za Afrika zilizocheza wiki nzima.
    • Uchambuzi wa timu ya Brazil na Croatia
    •  Timu ya Brazil ambayo ni waandaaji wa kombe la dunia
    Wiki iliyopita katika kipindi hiki cha Jamvi uchambuzi wa timu za Afrika zitakazocheza kombe la dunia mwezi ujao nchini Brazil, tuliizungumzia timu ya taifa ya Aljeria au "Mbweha wa Jangwani" jinsi ilivyoweza kufuzu michezo ya safari hii na jinsi ilivyofanya vibaya katika michuano ya kombe la dunia iliyopita. Bila kusahau mechi mbalimbali ilizoshiriki katika michuano mbalimbali duniani.
    • Uchambuzi wa timu ya Ghana
    Wiki iliyopita katika kipindi hiki cha Jamvi uchambuzi wa timu za Afrika zitakazocheza kombe la dunia mwezi ujao nchini Brazil, tuliizungumzia timu ya taifa ya Nigeria "Super Eagle" jinsi ilivyoweza kufuzu michezo ya safari hii na jinsi ilivyofanya vibaya katika michuano ya kombe la dunia mwaka 2002 kule Korea kusini na Japan na mwaka 2010 kule Afrika Kusini...
    • Kombe la dunia Fifa Brazil World Cup 2014
    Wiki iliyopita katika kipindi hiki cha Jamvi uchambuzi wa timu za Afrika zitakazocheza kombe la dunia mwezi ujao nchini Brazil, tuliizungumzia Ivory Coast ama "Tembo wa Afrika" jinsi ilivyoweza kufuzu michezo ya safari hii na jinsi ilivyofanya katika michezo ya dunia kule nchini Ujerumani na Afrika Kusini. Pia tulisema kuwa ni timu ambayo haijavuka hatua ya makundi katika safari zake zote mbili ilizoshiriki michuano hii mikubwa na mafanikio mbalimbali iliyopata katika michuano mbalimbali duniani.
    • Timu za Afrika zinazoshiriki kwenye kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazil
    Wiki iliyopita tuliizungumzia timu ya taifa ya Cameroon ambayo maarufu inajulikana kama "The Indomitable Lions", tulisema kuwa ni timu pekee iliyoitoa kimasomaso Afrika na kufika kwenye hatua ya fainali katika kombe la dunia. Pia kwa mara ya kwanza iliingia katika kombe la dunia mwaka 1982.
    • Bara la Afrika kuwakilishwa na timu 5 kwenye kombe la Dunia
    Bara la Afrika safari hii litawakilishwa na timu 5 kwenye kombe la Dunia huko Brazil. Timu hizo ni pamoja na Aljeria, Nigeria, Ghana, Ivory Coast na Cameroon. Timu ya taifa ya Cameroon almaarufu kama "The Indomitable Lions" ni miongoni mwa nchi zilizofuzu kucheza kombe la dunia mwaka huu huko Brazil, na imeshiriki mara 6 kwenye kombe hilo, haijawahi kushinda taji hili, pia iko katika nafasi ya 50 kwenye viwango vya FIFA
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako