• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • • China yamejenga mtandao mkubwa zaidi ya habari na mawasiliano duniani
     2019-09-20

    Waziri wa viwanda na habari wa China Bw. Miao Wei, leo hapa Beijing amesema katika muda miaka 70 iliyopita tangu Jamhuri ya Watu wa China ianzishwe, China imejenga mtandao mkubwa zaidi wa habari na mawasiliano duniani, na hivi sasa China inashika nafasi ya kwanza duniani kwa hataza za lazima za mtandao wa 5G, na mwakani itaanza rasmi kutoa huduma za mtandao huo katika sehemu mbalimbali nchini China.

    • China yatoa waraka kuhusu maendeleo ya mambo ya wanawake
     2019-09-19

    Ofisi ya habari ya baraza la serikali la China leo imetoa waraka kuhusu mambo ya wanawake, na kueleza mafanikio yaliyoipata China katika kuendeleza mambo ya wanawake katika miaka 70 iliyopita tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China.

    • China yakamilisha kimsingi mtandao wa kisasa wa posta
     2019-09-17

    Mkuu wa idara kuu ya posta ya China Bw. Ma Junsheng leo hapa Beijing amesema, katika miaka 70 iliyopita tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China, huduma za posta nchini China zimekua kwa mara 7,700, na China imekamilisha kimsingi mtandao wa kisasa wa posta.

    • China yatarajia kutimiza lengo la maendeleo ya uchumi
     2019-09-16

    Idara kuu ya takwimu ya China leo imetangaza takwimu ya maendeleo ya sekta muhimu za kiuchumi zikiwemo viwanda, matumizi na uwekezaji katika mwezi wa Agosti. Msemaji wa idara hiyo Bw. Fu Linghui amesema, katika mwezi uliopita, kwa ujumla uchumi wa China umedumisha mwelekeo mzuri wa maendeleo, na China ina msingi, mazingira na imani katika kutimiza lengo lake la kiuchumi kwa mwaka huu.

    • China kujenga mji wa Shenzhen kuwa eneo la kielelezo cha ujamaa wenye umaalum wa China
     2019-08-22

    Serikali ya China imetoa waraka wa kuunga mkono kuujenga mji wa Shenzhen kuwa eneo la kielelezo cha ujamaa wenye umaalum wa China, na kuutaka mji huo kuhimiza ujenzi wa eneo kubwa la ghuba ya Guangdong, Hong Kong na Macao.

    • Juhudi za China katika kutokomeza umaskini uliokithiri zaonyesha mafanikio 2019-08-21

    Tangu sera ya mageuzi na kufungua mlango ilipoanza kutekelezwa mwishoni mwa mwaka 1978, China imepata mafanikio makubwa katika kupunguza umaskini. Kwa mujibu wa vigezo vya kimataifa vya kupunguza umaskini, idadi ya watu wa China wanaokumbwa na umaskini imepungua kwa kiasi kikubwa.

    • China kupanua masoko ya vijijini 2019-08-05
    Mkutano wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) kuhusu kazi za uchumi kwa nusu ya pili ya mwaka huu uliofanyika wiki iliyopita umetaka kupanua soko katika sehemu za vijijini. Wasomi nchini China wanasema, wakati China inapopanua mahitaji ya ndani ya nchi, hadhi ya masoko ya vijijini imeanza kuzingatiwa zaidi.
    • Uvumbuzi wa sayansi na teknolojia zaelekeza maendeleo yenye sifa bora ya Beijing 2019-04-08
    Uchumi wa China umebadilika na kupata maendeleo yenye sifa bora kutoka katika kipindi cha ongezeko la kasi katika miaka ya hivi karibuni. Hivi sasa maendeleo yenye sifa bora yamekuwa na umaalumu muhimu kwa maendeleo ya Beijing, na uvumbuzi wa sayansi na teknolojia umekuwa msingi muhimu.
    • Waziri mkuu wa China asisitiza kulegeza masharti ya uwekezaji kwa wawekezaji wa kigeni 2019-03-28
    Sherehe ya ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka 2019 wa Baraza la Asia la Boao umefanyika mkoani Hainan leo asubuhi. Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang akihutubia mkutano huo amesisitiza kuwa, China itatangaza sheria na kanuni mapema kuhusu uwekezaji kutoka nje, kuzidi kulegeza masharti ya uwekezaji kwa wawekezaji wa kigeni, na kuendelea kupanua ufunguaji mlango katika sekta ya fedha.
    • China kuhimiza ufunguaji mlango katika kiwango cha juu na maendeleo ya uchumi yenye ubora zaidi 2019-03-26

    Mkutano wa kwanza wa Baraza la ngazi ya juu la Maendeleo la China umefungwa jana mjini Beijing. Maofisa wa idara mbalimbali za serikali ya China waliohudhuria mkutano huo wameonesha ishara wazi kwamba, China itahimiza kwa hatua madhubuti sera ya kufungua mlango kwenye kiwango cha juu zaidi, na maendeleo yenye ubora zaidi ya uchumi, ili kuzifanya nchi mbalimbali zinufaike zaidi kutokana na soko kubwa la China.

    • China yapiga hatua katika kubana matumizi ya maji
     2019-03-22

    Leo ni siku ya maji duniani. China ina idadi kubwa ya watu na maliasili chache ya maji, hivyo inatekeleza mfumo mkali wa kudhibiti matumizi ya maji. Naibu waziri wa maji na umwagiliaji wa China Bw. Wei Shanzhong amesema, China imepiga hatua chanya katika kuhimiza kubana matumizi, kuhifadhi na kusimamia maliasili ya maji, huku ikiharakisha kushughulikia suala la matumizi ya kupita kiasi ya maji yaliyoko chini ya ardhi katika sehemu ya kaskazini.

    • Huu ni mwaka muhimu kwa China kushinda vita dhidi ya umaskini
     2019-03-20

    Mikutano ya Bunge la Umma na Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China iliyofungwa wiki iliyopita imedhihirisha majukumu mapya ya mwaka huu ya watu wa China. Kati ya majukumu hayo, kushinda vita dhidi ya umaskini ni muhimu sana. Wakati wa mikutano hiyo, rais Xi Jinping alitaja suala la umaskini mara nyingi, na kusisitiza kuwa imebaki miaka mwili tu kabla ya kufikia mwaka 2020, ambao ni mwaka wa kutimiza lengo la kuondoa umaskini nchini China, hivyo sasa ni wakati muhimu, na inapaswa kufanya juhudi kadiri iwezekanavyo hadi kupata ushindi wa mwisho.

    • China kuongeza ushirikiano wa kibiashara katika ujenzi wa pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja"
     2019-03-18

    Katika miaka 6 tangu China itoe pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja", miradi mingi imetekelezwa katika nchi zilizojiunga na pendekezo hilo. Miradi hiyo imehimiza maendeleo ya uchumi wa nchi hizo, na pia kuzisaidia kuongeza uwezo wa kupata maendeleo zaidi. Katika siku zijazo, China itaongeza ushirikiano wa kibiashara katika miradi mikubwa ya pendekezo hilo.

    • Waziri mkuu wa China aonesha imani kubwa kuhusu uchumi wa China katika siku za baadaye 2019-03-15
    Mkutano wa Pili wa Bunge la Awamu ya 13 la Umma la China uliofungwa leo mjini Beijing umepitisha ripoti ya kazi ya serikali ya awamu hiyo, na sheria ya uwekezaji wa kigeni inayolenga kuhimiza ufunguaji mlango katika kiwango cha juu zaidi. Katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika baada ya kumaliza kwa mkutano huo, waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang ameeleza kuwa, China itafuata hali ilivyo hivi sasa, kutupia macho siku za baadaye, kudumisha ongezeko lenye utulivu la uchumi na mwelekeo mzuri wa ongezeko hilo.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako