Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia

  • Mchoraji Chen Zhizhuang
  •  2005/08/01
    Marehemu Chen Zhizhuang ni mchoraji aliyejulikana baada ya kufariki dunia. Alizaliwa mwaka 1913 na kufariki dunia mwaka 1976 katika wilaya ya Rongchang mkoani Sichuan. Wakati alipokuwa hai, alikuwa anaitunza familia yake yenye watu 7 kwa mashahara wake mdogo aliokuwa akilipwa kutoka kwenye jumba la utamaduni na historia la Sichuan.
  • Bingwa Mzee aliyevuka karne tatu
  •  2005/06/10
    Msanii mkubwa Bwana Liu Haisu, ni mwanzilishi wa elimu ya uchoraji wa kisasa wa China, alizaliwa mwezi Machi, 1896, huko mjini Changzhou, mkoani Jiangsu. Bw. Liu alianza kujifunza uchoraji tangu alipokuwa mtoto na alionekana mwenye kipaji.
  • Mchoraji maarufu Huang Zhou
  •  2005/05/20
    Huang Zhou ni mchoraji hodari wa picha za watu na wanyama. Michoro yake inayowapa watazamaji kumbukumbu nzuri ni ile inayoonyesha mila na desturi za wenyeji wa Xinjiang.
  • Ndege wa Vichakani
  •  2005/04/01
        Picha ndefu ya kuviringisha "NDEGE WA VICHAKANI" iliyochorwa kwenye karatasi ina urefu wa sentimita 34 na upana wa sentimita 1121.2. Katika picha ndefu za kuviringisha zilizochorwa mnamo Enzi ya Ming, ni nadra kwa picha ndefu kama hiyo kuonekana. Picha hiyo ni picha bora miongoni mwa picha za mchoraji Lin Liang zilizopokewa kizazi hadi kizazi.
  • Picha za kuchora za Li Qi
  •  2005/03/18
        Li Qi ni profesa wa Chuo Kikuu cha Uchoraji , aidha ni mchoraji maarufu wa sura za watu. Picha nyingi zaidi alizochora zinahusu watu mashuhuri wa zama zetu na vilevile nyingine zinahusu wafanyakazi, wakulima, askari na wasomi. Yeye anachora sura hizo za watu juu ya karatasi za Xuan (aina ya karatasi bora zilizotengenezwa Xuancheng jimboni Anhui) kwa kutumia nguvu ya brashi na kuonyesha tena mioyo ya binadamu, ili kuchechemua akili na tabia za watazamaji.
  • Michoro ya Milima na Mito
  •  2005/01/21
        Picha za kuchora za milima na maji ni moja ya michoro ya Kichina, ambazo ni picha zenye maudhui ya milima, mito na mandhari ya kimaumbile. Picha za aina hiyo zilikuwa zinaendelea polepole wakati wa enzi za Wei, Jin na Enzi sita ( yaani Enzi ya Wu 222-280, Enzi ya Jin ya Mashariki 317-420, Enzi ya Song 420-479, Enzi ya Qi 479-502, Enzi ya Liang 502-557 na Enzi ya Chen 557-589 ), kwa wakati huo milima na mito ilikuwa mingi zaidi, sehemu zenye mandhari nzuri na milima na mito ilikuwa ya kupendeza sana, hasa katika kipindi cha ustawi cha Enzi ya Tang, kwa kuwa amani ilidumu kwa miaka mingi, wachoraji walipata wakati wa kuchora picha hizo za kuonesha mazingira ya maumbile.
  • Michoro ya kijadi ya China
  •  2004/08/06
    Michoro ya kijadi ya mwaka mpya ya China huwa na maudhui ya mfalme wa kuku kuimarisha nyumba. Inasemekana kwamba Mfalme Yao aliposhika hatamu, dola moja ndogo ilimtunukia Ndege wa Zhongming, sura yake ilifanana na kuku, na kulia kama Phoenix. Aliweza kupigana na wanyama wakali na kuweza kuwafanya jini kutothubutu kuwaletea madhara binadamu. Ndege hao walikwenda na kurudi mara kwa mara, walipokuja walikaribishwa kwa kusafisha nyua za watu na walipoondoka, watu walichongachonga sanamu yake ya mbao na dhahabu, na kuweka mlangoni ili kuwaogofya majini.
  • Michoro ya wanawake wa Ansai
  •  2004/08/05
        Ansai, jimboni Shaanxi iko katika ukanda wa chimbuko la utamaduni nchini China, yapo masalia mengi ya kale na mila chache za kikale. Wanawake wanaoishi sehemu hiyo wote wana maarifa ya sanaa za kukata karatasi, kutarizi na kufinyanga. Lakini wanavyojua zaidi ni kuchora michoro.
  • Michoro ya rangi ya maji
  •  2004/07/29
    Michoro ya rangi ya maji nchini China ilitoka Ulaya karibu miaka 100 iliyopita. Katika kipindi kirefu, michoro hiyo ambayo ni aina ndogo ya sanaa ya uchoraji haikuwa na wachoraji maarufu. Miaka ya karibuni kwa sababu ya mageuzi na mlango wazi, watu wanapanua shauku zao, na hivyo homa ya michoro ya rangi ya maji imetokea polepole. Maonyesho ya 6 ya sanaa ya taifa ya mwaka 1984 na maonyesho ya 7 ya mwaka 1989 yalikuwa na sehemu yake pekee ya michoro ya rangi ya maji. Michoro ya aina hiyo ya wasanii wa China pia imekwenda nchi za nje na kusifiwa huko Japani, Marekani na nchi za Ulaya Kaskazini.
  • Michoro ya Kuku
  •  2004/03/28

    Michoro ya kijadi ya mwaka mpya ya China huwa na maudhui ya mfalme wa kuku kuimarisha nyumba. Inasemekana kwamba Mfalme Yao aliposhika hatamu, dola moja ndogo ilimtunukia Ndege wa Zhongming, sura yake ilifanana na kuku, na kulia kama Phoenix. Aliweza kupigana na wanyama wakali na kuweza kuwafanya jini kutothubutu kuwaletea madhara binadamu.

    More>>
    More>>