Waziri wa mambo ya nje wa China asema China itaendelea kuzisaidia nchi za Afrika bila ya kujali mwenendo wa uchumi wa dunia Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi ameongea na waandishi wa habari kutoka nchi mbalimbali kando ya Mkutano wa bunge la umma la China unaoendelea hapa Beijing. Kwenye mkutano huo, Wang Yi alieleza sera za China na mambo yanayohusu China katika mazingira ya sasa ya dunia.
|
Matarajio ya Mikutano Miwili ya China kupitia kwa macho ya mtaalam wa Kenya Mkutano wa 5 wa Bunge la 12 la Umma la China na Mkutano wa 5 wa Baraza la 12 la Mashauriano ya kisiasa la China inafanyika mjini Beijing, mojawapo ya masuala muhimu yatakayojadiliwa kwenye mikutano hiyo miwili ni mahusiano ya kibiashara kati ya China na dunia ikiwemo Afrika. Mwandishi wetu wa Nairobi Ronald Mutie amezungumza na mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kenyatta anayefundisha masomo ya sayansi ya siasa Dkt Otiato Wafula.
|
Waziri Mkuu asisitiza kuwa China itaendelea kuwa wazi kwa biashara Mkutano wa tano wa Bunge la awamu ya 12 la umma la China unaendelea leo hapa Beijing, kwa wawakilishi kujadili ripoti ya mipango ya kazi za serikali kwa mwaka huu. Jana kwenye ufunguzi wa mkutano waziri Mkuu Bw Li Keqiang alianza kwa kuwasilisha ripoti hiyo mbele ya bunge ili ijadiliwe. Ripoti hiyo imekuwa na mambo mbalimbali yanayofuatiliwa, ili kujua mwelekeo wa uchumi wa China kwa mwaka huu utakuwaje, na utakuwa na athari gani kwa uchumi wa nchi nyingine duniani na hata uchumi wa dunia.
|
Mwanahabari wa Shirika la utangazaji la Kenya KBC Bw Eric Biegon afuatilia maendeleo ya mkutano wa bunge Kikao cha tano cha bunge la 12 la umma la China kimefunguliwa leo asubuhi hapa Beijing. Waziri Mkuu wa China Bw Li Keqiang amewasilisha ripoti ya kazi za serikali kwa mwaka huu, ikitaja mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na makadirio ya ongezeko la uchumi kupungua kutoka asilimia 6.7 ya mwaka jana hadi asilimia 6.5. Mwanahabari wa Shirika la utangazaji la Kenya KBC Bw Eric Biegon anayefuatilia maendeleo ya mkutano wa bunge.
|
China yaongeza nguvu katika kuvutia fedha za kigeni Waziri wa biashara wa China Bw. Gao Hucheng amesema, kauli kuhusu kuondoa uwekezaji kutoka China si ya kweli, kwani kuvutia fedha za kigeni ni jambo muhimu katika sera ya China kuhusu ufunguaji mlango, na mwaka huu China itaongeza nguvu ya kuvutia uwekezaji.
|
Mwezi Januari thamani ya uagizaji wa bidhaa wa China kutoka nje na uuzaji wa bidhaa kwa nje zilizidi kuliko ilivyotarajiwa Takwimu zilizotolewa leo na Idara kuu ya Forodha ya China zimeonesha kuwa, mwezi Januari mwaka 2017, thamani ya jumla ya uagizaji wa bidhaa kutoka nje na uuzaji wa bidhaa kwa nje ilikuwa RMB yuan trilioni 2.2, hili ni ongezeko la asilimia 19.6 kuliko mwaka jana wakati kama huu.
|
|
More>> |