Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
 
 • Mji wa Hohhot
 •  2005/08/25
  Mji wa Hohhot ni mji mkuu wa mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya Ndani, pia ni kituo cha kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni cha mkoa huo.
 • Mji wa Chengdu
 •  2005/08/04
  Mji wa Chendu ni mji muhimu ulioko kusini magharibi mwa China tokea enzi za kale. Ulikuwa mji mkuu wa dola la Shu katika Enzi ya Madola matatu na mji mkuu wa dola la Shu ya kwanza na Shu ya pili katika kipindi cha Enzi Tano na Madola kumi.
 • Mji wa Changsha
 •  2005/07/14
  Mji wa Changsha ni mji mkuu wa mkoa wa Hunan, pia ni kituo cha kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni, sanyasi, elimu na habari cha mkoa huo.
 • Mji wa Lhasa
 •  2005/06/23
  Mji wa Lhasa ambao ni mji mkuu wa mkoa wa Tibet uko katika tambarare ya sehemu ya katikati ya mto Lhasa ambao ni tawi la Mto Yarlung Zangbo.
 • Mji wa Guangzhou
 •  2005/06/02
  Mji wa Guangzhou ni mji mkuu wa mkoa wa Guangdong na ni kituo cha siasa, teknolojia na utamaduni cha mkoa huo. mji huo uko kusini mashariki mwa mkoa huo, na kaskazini mwa delta ya Mto Zhujiang. Unapakana na bahari ya kusini, Hongkong na Macao.
 • Mji wa Shenzhen
 •  2005/05/12
      Mji wa Shenzhen ni mji wa pwani ulioko kusini mwa china. Uko katika kusini ya mstari wa tropiki ya Kansa. Kwa upande wa mashariki unapakana na Ghuba ya Daya na Ghuba ya Dapeng, kwa upande wa magharibi inakaribia sehemu ya mwisho ya Mto Zhujiang na bahari ya Lingding, kwa upande wa kusini unaunganishwa na Hongkong na Mto Shenzhen, na kwa upande wa kaskazini unapakana na miji ya Dongguan na Huizhou.
 • Mji wa Hangzhou
 •  2005/04/14
  Mji wa Hangzhou uko kusini mwa Delta ya Mto Changjiang, magharibi ya Ghuba ya Hangzhou, sehemu ya chini ya Mto Qiantang na sehemu ya kusini ya Mfereji wa Jinghang. Mji huo ni kituo muhimu cha mawasiliano katika Delta ya Mto Changjiang na sehemu ya kusini mashariki mwa China.
 • Mji wa Nanjing
 •  2005/03/24
      Mji wa Nanjing ambao ni mji mkuu wa Mkoa wa Jiangsu unaitwa Ning kwa kifupi. Mji huo uko kwenye tambarare ya sehemu ya chini ya Mto Changjiang na sehemu ambayo yenye nguvu kubwa ya kiuchumi nchini China yaani Delta ya Mto Changjiang. Umbali kutoka kwenye mji huo hadi mji wa Shanghai ni kilomita 300, ni kilomita 1200 hadi Beijing, na kilomita 1400 hadi Chongqing.  
 • Mji wa Harbin
 •  2005/03/04
  Mji wa Harbin uko kaskazini mashariki mwa China. Mto Songhuajiang unapitia kwenye mji huo, na kuufanya mji huo uwe na mandhari nzuri zaidi na maliasili nyingi.
 • Mji wa Shanghai
 •  2005/01/27
  Mji wa Shanghai unaitwa Hu kwa kifupi, na pia unaitwa Shen. Inasemekana kuwa katika Enzi ya Madola ya Kivita, sehemu hiyo ilikuwa sehemu iliyotawaliwa na Dola la Chu.
 • Mji wa Beijing
 •  2005/01/06
      Beijing ni mji mkuu wa Jamhuri ya Watu wa China. Si kama tu mji huo ni kituo cha kisiasa nchini China, bali pia ni kituo cha utamaduni, sayansi, elimu na mawasiliano. Mji huu uko kaskazini mwa Tambarare ya Huabei. Katika upande wa magharibi, kaskazini na mashariki ya mji huo kuna milima, na katika upande wa kusini mashariki ni tambarare. Hali ya hewa ya Beijing ni ya kanda ya fufutende. Kuna majira manne, majira ya spring huwa ni mafupi, katika majira ya joto mvua hunyesha, majira ya baridi huwa ni marefu na kuna baridi kali, na katika majira ya mpukutiko hali ya hewa huwa ni ya kupendeza.
 • Mji wa Xi'an
 •  2004/12/16
  Mji wa Xi'an katika enzi za kale uliitwa Chang'an na pia uliwahi kuitwa Xidu, Xijing, Daxingcheng, Jingzhaocheng, Fengyuancheng n.k.