• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya

  • Mkutano wa mwaka wa Baraza la 12 la mashauriano ya kisiasa la China wafunguliwa
    Habari
    • Jaji mkuu wa China aahidi kupambana na ugaidi 2014-03-10
    • China kuwekeza zaidi ya dola bilioni 817 kwenye mpango wake wa kuhifadhi mazingira 2014-03-08
    • Waziri mkuu wa China kuizuru Afrika 2014-03-08
    • China yasisitiza kuendelea kufanya kazi ikiwa nchi kubwa inayowajibika 2014-03-08
    • China yapinga wabunge wa bunge la Marekani kukutana na Dalai Lama 2014-03-07
    More>>
    Maelezo
    • Serikali ya China yaweka mipango mipya kuhusu kazi ya mwaka 2014
    Mkutano wa mwaka wa bunge la umma la China ambacho ni chombo cha juu cha utungaji wa sheria cha China umefunguliwa leo asubuhi mjini Beijing, ambapo viongozi wa chama na serikali ya China, pamoja na wajumbe karibu na elfu tatu wa bunge hilo wanashiriki. Mkutano huo umeanza kwa wajumbe wote kuwakumbuka watu waliouawa katika tukio la kigaidi lililotokea usiku wa tarehe 1 Machi katika kituo cha treni kilichoko huko Kunming, mkoani Yunnan.
    • Mkutano wa mwaka wa bunge la umma la China kufunguliwa
    Mkutano wa mwaka wa bunge la umma la China utafunguliwa tarehe 5 Machi, ambapo wajumbe zaidi ya elfu mbili wa bunge hilo kutoka sehemu mbalimbali za China watashiriki. Mkutano wa kwanza na waandishi wa habari wa mkutano huo umefanyika leo asubuhi ambapo msemaji wa mkutano huo Bibi Fu Ying amejibu maswali kuhusu masuala yanayofuatiliwa sana na watu.
    • Mkutano wa mwaka wa Baraza la 12 la mashauriano ya kisiasa la China wafunguliwa
    Mkutano wa mwaka wa Baraza la 12 la mashauriano ya kisiasa la China umefunguliwa katika Jumba la mikutano ya umma mjini Beijing, ambapo viongozi wa China akiwemo rais Xi Jinping na waziri mkuu Li Keqiang wamehudhuria. Mkutano huo umeanza kwa wajumbe wanaohudhuria mkutano huo kuwakumbuka watu waliouawa katika tukio la kigaidi lililotokea tarehe 1 Machi kwenye kituo cha treni kilichoko Kunming, mkoani Yunnan. Mwenyekiti wa baraza la mashauriano ya kisiasa la China Bw. Yu Zhengsheng ametoa ripoti ya kazi ya baraza hilo, na kueleza utekelezaji wa kazi katika mwaka uliopita, na kuweka mipango ya kazi kwa mwaka huu.
    • China yaamua Siku ya kuadhimisha ushindi katika Vita dhidi ya Wajapani na Siku ya Kuwakumbuka waliouawa katika Mauaji ya Nanjing
    Bunge la Umma la China ambalo ni chombo cha kutunga sheria nchini China leo limepitisha azimio la kufanya tarehe 9 Septemba kuwa Siku ya Kuadhimisha Ushindi wa Wananchi wa China katika Vita dhidi ya Wajapani na tarehe 13, Desemba kuwa Siku ya Kuwakumbuka watu waliouawa katika Mauaji ya Halaiki ya Nanjing. Azimio hilo linatokana na hoja zilizotolewa na wajumbe wa bunge kwa miaka mingi. Wakizungumza na waandishi wa habari, wajumbe hao waliowahi kutoa hoja hizo walisema azimio hilo limeitikia matakwa ya wananchi, kuonesha nia ya China ya kupata amani na pia linalingana na utaratibu wa kimataifa.
    • Kazi ya usimamizi ya Bunge la 12 la Umma la China yatoa ufanisi
    Usimamizi ni kazi muhimu ya Bunge la Umma la China kwa mujibu wa katiba. Mwaka jana Bunge la Umma la China na kamati yake ya kudumu ziliimarisha usimamizi wa kazi na hali ya utekelezaji wa sheria katika serikali, mahakama na idara ya uendeshaji mashtaka, wakizungumza na wakazi, kutuma fomu za sensa na kuomba maoni ili kufanya uvumbuzi kuhusu njia za usimamizi, na kazi za usimamizi za Bunge la Umma la China la awamu mpya zimekuwa na ufanisi zaidi. Fadhili Mpunji ana maelezo zaidi.
    • China yaeleza hali ya utungaji wa sheria kwa mwaka jana
    Bunge la Umma la China litaitisha mkutano wa mwaka hivi karibuni, na kabla ya kufanyika kwa mkutano huo, maofisa wa idara inayoshughulikia mambo ya sheria katika Kamati ya kudumu ya Bunge la Umma la China wamefafanua kazi walizofanya katika mwaka jana.
    More>>
    Picha
    More>>
    Mikutano ya miaka iliyopita
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako