• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • • Biashara bidhaa za kilimo China-Afrika yafika $6 bilioni 2018-08-29

  Biashara ya bidhaa za kilimo kati ya China na Afrika imeongezeka na kufikia dola bilioni 6.02 za Kimarekani mwaka 2017, imeelezwa.

  • FOCAC kuhusianisha Ukanda Mmoja, Njia Moja na agenda za AU, UN 2018-08-23

  Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika, FOCAC, utakaofanyika kati ya Septemba 3 na 4 unategemewa kuhusianisha malengo ya Ukanda Mmoja, Njia Moja, Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Maendeo Endelevu na Agenda 2063 ya Umoja wa Afrika.

  • China yashauri namna bora ya kupambana na umaskini 2018-08-20

  China imependekeza uimarishwaji wa tafiti, uendelezwaji wa vipaji kwa vijana na uanzishwaji wa miradi ya mifano kati yake na Afrika ili kufanikiwa katika vita dhidi ya umaskini.

  • Afrika yashauriwa kuiga China vita dhidi ya umaskini 2018-08-20

  Wawakilishi kutoka Afrika katika mkutano wa Ushirikiano wa China na Afrika katika kupunguza umaskini wameshauri nchi zao kuiga mfano wa China katika vita dhidi ya umaskini.

  • Bijie: Mji uliotangazwa eneo hatari kuishi ulivyojipanga kumaliza umaskini 2020 2018-08-20

  Umaskini ni hali ya ukosefu wa mahitaji ya msingi ya binadamu kama vile chakula, maji salama, huduma za afya, mavazi na nyumba kutokana na kukosa uwezo wa kuvinunua.

  • Historia, asili ya Wachina katika Makumbusho 2018-08-06

  Makumbusho ni jengo au taasisi penye maonyesho ya vitu vya kale, kazi za sanaa, sampuli za malighafi au vifaa kwa ajili ya kutunza kumbukumbu ya jamii. Mkusanyiko wa aina hii hulenga kuonyesha mifano ya sanaa, utamaduni, teknolojia au mazingira asilia kwa manufaa ya kuwaelimisha watazamaji

  • China na utamaduni wa unywaji chai 2018-07-26
  • China kuendelea kushirikiana na Afrika kuboresha afya 2018-06-05

  China imesema itaendelea kuimarisha ushirikiano na Afrika katika sekta ya afya kwa kutoa misaada ya kitaalamu na kuboresha miradi inayotekelezwa kwa pamoja kati yake na nchi za bara hilo.

  • China yataka Afrika kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji 2018-05-31

  China imetoa changamoto kwa bara la Afrika kuhakikisha linazidi kuweka mazingira mazuri ikiwemo sera rafiki ili uwekezaji wake barani humo uzidi kuboreka kwa manufaa ya pande zote mbili.

  • Uwekezaji China Afrika kuongezeka 2018 2018-05-31

  Uwekezaji wa China barani Afrika ukiwa umefika jumla ya dola za Kimarekani bilioni 170 mwaka jana, Wizara ya Biashara ya China imesema kwa mwaka huu wa 2018, inategemea uwekezaji huo kuongezeka.

  • China: Uhifadhi mazingira Afrika moja ya vipaumbele vyetu 2018-05-30

  WIZARA ya Ekolojia na Mazingira ya serikali ya China imesema inachukua hatua mbalimbali kuhakikisha mazingira ya bara la Afrika yanalindwa dhidi ya uchafuzi, athari ya mabadiliko ya tabianchi na changamoto mbalinmbali zinazotokana na uharibifu wa mazingira.

  • Rais Xi aikaribisha Burkina Faso FOCAC 2018-05-28

  Rais wa China Xi Jinping amemualika rasmi Rais wa Burkina, Faso Roch Marc Christian Kaboré, kushiriki mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano wa China na Afrika, FOCAC, utakao fanyika mwezi Septemba jijini Beijing.

  • Nafasi ya FOCAC utekelezaji wa Agenda 2063 2018-05-28

  Afrika haina budi kutumia vizuri fursa zilizopo kwenye Jukwaa la Ushirikiano wa bara hilo na China (FOCAC) ili iweje kufanikisha agenda yake ya 2063 uliopitishwa na Umoja wa Afrika (AU).

  • Hadithi yangu Afrika: Maisha mapya mbali na nyumbani 2018-05-25

  Binadamu yeyote hupenda maisha mazuri, furaha, kuishi karibu na familia, ndugu, jamaa na marafiki --na zaidi ya yote kuishi na kufanya kazi nyumbani.

  • Mwanadiplomasia maarufu atoa neno ushirikiano China, Afrika 2018-05-21

  Bara la Afrika limeshauriwa kutumia vizuri fursa ya mahusiano yake na China ili liweze kutatua changamoto mbalimbali zinazolikabili na kujipatia maendeleo.

  • Ufunguaji mlango ulivyoendeleza China 2018-05-21

  CHINA, nchi ya pili kwa uchumi bora duniani, mwaka huu unatimiza miaka 40 ya mageuzi na ufunguaji mlango--sera ambayo imeiwezesha taifa hilo kupiga hatua kimaendeleo na kuimarisha uwekezaji ndani na nje ya nchi.

  • Serikali China haitengenezi, haisafirishi bidhaa feki 2018-05-02

  China imezitaka nchi za Afrika kuhimarisha ulinzi na ukaguzi mipakani na maeneo yote muhimu ikiwemo bandari na viwanja vya ndege ili kudhibiti uingizwaji wa bidhaa zisizokidhi viwango.

  • China yaonya usafirishaji pembe za ndovu 2018-05-02

  Huku ujangili ukiripotiwa kupungua katika nchi za Afrika, China imetoa onyo kali kwa raia wake watakaobainika kujihusisha na usafirishaji wa pembe za ndovu kutoka barani humo. Serikali ya China imetangaza na kusisitiza kuwa, kwa namna yoyote ile, haitamvumilia raia wake atakaebainika kujihusisha na biashara hiyo haramu.

  • Mkurugenzi masuala ya Afrika azungumzia maandalizi ya FOCAC 2018-05-02

  Maandalizi ya mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano wa China na Afrika (FOCAC) utakaofanyika mwezi Septemba, jijini Beijing, unaendelea vizuri. Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Masuala ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje Bw. Dai Bing wakati akifanya mazungumzo na waandishi wa habari kutoka Afrika walioko nchina China katika programu maalum ya mafunzo.

  • Dunia na Ukimya juu ya mgogoro wa kibiashara 2018-04-18

  Mgogoro wa kibiashara kati ya China na Marekani umefika pabaya. Si pazuri kwa China. Si pazuri kwa Marekani. Si pazuri kwa dunia.

  • Media za China kujikita kwenye kiini cha vita ya kibiashara 2018-04-18

  China itaendelea kuieleza dunia sababu, kiini na msingi wa mgogoro wa kibiashara kati yake na Marekani kupitia vyombo vyake vya habari.

  • Sanya kuongeza watalii kwa asilimia 10 2018-04-13

  Uongozi wa Manispaa ya Sanya, mji maarufu kwa utalii uliopo kusini zaidi mwa China, imetangaza mkakati wake wa kuongeza idadi ya watalii kwa asilimia 10 kila mwaka.

  • China, Marekani zikipata hasara, dunia itapata hasara zaidi 2018-04-03

  Ni dhahiri shairi kuwa China na Marekani zipo katika mgogoro wa kibiashara. Hali hii inahitaji majadiliano mapana na ya kina baina ya pande zote mbili.

  Bila udhibiti na utatuzi wa mapema wa hali hii, ni wazi kuwa madhara yake hayatakuwa kwa China au Marekani tu, dunia nzima itapata hasara kwa namna yoyote ile.

  • Balozi Kairuki: Kuchaguliwa kwa Rais Xi neema Afrika 2018-03-18

  Balozi wa Tanzania nchini China Bw. Mbelwa Kairuki amemuelezea Rais Xi Jinping kama kiongozi imara ambaye anaamini ataendelea kusimamia mipango mbalimbali ya maendeleo aliyoanzisha kati ya China na nchi za Afrika.

  • 

  Ni Xi Jinping tena, Bunge laamua

   Abebeshwa matumaini ya China mpya

   Je, Afrika wana chao? Kipi?

   2018-03-17

  Kuchaguliwa tena kwa Rais Xi Jinping kuongoza China kunafungua ukurasa mwingine mpya wa ushirikiano kati ya nchi hiyo na mataifa mengine hususan nchi za bara la Afrika.

  • Ije jua ama mvua, China-Afrika ipo sana 2018-03-09

  China imetangaza rasmi. Imesisitiza. Imeeleza tena. Mahusiano yake na nchi za Afrika, bado yapo sana. Ije mvua, ije jua. Yaje mabadiliko ya aina gani, hakuna kitakachobadili. Ahadi zake kwa Afrika ziko palepale.

  • China inavyotekeleza Diplomasia ya Uchumi kwa vitendo 2018-03-07

  Bunge la Umma la China linaendelea na vikao vyake. Pamoja na mambo mengine yanayojadiliwa, suala la mahusiano yake na mataifa mengine duniani linapewa msisitizo na uzito unaosatahili. Hivi karibuni, Baraza la Mashauriano la Kisiasa la China, ikitoa ripoti ya kazi kwa kipindi kilichopita, limeweka bayana kuwa limefanyia tathmini mfumo wa mahusiano yake na mataifa mengine na kuangalia namna ya kuboresha mahusiano hayo ili yawe bora zaidi.

  • China, maneno kidogo, vitendo kwa sana 2018-03-06

  WAZIRI Mkuu wa China Bw. Li Kequiang mapema leo ametoa ripoti juu ya utendaji wa serikali katika miaka mitano iliyopita. Ni miaka ya mafanikio makubwa, katika nyanja zote za kijamii, kiuchumi na kisiasa.

  • Utekelezaji wa Ukanda Mmoja na Njia Moja wapata msukumo mpya 2018-03-05

  UTEKELEZAJI wa mradi wa Ukanda Mmoja na Njia Moja umepata msukumo mpya baada ya kutajwa kuwa ni moja ya mambo yanayopewa kipaumbele na Baraza la Mashauriano la Kisiasa la China.

  • Majaliwa Christopher Oswero, mhariri wa Habari Msaidizi, Daily News, Tanzania 2018-03-05
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako