v Mwandishi wa habari aliyejikita kwenye uhifadhi wa mazingira 2007/07/05 Bw. Huang Chengde ni mwandishi wa habari na mpiga picha mzoefu wa gazeti la Guiyangribao, mkoani Guizhou, kusini magharibi mwa China. Mpaka sasa amefanya kazi kwenye gazeti hilo kwa miaka 25. Katika miaka 10 iliyopita, mara kwa mara alikuwa anatembelea sehemu ya magharibi ya China. Kwa kutumia kalamu na kamera, alifichua vitendo vilivyokuwa vinasababisha uharibifu wa mazingira, na kuhamasisha jamii izingatie umuhimu wa kuhifadhi mazingira.
|
v Jumba la sinema kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa macho 2007/06/21 Jumba la sinema ni mahala zinapooneshwa filamu. Je, watu wenye ulemavu wa macho wanaweza kupata burudani kwenye jumba la sinema? Jibu ni ndiyo. Hapa mjini Beijing, kuna jumba la sinema linalowahudumia watu wenye ulemavu wa macho. Hivi karibuni mwandishi wetu wa habari alitembelea jumba hilo la sinema.
|
v Tiba na dawa za kitibet zinazotumia sayansi na teknolojia ya hali ya juu 2007/05/30 Kutokana na maendeleo ya kasi ya sayansi na teknolojia ya kisasa, kati ya mifumo minne ya matibabu ya jadi yaliyowahi kuleta athari kubwa kwa binadamu duniani, yaani matibabu ya jadi ya kichina, matibabu ya kitibet, matibabu ya kale ya India na matibabu ya kale ya kiarabu, ni matibabu ya jadi ya kichina na ya kitibet tu ambayo yamehifadhiwa kikamilifu hadi leo, na kupata maendeleo na uvumbuzi bila kusita, matibabu hayo yametoa mchango mkubwa katika kuwasaidia binadamu kupambana na magonjwa na kujenga mwili.
|
v Kijana Pingping anayetarajia kununua nyumba 2007/05/17 Kutokana na kuinuka kwa kiwango cha maisha, hivi sasa watu wengi zaidi wa China wanazingatia zaidi hali ya nyumba wanazoishi. Vijana wengi wanaoishi pamoja na wazazi wao wanapenda kumiliki nyumba zao wenyewe.
|
v Wakili anayetoa msaada wa kisheria kwa wakulima 2007/05/10 Siku ya wafanyakazi wa duniani mwaka huu, yaani tarehe mosi Mei ni siku yenye umuhimu mkubwa kwa Bw. Tong Lihua ambaye ni wakili mmoja nchini China, kwani katika siku hiyo alipewa tuzo ya wafanyakazi na serikali ya China, ambayo ni tuzo yenye heshima kubwa kabisa kwa wafanyakazi wa China.
|
v Luoping, peponi kwa ndege 2007/04/26 Luoping ni wilaya moja iliyopo katika mkoa unaojiendesha wa Ningxia Wahui, kaskazini magharibi mwa China. Ardhi ya huko ina chumvi na magadi nyingi na ipo kwenye mteremko, pia kuna maziwa mbalimbali na eneo kubwa la ardhi oevu. Baada ya juhudi za kuboresha mazingira katika miaka zaidi ya 10 iliyopita, uvuvi umeendelezwa sana huko Luoping, jambo ambalo limefanya mazingira ya huko yaboreshwe sana na kuvutia ndege wengi wanabaki huko kupitisha siku za baridi. Hivi sasa wilaya ya Luoping inajulikana kama peponi kwa ndege.
|
v Watu elfu 50 wametoa maombi ya kununua tiketi za michezo ya Olimpiki katika siku ya kwanza baada ya tiketi za michezo hiyo zianze kuuzwa 2007/04/19 Tangu tiketi za michezo ya Olimpiki ya Beijing zianze kuuzwa tarehe 15 Aprili, katika siku ya kwanza peke yake, watu zaidi ya elfu 50 walitoa maombi ya kununua tiketi zipatazo laki 2.5 kwa kupitia tovuti ya michezo hiyo kwenye mtandao wa Internet. Imefahamika kuwa, uuzaji wa tiketi za michezo ya Olimpiki utakuwa na vipindi vitatu.
|
v Mbinu ya kuongeza mapato ya wakulima wa China 2007/03/29 Maelezo ya leo yanamhusu mkulima mmoja anayejulikana kwa jina kaka Niu, Niu maana yake ya Kichina ni ng'ombe, ambaye anaishi huko Shuangxi, kitongoji cha mji wa Hangzhou, mji maarufu wa utalii uliopo mashariki mwa China. Katika miaka ya hivi karibuni, shughuli za utalii kwenye maskani ya kijana huyo zimeendelezwa sana, ambapo yeye na wakulima wenzake wamepata mbinu mpya ya kuongeza mapato.
|
v Juhudi za kulinda haki na maslahi halali ya wakulima wanaofanya kazi za vibarua mijini nchini China 2007/03/15 Kutokana na maendeleo ya kasi ya utandawazi wa viwanda na miji nchini China, wakulima wengi wanakwenda mijini kufanya kazi za vibarua. Imefahamika kuwa, hivi sasa kati ya wakulima wapatao milioni 800 nchini China, wakulima karibu milioni 200 wanafanya kazi za vibarua mijini.
|
v Mkahawa wa Starbucks ulioanzishwa ndani ya Kasri la kifalme la China wazusha mjadala 2007/03/01 Kasri la kifalme la China liitwalo Forbidden City lipo katikati ya mji mkuu wa China, Beijing. Kasri hilo lina historia ya miaka zaidi ya 600, liliwahi kutumika na wafalme wa China katika enzi za Ming na Qing, ambazo ni enzi za mwisho za kifalme katika historia ya China. Hivi sasa kasri hilo linawavutia watalii wengi sana wa China na wa ng'ambo. Hivi karibuni ulizuka mjadala mkubwa uliosababishwa na mkahawa mmoja wa kigeni kuanzishwa ndani ya kasri hilo.
|
v Mafundi wa kabila la Wahezhe waendeleza ufundi wa jadi 2007/02/15 Mliosikia ni wimbo unaojulikana miongoni mwa watu wa kabila la Wahezhe, uitwao kaka aliyekwenda kuwinda amerudi nyumbani. Hapo awali Wahezhe walikuwa wanajishughulisha na uvuvi na uwindaji, walikuwa hodari katika mambo ya uvuvi na uwindaji, kama vile kutengeneza mashua kwa magamba ya miti na kutengeneza nguo kwa kutumia ngozi ya samaki. Hivi sasa baadhi ya Wahezhe wameanza kujishughulisha na kilimo au viwanda. Je, ufundi wa jadi wa kabila hilo unaendelea vipi?
|
v Xiang Laosai, fundi hodari wa kutengeneza visu 2007/02/01 Katika kijiji cha Husa, mkoani Yunnan kusini magharibi mwa China, kila asubuhi majira ya saa 12 zinasikika kelele za kutengeneza visu.
|
v Wazee wanastahili maisha ya raha mustarehe 2007/01/18 China ni nchi yenye watu bilioni 1.3, na ni moja kati ya nchi ambazo idadi ya wazee inaongezeka kwa kasi. Hivi sasa wananchi wa China wenye umri wa zaidi ya miaka 60 wamefikia watu milioni 144, idadi ambayo ni nusu ya wazee wa bara zima la Asia. Inakadiriwa kuwa hadi kufikia mwaka 2020, idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka kwa watu milioni 100. Namna ya kuwahakikisha wazee waishi kwa raha mustarehe ni suala linalofuatiliwa na jamii ya China.
|
v Watu wa kabila la Wajing wanaoishi visiwani karibu na mpaka wa Vietnam 2007/01/11 Miongoni mwa makabila yote 56 hapa nchini China, kabila la Wajing ni kabila lenye watu wachache sana, ambao wanaishi kwenye visiwa vitatu vilivyopo kusini mwa China, kwenye mpaka kati ya China na Vietnam. Hivi karibuni mwandishi wetu wa habari aliwatembelea watu hao kwenye kijiji kiitwacho Wanwei.
|
v Lugha ya Kitatar yasaidia kupokezana kwa utamaduni wa kabila la Watatar 2007/01/04 Miongoni mwa waislamu wanaoishi katika mkoa unaojiendesha wa kabila la Wauygur wa Xinjiang, China, Watatar ni kabila lenye watu wachache zaidi kuliko makabila mengine. Kabila hilo sasa lina watu elfu 6 hivi, ni kabila dogo kati ya makabila madogomadogo yapatayo 55 ya China
|
v Ziara ya mwandishi wa habari wa BBC mkoani Guangdong, China 2006/12/21 George Arney ni mwandishi wa habari wa BBC. Mwezi Oktoba mwaka huu, yeye na waandishi wa habari wenzake karibu 10 walitembelea Guangdong, mkoa uliopo kusini mwa China. Katika ziara hiyo ya siku 11, Bw. George alipata picha mpya kuhusu China ambayo ni tofauti kabisa na ile aliyekuwa nayo kabla ya kuja China, kiasi kwamba alipomaliza ziara hiyo alisema, ujuzi wake kuhusu China kweli ni mdogo sana.
|
v Harusi za aina mpya zawavutia maharusi wengi nchini China 2006/12/07 Katika miaka ya hivi karibuni, jamii ya China inaendelea kwa haraka, ambapo harusi za Wachina pia zinabadilika na kuwa za aina mbalimbali. Kuna maharusi ambao wamejipangia harusi maalumu, ili kujiwekea kumbukumbu zisizosahaulika na pia kuwavutia wageni wanaoalikwa kuhudhuria harusi zao.
|
v Wakulima wa China waliotafuta kazi za vibarua mijini wabadilika kuwa wakazi wa mijini 2006/11/23 Bw. Zhou Jinglong mwenye umri wa miaka 38 alizaliwa na kukulia katika kijiji cha Xincun, mkoani Anhui uliopo mashariki mwa China. Mkulima huyo pia ni fundi seremala hodari, katika kipindi cha miaka 7 iliyopita, alikuwa anahangaika kwenye viwanja mbalimbali mjini Hefei, mkoani Anhui ambako miradi mbalimbali ya ujenzi ilikuwa inajengwa, wakati ambapo kulikuwa na pilikapilika mashambani, alirudi kijijini kwao kuwasaidia jamaa zake.
|
v Jinsi wakazi wa jiji la Chongqing, China walivyokabiliana na maafa makubwa ya ukame mwaka huu 2006/11/09 Katika siku za joto mwaka huu, jiji la Chongqing lililopo kusini magharibi mwa China lilikumbwa na maafa makubwa ya ukame ambayo hayakutokea katika kipindi cha miaka 60 iliyopita, ambapo wakazi na mifugo walikosa maji safi ya kunywa, mimea ya kilimo iliharibika sana na moto ulitokea misituni mara kwa mara.
|
v Mwalimu aliyewabeba watoto kwenda shuleni 2006/10/19 Mto Sichuan ni mto mdogo uliopo kusini magharibi mwa China. Kijiji cha Longjia kipo kando ya mto huo. Awali watoto wa kijiji hicho walilazimika kuvuka mto huo kwenda shule ya msingi iliyopo katika upande mwingine wa mto kwa vile ilikuwa hakuna daraja kwenye mto huo.
|
v Askari polisi wa China wanaoshiriki kwenye jukumu la Umoja wa Mataifa la kulinda amani nchini Afghanistan 2006/10/05 Bw. Qiu Chongwen mwenye umri wa miaka zaidi ya 30 ni askari polisi wa China. Mwezi wa Mei mwaka 2005, afisa huyo alitumwa na wizara ya usalama wa raia ya China nchini Afghanistan kushiriki kwenye jukumu la Umoja wa Mataifa la kulinda amani
|
v Kinyang'anyiro cha kuwatafuta warembo wa makabila mbalimbali ya China 2006/09/28 China ina makabila 56. Hivi karibuni kinyang'nyiro cha kuwatafuta warembo wa makabila hayo kilifanyika hapa Beijing, ambapo makabila hayo 56 kila moja lilimchagua msichana mmoja mwerevu apewe sifa ya mrembo wa kabila lake
|
v Wachina wanaoishi ng'ambo wafuatilia maendeleo ya vijiji vya China 2006/09/14 Hivi karibuni katika kijiji cha Dacheng mkoani Henan, katikati ya China watu waliwazungumzia sana wazee wawili waliokuja kutembelea kijiji hicho. Wazee hao ni wakalimani wenye uzoefu mkubwa wa Umoja wa Mataifa, Bw. Hua Junxiong kutoka Taiwan, China na Bw. Liu Dazheng kutoka Hong Kong, China. Hivi sasa wazee hao wawili wameteuliwa kuwa wakuu wa heshima wa kijiji cha Dacheng.
|
v Mwanamke anayeongoza kijiji chake kupata maendeleo 2006/08/31 Kijiji cha Jinghua kipo wilayani Xinxiang, mkoani Henan, katikati ya China. Hivi sasa kijiji hicho kinajulikana kutokana na maendeleo yake. Wanakijiji wenyewe walisema hapo awali kijiji hicho kilikuwa maskini, baada ya Bibi Liu Zhihua kuchaguliwa kuwa mkuu wa kijiji hicho, juhudi za kuondokana na umaskini zikaanza kuzaa matunda.
|
v Daktari aliyepata heshima kutoka kwa wagonjwa kutokana na kushikilia maadili ya udaktari 2006/08/24 Daktari Hua Yiwei aliyekuwa na umri wa miaka 73 alifariki dunia jioni ya tarehe 12 Agosti baada ya kuugua ugonjwa wa saratani kwa siku zaidi ya 380. Hata alipokuwa amelazwa, daktari huyo alikuwa anaweka kumbukumbu kuhusu alivyokuwa anajisikia kutokana na dalili za ugonjwa, ili ziwasaidie wagonjwa wengine katika matibabu yao.
|
v Kumbukumbu ambazo watoto yatima waliopoteza wazazi wao katika tetemeko kubwa la ardhi la Tangshan hawatazisahau 2006/08/10 Tetemeko kubwa la ardhi lililoukumba mji wa Tangshan miaka 30 iliyopita, ni tukio ambalo Wachina hawataweza kulisahau. Maafa hayo yalisababisha vifo vya watu laki 2 na elfu 40, na kuwafanya watoto zaidi ya elfu 4 wapoteze wazazi wao.
|
v Siku ya majirani yaimarisha ujirani mwema katika miji ya kisasa 2006/07/27 Wachina huzingatia ujirani mwema, kuna methali ya Kichina inayosema "Majirani huweza kukusaidia kuliko jamaa walioko mbali". Lakini hivi sasa wakazi wa miji ya China ya zama tulizo nazo wameona kuwa, uhusiano wa karibu kati ya majirani unapotea siku hadi siku
|
v Wanamitindo wa China wanaong'ara kwenye jukwaa la maonesho 2006/07/13 Kutembea jukwaani, kuonesha mitindo ya mavazi na kufuatiliwa na kamera, ni kazi ya uanamitindo inayowavutia sana warembo. Katika makala hii, mtasikia maelezo kuhusu wanamitindo kadhaa wa China.
|
v Mwanamke aliyejikita kuwaokoa tiger 2006/06/22 Tiger ni chui mkubwa mwenye milia. Hivi sasa wanyama hao hawapo barani Afrika, hata barani Asia tiger pori ni wachache sana kiasi ambacho wanyama hao wako hatarini kutoweka. Hali hiyo inafuatiliwa na watu wengi, na mmoja wao ni Bibi Quan Li, ambaye alianzisha mfuko mmoja wa kimataifa wa kuwaokoa tiger wa kichina.
|
v China yafanya sensa ya pili ya walemavu ili kuwahudumia vizuri zaidi wananchi wenye ulemavu 2006/06/08
Mwezi Aprili mwaka huu, sehemu nyingi nchini China zilikuwa zimeingia katika majira ya mchipuko na hali ya hewa ilikuwa inaelekea kuwa joto, lakini mabaki ya theluji bado yalikuwa yanaonekana katika mbuga mkoani Qinghai, magharibi mwa China. Bibi Miao Zirun mwenye umri wa miaka 20 ni mkazi wa wilaya inayojiendesha ya Gangcha ya kabila la Watibet mkoani humo.
|