Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
 
v Maisha ya Mwanafunzi Anayejitolea Katika Magharibi ya China 2004/06/17
Sehemu ya magharibi ya China ni sehemu yenye mazingira magumu, wakazi wa sehemu hiyo wanaishi maisha ya umaskini, watoto wao wanasoma katika shule zenye hali duni sana.  Lakini katika miaka ya hivi karibuni tangu serikali ya China kutilia maanani kuendeleza sehemu ya magharibi, na kupeleka vijana wanaojitolea kufanya kazi huko kama walimu, sehemu hizo zimeongezwa nguvu na uhai.
v Walinzi wa bendera ya taifa 2004/06/10
v Maisha ya wanakijiji katika kijiji kongwe kiitwacho Tunbao 2004/06/10
v Maisha ya wakazi wa Shanghai,China 2004/06/03
Sehemu ya Waitang iliyoko magharibi ya mto Huangpu ni mahali muhimu kwa wakazi wa Shanghai. Sehemu hiyo yenye mandhari nzuri na majengo mengi yenye mtindo wa kimagharibi, kila siku panawavutia watalii wengi wa nchini China na nchi za nje.     
v Maisha ya Wakazi wa Guangzhou 2004/05/27
 Mji wa Guangzhou ulioko kusini mwa China ni mji mzuri wa kuishi. Ukienda mjini Guangzhou utakuta vyakula vitamu vya aina nyingi, mikahawa ya chai na baa ziko nyingi. Wakazi wazee na wa makamo wa Guangzhou wanaishi maisha ya raha, na vijana wa mji huo pia wanafurahia maisha ya utajiri baada ya kazi.         
v Maisha ya wakazi wa Beijing  2004/05/20
v Kukua Pamoja Katika Miji 2004/05/13
v Wakulima wa Mkoa wa Ningxia Watajirika kwa makwao na Kutafuta Ajira nje 2004/05/06
v Watu wa eneo la mfereji 2004/04/29
v Misaada kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kutoka familia maskini nchini China 2004/04/22
v Mshairi Mkulima 2004/04/22
 Huko Tianjin, mji wa kaskazini mwa China, kuna mkulima aitwaye Dou Xizhen, ambaye pia ni msanii. Bw. Dou hakupata mafunzo yoyote ya uchoraji wa kitaaluma, lakini amejifundisha mwenyewe. Picha zake zimechanganya umaalumu wa uchoraji wa kichina na kimagharibi, hivyo zinapendwa na Wachina na wageni.
v Soko la ajira nchini China kwa wahitimu wa vyuo vikuu 2004/04/15
Tokea mwishoni mwa miaka ya 80 ya karne iliyopita, serikali ya China ilifuta hatua kwa hatua sera ya kuwapa ajira wahitimu wa vyuo vikuu. Na katika muda huu, vyuo vikuu vya China viliongeza kuwaandikisha wanafunzi, na idadi ya wahitimu wa vyuo vikuu pia iliongezeka haraka. Kadiri ushindani katika soko la ajira unavyozidi kuwa mkali miongoni mwa wahitimu wa vyuo vikuu, mawazo yao kuhusu mambo ya ajira yanavyobadilika, na mawazo ya kujitafutia ajira yameimarika.          
v Uhifadhi wa mimea adimu katika eneo la magenge matatu 2004/04/07
Katika majadiliano kuhusu manufaa na athari mbaya kutokana na mradi wa magenge matatu, suala moja linalofuatiliwa na watu ni uhifadhi wa mimea adimu ambayo ni maalumu katika eneo la ujenzi wa mradi huo. Pamoja na majadiliano hayo, hatua zimechukuliwa ili kuhifadhi mimea hiyo adimu. Makala hii ni kuhusu Bw. Xiang Xiufa na bustani yake ya mimea adimu.
v Kijana mlemavu anayefanya mwujiza 2004/03/29
Kuvuka mlangobahari wa Uingereza kumekuwa ni ndoto ya watu wengi wanaopenda mchezo wa kuogelea. Tokea mwaka 1875 mpaka hivi sasa, kumekuwepo na watu zaidi ya elfu 6 ulimwenguni waliojaribu kuogelea na kuvuka mlangobahari wa Uingereza, lakini ni watu wapatao 800 tu ambao wamepata mafanikio. Tarehe 24, Agosti, mwaka 2003, Bw. Xie Yanhong kutoka Dalian, China, alifanya mwujiza na kuwa mlemavu wa kwanza duniani aliyefanikiwa kuongelea na kuvuka mlangobahari huo.
v Maisha ya watu wanaoishi pembeni mwa Mfereji Jinghang 2004/03/23
Katika sehemu ya mashariki ya China, upo mfereji mkubwa wenye urefu wa kilomita karibu 1,800. Kwa kuwa unaunganisha mji mkuu Beijing na mji mwingine Hangzhou, unaitwa mfereji wa Jianghang, ambao ni mrefu kabisa duniani.
v Bw. Song Fengnian, mbunge mkulima wa Bunge la Umma la China  2004/03/10
Nje ya Zhengzhou, ambao ni mji mkuu wa mkoa wa Henan uliopo katikati ya China, kuna kijiji kiitwacho Song Zhai. Ukifanya matembezi katika kijiji hicho, utajikuta katika makazi safi, maeneo yenye nyasi na wakazi wenye furaha, hali ambayo ni sawa na ile inavyoonekana mijini. Lakini kijiji hicho zamani kilikuwa ni maarufu kwa uchafu na umaskini, na mabadiliko yake makubwa ya namna hii yametokana na juhudi za mbunge wa bunge la umma la taifa aitwaye Song Fengnian.
v Mji wa Shihezi, lulu la jangwa katika kaskazini magharibi ya China. 2004/02/26
Mji wa Shihezi uliopo ndani ya jangwa, lakini unaonekana kuwa na rangi ya kijani. Ukiambiwa kuwa, katika miaka 50 iliyopita, mji huu maarufu kama lulu la jango kwa hivi sasa, ulikuwa mji mdogo uliojaa matete, utelezi na jangwa, utaweza kuamini?
v Wakulima wa China wapata pesa kutokana na upandaji wa miti ya LOQUAT 2004/02/23
Mkoa wa Sichuan uliopo kusini magharibi mwa China ni mkoa wa pili kwa idadi kubwa ya watu, na pia unajulikana sana kwa shughuli za kilimo. Kwa ajili ya kuongeza mapato ya wakulima, mkoa huo umetekeleza mkakati unaoitwa "kusitawisha kilimo kwa sayansi na elimu". Upandaji miti ya Loquat ndiyo sehemu ya mkakati huo, na wanavijiji wengi wamenufaika.
v Uhifadhi wa Panda nchini China. 2004/02/10
Panda,  maarufu kama hazina ya taifa ya China, ni aina ya wanyama ambao wapo katika hatari ya kutoweka kabisa. Takwimu zinaonesha kuwa, hivi sasa, kuna panda wapatao elfu 1 tu duniani, na wengi wao wanaishi milimani kaskazini magharibi na kusini magharibi mwa China.
v Mzee Chen Banggui na nyimbo za Haozi. 2004/01/13
  Katika sehemu ya mwanzo ya mto Changjiang ambao ni mto mkubwa wa kwanza nchini China, hapo awali, usafiri wa boti ulikuwa mgumu sana na kubidi kusaidiwa na wafanyakazi maalumu, ambao walikuwa wanafanya kazi kuzisaidia boti huku wakiimba nyimbo zenye mahadhi maalumu, nyimbo hizo zimepewa jina la "Haozi".
v Maisha ya Familia ya Wahamiaji wa Mradi wa Maji wa Magenge Matatu. 2004/01/07
Kutokana na ujenzi wa bwawa kubwa la magenge matatu kwenye mto Changjiang, ambao ni mto wa kwanza kwa ukubwa nchini China, makazi ya watu wapatao milioni moja waliokuwa wanaishi kando za mto huo yamefunikiwa na maji. Tokea mwaka 1993, China ikigharimia fedha nyingi, ilianza kutekeleza mradi mkubwa wa uhamiaji, na kujenga makazi mapya kwa watu waliohamishwa. Hivi sasa, miaka 10 imeshapita. Je, maisha ya wahamiaji hao yanaendelea vipi? Sasa hebu tutembelee familia moja ya wahamiaji, na kushuhudia maisha yao yanavyoendelea.
v Maisha Ya Watu Wa Kawaida Wa Nan Chizi Mjini Beijing 2003/12/12
Mzee Qin Zhen mwenye umri wa miaka 74, akiambatana na watoto na wajukuu wake, alirudi kwenye makazi yake yaliyopo Nan Chizi, katikati ya mji wa Beijing
1 2 3 4 5