Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
 
v Simu na hadhi yake katika maisha ya watu wa China 2008/11/20
Hivi sasa simu za mkononi zinachukua hadhi muhimu katika maisha ya watu wa China, kiasi kwamba ni mahitaji ya kila siku. Lakini amini usiamini, miaka 30 iliyopita katika sehemu nyingi nchini China, simu ilikuwa ni bidhaa isiyo ya kawaida, wakati huo njia ya posta ilikuwa ni njia muhimu ya mawasiliano kati ya watu wanaoishi katika sehemu mbili zilizoko mbali.
v Mkoa wa Ningxia wahimiza utoaji mafunzo ya ufundi wa kazi 2008/11/03
Mkoa unaojiendesha wa kabila la Wahui wa Ningxia una watu wengi, lakini mashamba ya mkoa huo ni machache. Ili kuhamisha ziada ya nguvukazi vijijini, serikali ya huko inafuata hali halisi, na kuwahimiza watu hao kwenda nje ya mkoa huo kufanya kazi. Ili kuinua sifa ya watu hao, mkoa wa Ningxia unaimarisha kuhimiza utoaji mafunzo ya ufundi wa kazi.
v Watu wenye tabasamu waonesha sura nzuri ya Beijing 2008/09/24
Katika Michezo ya Olimpiki ya Beijing iliyomalizika siku chache zilizopita, kuna watu wanaojitolea milioni 1.47 waliotoa huduma katika kazi mbalimbali zikiwemo maandalizi ya mashindano, usalama, mawasiliano, utoaji huduma kwa vyombo vya habari na uendeshaji wa mji.
v Wimbo wa Michezo ya Olimpiki "Beijing" 2008/09/11
Wanamuziki wa Bendi ya The SMU ya Ujerumani walikuja Beijing wakiwa na wimbo wao uitwao "Beijing" walioutunga kwa ajili ya Michezo ya Olimpiki ya Beijing 2008.
v Maisha ya Bw. Nuttavudh Photisaro mjini Guangzhou 2008/06/19
Bw. Photisaro ni konsela wa Thailand mjini Guangzhou, China, zamani aliwahi kuwa konsela wa Thailand nchini Cambodia. Muda wake wa kufanya kazi hapa China haujatimia mwaka mmoja, lakini ameupenda mji huo mzuri.
v Maelezo kuhusu polisi wawili wa kike  2008/05/29
Mjini Pengzhou mkoani Sichuan kuna polisi mmoja wa kike anayeitwa Jiang Min. Yeye ni mtu wa kabila la Waqiang, na wazazi wake pamoja na binti yake mwenye umri wa miaka miwili walipoteza maisha yao kwenye tetemeko la ardhi. Lakini katika hali hii, yeye alivumilia uchungu mkubwa, na bado aliendelea kufanya kazi ya uokoaji kwenye mstari wa mbele.
v Mjapan Bw. Kobori Shogo anayeishi nchini China 2008/05/08
Bw. Kobori Shogo ana umri wa miaka 60, hivi sasa yeye ni naibu meneja mkuu wa kiwanda cha kutengeneza mashine nchini China, ambacho ni tawi la kampuni moja ya Japan. Aliwasalimia wasikilizaji wa Radio China Kimataifa kwa lugha ya Kichina. Akisema "Hamjambo wasikilizaji. Mimi ninaitwa Kobori Shogo, leo nimefurahi sana. Asanteni."
v Mabadiliko ya makazi ya watu 2008/04/17
Makazi siku zote ni jambo muhimu katika maisha ya watu wa China. Katika miaka ya hivi karibuni, kuboresha hali ya makazi pia ni jambo wanalozungumzia sana watu wa China
v Mabadiliko ya mavazi ya waislamu nchini China 2008/04/03
Mavazi ni kama kumbukumbu ya aina moja na historia inayovaliwa, na mabadiliko ya mavazi yanaonesha mabadiliko ya jamii. Katika maelezo hayo, mwandishi wetu wa habari aliwahoji waislamu wa China wanaotoka makabila tofauti, wakielezea jinsi mavazi ya watu wa China yalivyoendelezwa katika miaka 30 iliyopita.
v Wilaya ya Yanchi mkoani Ningxia nchini China yapata ufanisi mkubwa katika kuzuia kuenea kwa jangwa 2008/03/27
Mkoa unaojiendesha wa kabila la Wahui wa Ningxia ulioko kaskazini magharibi mwa China, ni mmoja kati ya mikoa iliyoathiriwa vibaya kabisa na jangwa nchini China. Katika miaka 20 iliyopita, eneo la ardhi yenye hali ya jangwa la wilaya ya Yanchi mkoani Ningxia lilichukua karibu asilimia 42 ya eneo la wilaya hiyo.
1 2 3 4 5 6 7 8 9 10