Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
 
  • Mwandishi wa vitabu ambaye pia ni askari polisi, Cao Naiqian
  •  2007/07/30
    Bw. Cao Naiqian mwenye umri wa miaka 59 ni askari polisi katika mji wa Datong mkoani Shanxi. Lakini tofauti na askari polisi wengine, yeye pia ni mwandishi mashuhuri wa vitabu. Vitabu vyake zaidi ya 30 vimetafsiriwa kwa lugha za kigeni na kusambazwa katika nchi za Japani, Marekani, Canada na Uswis.
  • Mcheza Filamu Mwanamke Yu Feihong
  •  2007/07/16
    Yu Feihong ni mcheza filamu nyota nchini China, ingawa yeye bado ni kijana na jina lake linavuma sana miongoni mwa watazamaji, lakini anaishi kimya na kawaida kabisa.
  • Tamasha la filamu za Hong Kong lafanyika kwenye kasri la mataifa la Umoja wa Mataifa
  •  2007/07/04
    Tarehe mosi Julai ilikuwa ni siku ya kuadhimisha mwaka wa kumi tokea Hong Kong irudishwe nchini China. Tarehe 3 jioni tamasha la filamu za Hong Kong lilizinduliwa katika kasri la mataifa la Umoja wa Mataifa, katika tamasha hilo la siku tatu filamu tatu mpya za Hong Kong zitaoneshwa na pia yatafanywa maonesho ya picha zinazoonesha maisha wa wakazi wa Hong Kong kutoka pande mbalimbali
  • Maisha ya furaha yanapatikana kutokana na kuwa na ndoto
  •  2007/07/02
    Dansi ya "Ndoto Yangu" iliyochezwa na wasanii hao ilipomalizika tu, mara makofi yalipigwa kwa muda mrefu ndani ya ukumbi wa ubalozi wa China mjini Berlin Ujerumani. Watazamaji wa Wachina na Wajerumani walivutiwa na kufurahia maonesho hayo ya ajabu. Hayo ni maonesho ya mwisho katika maonesho ya mzunguko katika nchi tano barani Ulaya.
  • Mtungaji muziki wa opera ya Huangmei Bw. Shi Bailin
  •  2007/06/18
    Opera ya Huangmei ni opera muhimu katika mkoa wa Anhui, mkoa uliopo katikati ya China. Opera hiyo inaimbwa kwa lahaja ya kimkoa. "Ndoa ya Malaika" ni hadithi ya kusisimua na kuchezwa kwa opera ya Huangmei, ni opera ambayo inajulikana sana kati ya opera zote za Haungmei.
  • Michezo ya sanaa ya China inavutia zaidi katika Tamasha la "Kukutana Mjini Beijing"
  •  2007/06/04
    Tokea mwisho wa mwezi Aprili Tamasha la "Kukutana Mjini Beijing" lianzishwe, vikundi vya sanaa zaidi ya 40 kutoka nchi 20 vimeshiriki kwenye tamasha hilo. Michezo ya sanaa ya China ni sehemu muhimu katika tamasha hilo.
  • Maingiliano ya utamaduni kati ya China na Ufaransa yapamba moto nchini China
  •  2007/05/28
    Tokea mwanzoni mwa mwezi Aprili hadi mwishoni mwa mwezi Juni, shughuli za maingiliano ya kiutamaduni kati ya China na Ufaransa zimekuwa zinapamba moto katika miji 14 ya China, shughuli hizo ni pamoja na muziki, mashairi, filamu na picha za kamera.
  • Mchoraji na sufii wa dini ya Buddha Shi Guoliang
  •  2007/05/21
    Bw. Shi Guoliang mwenye kuvaa joho la dini ya Buddha ni mchoraji maarufu nchini China. Maishani mwake licha ya kufanya utafiti kuhusu ubuddha alikuwa anatumia wakati wote kuchora picha, na yeye pia ni profesa mwalikwa wa vyuo vikuu kadhaa.
  • Bw. Guo Degang na mchezo wake wa ngonjera ya kuchekesha
  •  2007/05/07
    Ngonjera ya kuchekesha iliwahi kuwa ni aina moja ya michezo ya sanaa inayowavutia sana Wachina, lakini katika miaka ya karibuni mchezo wa aina hiyo umekuwa katika hali ya kudidimia, baadhi ya watu walitoa kauli wakisema, "Tuokoe mchezo wa ngonjera ya kuchekesha!"
  • Mchoraji wa picha za katuni Fang Cheng
  •  2007/04/23
    Mzee Fang Cheng mwenye umri wa miaka 89, ni mchoraji mashuhuri wa picha za katuni nchini China, ameshughulika na utafiti wa uchoraji wa picha za katumi kwa miaka mingi. Picha alizochora zinawachekesha sana watu hata kuwavunja mbavu, na huku zinawafanya watu watafakari. Licha ya kuchora picha, ameandika vitabu vingi vya nadharia ya uchoraji wa picha za katuni.
  • Mwongozaji wa filamu wa China Chen Daming
  •  2007/04/09
    Bw. Chen Daming aliyekuwa mwigizaji wa filamu nchini Marekani kwa miaka mingi, amerudi nyumbani China ili kutimiza ndoto yake ya kuwa mwongozaji wa filamu. Mwaka 2006 filamu ya "Mahangaiko ya Kutafuta Maisha" aliyoongoza upigaji wake, ilitingisha nyanja ya filamu.
  • Juhudi za Kulinda Hakimiliki Nchini China Zapata Mafanikio Siku hadi Siku Nchini China
  •  2007/03/26
    Muda si mrefu uliopita, kutokana na filamu ya "Shrek 2" kurudufiwa na kuwa sahani za video na kuuzwa madukani nchini China, Studio ya kutengeneza filamu hiyo nchini Marekani iliilalamikia China. Baada ya kupata malalamiko hayo Idara ya Kulinda Hakimiliki ya China mara moja ilichukua hatua ya kusaka sahani hizo katika miji ya Beijing, Shanghai na Guangzhou, licha ya kuzoa sahani hizo iliyatoza faini maduka 50 husika.
  • Wajumbe wa nyanja ya fasihi na sanaa washiriki mkutano wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China
  •  2007/03/19
    Mkutano wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China ulifanyika hapa Beijing. Miongoni mwa wajumbe walioshiriki katika mkutano huo wako wajumbe zaidi ya 150 kutoka nyanja ya fasihi na sanaa, ambao kama wajumbe wengine walijitahidi kutoa maoni na mapendekezo yao kutokana na uchunguzi wao.
  • Mwongozaji filamu wa China Liu Jie
  •  2007/03/05
    Miezi kadhaa iliyopita, filamu ya China iitwayo "Korti Kwenye Mgongo wa Farasi" ilipata tuzo katika Tamasha la Filamu la Venice. Mwongoza filamu hiyo anaitwa Liu Jie, kabla ya hapo hakutegemea kama filamu hiyo ingepata tuzo katika tamasha hilo, kwani ni mara ya kwanza kuongoza kwake upigaji wa filamu .
  • Chakula cha Kichina jiaozi
  •  2007/02/21
    Tarehe 18 ni sikukuu ya mwaka mpya wa Kichina. Katika siku hiyo Wachina karibu wote wana desturi ya kula chakula cha jiaozi. Jiaozi ni chakula kama sambusa ndogo yenye umbo la nusu mwezi na kinachopikwa kwa kuchemshwa ndani ya maji
  • Mtaalamu wa taaluma ya riwaya ya "Ndoto kwenye Jumba Jekundu"
  •  2007/02/05
    "Ndoto kwenye Jumba Jekundu" ni riwaya maarufu katika fasihi ya kale nchini China. Wasomi wengi wamewahi kufanya utafiti kuhusu riwaya hiyo na mwandishi wake Cao Xueqin, na kuufanya utafiti huo kuwa taaluma. Mmoja wa watafiti hao anaitwa Zhou Ruchang.
  • Uzalishaji kwenye sekta ya utamaduni nchini China waendelea kwa kina
  •  2007/01/22
    Kongamano la nne kuhusu uzalishaji kwenye sekta ya utamaduni ulimalizika siku chache zilizopita mjini Beijing. Wajumbe kutoka idara za serikali, makampuni na idara za watafiti zaidi ya mia moja walihudhuria kongamano hilo na kujadili kwa kina kuhusu maendeleo ya uzalishaji katika sekta ya utamaduni nchini China.
  • Shughuli za utamaduni zachangia mkutano wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika
  •  2006/12/11
    Katika siku ambapo mkutano wa wakuu wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika ulipofanyika mjini Beijing, shughuli nyingi za utamaduni wa Afrika pia zilifanyika mjini Beijing.
  • Maingiliano ya kiutamaduni kati ya China na Afrika yanazidi kuimarika
  •  2006/11/13
    Wakati mkutano wa viongozi wakuu wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika ulipokaribia kufanyika, tarehe 25 wasanii kutoka nchi tano za Afrika walifanya maonesho ya michezo ya sanaa mjini Beijing.
  • Waongoza filamu vijana wa China wavutia macho nchini China na nchi za nje
  •  2006/10/23
    Hivi sasa nchini China wameibuka waongoza filamu vijana ambao katika ushindani wa soko la filamu wanashikilia mtindo wao wa sanaa na kusogeza filamu zao karibu na watazamaji. Filamu zao zinavutia nchini China na nchi za nje.
  • Viongozi wa sekta ya utamaduni wafafanua Mpango wa Maendeleo ya Utamaduni nchini China
  •  2006/10/02

    Hivi karibuni viongozi wa Wizara ya Utamaduni, Idara Kuu ya Redio, Filamu na Televisheni pamoja na Ofisi Kuu ya Uchapishaji nchini China walifanya mkutano na waandishi wa habari, kwenye mkutano huo walifafanua Mpango wa Maendeleo ya Utamaduni katika miaka mitano ijayo nchini China

  • Mtengeneza sanamu kijana Wu Weishan
  •  2006/09/11
    Mtengeneza sanamu wa China Wu Weishan ingawa bado ni kijana, lakini sanamu 300 za wanautamaduni mashuhuri wa China ya kale alizotengeneza zinathaminiwa sana na kuhifadhiwa nchini China na katika nchi za nje, mtengeneza sanamu huyo ni msanii pekee wa Asia katika Shirikisho la Wachonga Samanu la Kifalme nchini Uingereza yaani the Royal Society of British Sculptors.
  • Mwongoza filamu Ning Hao
  •  2006/08/21
    Filamu ya "Hadithi ya Jade" iliyooneshwa hivi karibuni nchini China imeleta mapato mara tatu kuliko yuan milioni tano iliyowekezwa, mwongoza filamu hiyo Bw. Ning Hao alijulikana ghafla na kuwa mtu wa kuvutia sana wawekezaji wa filamu.
  • Mtaalamu wa magofu ya mji wa Yin wa Enzi ya Shang, Yang Xizhang
  •  2006/08/14
    Hivi karibuni kwenye mkutano wa urithi wa utamaduni duniani uliofanyika nchini Lithuania, magofu ya mji wa kale wa Yin nchini China yamewekwa kwenye orodha ya urithi wa utamaduni duniani.
  • Mwigizaji filamu Wang Fuli
  •  2006/07/24
    Bibi Wang Fuli ni mwigizaji mashuhuri wa filamu, alipitia vipindi kadhaa vya maendeleo ya filamu nchini China na alifanikiwa kuigiza wahusika wa aina tofauti ambao waliwaingia sana akilini watazamaji katika filamu.
  • Mchoraji anayetamani amani ya Mashariki ya Kati, Feng Shaoxie
  •  2006/07/10
    Maonesho ya picha za mchoraji Feng Shaoxie yanayofanyika katika Jumba la Sanaa la Beijing yanayoitwa "Njiwa wa Mashariki ya Kati" yanavutia watazamaji wengi. Picha zilizochorwa zenye mada ya amani ni nadra kupatikana katika historia ya uchoraji nchini China. Picha hizo zinawavutia sana watazamaji.
  • Msanii wa uchapaji urembo kwenye nguo kwa nta, Hong Fuyuan
  •  2006/06/26
    Uchapaji urembo kwenye nguo kwa nta ni sanaa ya aina pekee ya makabila madogo madogo kwenye sehemu ya milimani, kusini magharibi mwa China. Ingawa sanaa hiyo imekuwepo kwa miaka elfu kadhaa lakini bado ina nguvu kubwa ya uhai. Bw. Hong Fuyuan anayesanifu na kukusanya michoro ya uchapaji huo, aliita sanaa hiyo kuwa ni chemchemi ya milimani.
  • "Siku ya India" yafanyika katika Chuo Kikuu cha Beijing
  •  2006/06/12
    Katika siku za karibuni Chuo Kikuu cha Beijing kilikuwa na shamrashamra za utamaduni wa India kutokana na siku ya India kufanyika huko.
  • Mwongozaji wa michezo ya kuigiza televisheni, mkulima Zhou Yuanqiang
  •  2006/06/05
    Zhou Yuanqiang ni mmoja wa wakulima milioni 900 wa China. Miaka 13 iliyopita aliongoza wakulima wenzake kuhariri na kutengeneza mchezo wa kuigiza televisheni kwa kamera yake ya video.
  • Mhifadhi wa utamaduni wa jadi wa China Bw. Feng Jicai
  •  2006/05/15
    Bw. Feng Jicai ni mwandishi wa vitabu na mchoraji mashuhuri nchini China. Katika miaka ya karibuni, kwa moyo wote anajishughulisha na kazi ya kuokoa na kuhifadhi utamaduni wa jadi unaokaribia kutoweka na ameanzisha "mradi wa kuhifadhi utamaduni wa jadi wa China". Juhudi zake zinaungwa mkono na sekta mbalimbali za jamii, watu wanamsifu kuwa ni "mhifadhi wa utamaduni wa jadi wa China".
    1 2 3