• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • • Hatuwezi kuongeza mishahara kila mara asema rais wa Kenya 2019-02-22
  Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema serikali haiwezi kuwa na fedha za kuongezea watu wote mishahara kila mara na kuwataka watumishi wa umma wafikirie kwanza wananchi wa kawaida badala ya kuitisha migomo kila mwaka.
  • Kenya na Somalia zatakiwa kutafuta suluhu la kidiplomasia kuhusu mzozo wa mpaka 2019-02-21
  Huku serikali za Somalia na Kenya zikiendelea kutafuta suluhu la mzozo wa baharini ulioibuka hivi karibuni, sasa kampuni moja ya Norway imesema ilipata sehemu hiyo inayozozaniwa kutoka Somalia na baadaye kutafuta wanunuzi wa Uingereza.
  • Chama tawala nchini Uganda champitisha rais Museveni kugombea tena urais mwaka 2021
   2019-02-20

  Kamati Kuu ya chama tawala nchini Uganda NRM imetangaza kuwa, rais wa sasa wa nchi hiyo Yoweri Museveni atagombea tena nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka 2021.

  • Somalia na Umoja wa Mataifa zatafuta njia za kuboresha juhudi za ujenzi wa amani
   2019-02-19

  Somalia na Umoja wa Mataifa zimezindua Mfuko wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Ujenzi wa Amani (PBF) ili kusaidia ujenzi wa amani nchini Somalia ukilenga zaidi miradi inayofanywa na serikali.

  • Aina mpya ya mnazi yazinduliwa Kwale,Kenya 2019-02-18

  Wakulima katika ukanda wa Pwani nchini Kenya huenda wakaona faida za kilimo cha minazi kufuatia kuzinduliwa kwa aina mpya ya mnazi katika kaunti ya Kwale.

  Hii ni mara ya kwanza kwa wakulima wa nazi nchini Kenya kupanda aina hii mpya ya minazi iliyoboreshwa.

  • Mkutano wa 32 wa viongozi wa AU wamalizika Addis Ababa 2019-02-12

  Mkutano wa kila mwaka wa viongozi na wakuu wa serikali wa nchi za Afrika umemalizika mjini Addis Ababa Jumatatu baada ya kujadili masuala ya mabadiliko ya taasisi za umoja huo, usalama na suala la wakimbizi. Kwenye mkutano huo, wa siku mbili, rais Paul Kagame wa Rwanda alimkabidhi uwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) rais Abdel Fatah el Sissi wa Misri aliyepokea zamu ya uongozi kwa mwaka mmoja .

  • Rais Kenyatta asisitiza umuhimu wa bara la Afrika kukumbatia Pendekezo la Ukanda mmoja na Njia moja 2019-02-08
  • Wanafunzi wa taasisi wa confucious cho cha Kenyatta wakaribisha mwapa mpya wa kichina 2019-02-05
  • Mkutano wa 20 wa Marais wa EAC wafanyika wiki iliyopita 2019-02-04
  Mkutano wa 20 wa Marais wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, ulifanyika mwishoni mwa juma lililopita, Arusha, Tanzania. Hii ni baada ya kuahirishwa mara mbili mwezi Novemba na Disemba mwaka jana.
  • Kampuni ya ndege ya Zambia yasimamisha usafiri wa kwenda Zimbabwe 2019-01-24

  Kampuni ya ndege ya Zambia jana imetangaza kusitisha safari kati ya mji mkuu ya nchi hiyo Lusaka na mji mkuu wa Zimbabwe, Harare.

  • Rais wa Zambia hataongeza mkataba wa mkuu wa huduma za umma
   2019-01-22

  Rais Edgar Lungu wa Zambia amefanya mabadiliko madogo kwa makatibu wakuu wa nchi hiyo, ambapo ameeleza kuwa hataongeza mkataba wa katibu wa Baraza la Mawaziri la nchi hiyo, Bw. Roland Msiska, unaomalizika tarehe 20 mwezi ujao.

  • Uganda yazindua kituo kikubwa zaidi cha umeme wa kutumia jua katika kanda ya Afrika Mashariki na Kati 2019-01-10

  Rais Yoweri Museveni wa Uganda amezindua kituo kikubwa zaidi cha umeme wa kutumia jua katika kanda ya Afrika Mashariki na Kati, ambacho kina uwezo wa kutoa megawati 20 za umeme.

  • Watu watatu wafariki na wengine 620 kujeruhiwa katika ajali ya treni nchini Afrika Kusini 2019-01-09

  Watu watatu wamefariki na wengine 620 kujeruhiwa baada ya treni mbili za abiria kugongana jana asubuhi nchini Afrika Kusini.

  • Kenya yapanga kuanza kufundisha kichina mashuleni mwaka 2020 2019-01-08

  Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya mitaala ya taifa ya Kenya (KICD) Bw. Julius Jwan, amesema Kenya inapanga kuanzisha mafundisho ya lugha ya kichina kuanzia darasa la nne kwa wanafunzi wanaotaka kujifunza lugha ya Asia katika mwaka 2020, na lugha ya kichina itafundishwa kama lugha ya kigeni pamoja na Kifaransa, Kiarabu na Kijerumani.

  • Kenya yaweka rekodi mwenye mbio za masafa marefu 2018-12-28
  Mwanariadha Eliud Kipchoge ameweka taifa la Kenya kwenye ramani ya dunia kwa mara nyingine tena mwaka huu, kwa kushinda tuzo la mwanariadha bora wa kiume wa mwaka wa 2018. Kipchoge ameshinda mataji mengi sana ila ushindi wake wa mbio za Berlin Marathon na kuweka rekodi mpya ambayo haijawahi kushuhudiwa kwenye mbio hizo, ni jambo ambalo limempa sifa kote duniani.
  • Makubaliano ya kisiasa yasaidia ukuaji wa uchumi na kuleta amani Kenya 2018-12-27
  Mwaka 2018 Kenya imeshuhudia maendeleo makubwa ya kisiasa na kufungua ukarasa mpya katika kukuza amani, mashikamano na kukabiliana na migawanyiko ya kikabila.
  • Kenya na China zaendelelea kukuza ushirikiano wa kunufaishana 2018-12-26
  Ushirikiano wa China na Kenya Mwaka wa 2018 umendelea kupiga hatua mpya ukifaidi watu wa pande hizo mbili.
  • Watu wawili wauawa katika shambulizi la kigaidi dhidi ya makao makuu ya wizara ya mambo ya nje ya Libya 2018-12-25

  Shambulizi la kigaidi lililotokea katika makao makuu ya wizara ya mambo ya nje ya Libya limesababisha vifo vya watu wasiopungua wawili.

  • Kongamano la kwanza la Kimataifa la Uchumi wa rasilimali za majini lafanyika Nairobi 2018-12-25
  Kongamano la kwanza la kimataifa la uchumi endelevu wa rasilimali za majini lilingóa nanga jijini Nairobi katika jumba la mikutano la KICC kuanzia tarehe 26 hadi 28 Novemba 2018.
  • Kenya yajitahidi kutoa huduma bora za afya kwa wote 2018-12-24
  Serikali ya Kenya mwaka 2018 imepiga hatua katika utoaji wa huduma za afya kwa wote na kwa gharama nafuu.
  prev 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 next
  SearchYYMMDD  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako