Mabalozi wa China barani Afrika wapongeza ushirikiano kati ya pande hizo katika kukabiliana na COVID-19 2020-06-17 Mabalozi wa China katika nchi kadhaa za Afrika hivi karibuni wamesema, tangu kutokea kwa mlipuko wa virusi vya Corona, China na Afrika zimeshirikiana kukabiliana na virusi hivyo, na kupata ufanisi mkubwa. Wakati huohuo, urafiki kati ya pande hizo mbili pia umeimarika. |
![]() Wizara ya afya nchini Kenya imetahadharisha kuwa mtu aliye na virusi vya corona lakini hana dalili bado anaweza kuambukiza wengine. Aidha serikali imetoa mwongozo wa kujitenga nyumbani kwa wale wanaotaka kufanya hivyo. |
![]() Hafla ya kukabidhi awamu ya pili ya msaada wa vifaa vya kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona uliotolewa na serikali ya China kwa Zimbabwe imefanyika Ikulu mjini Harare. Akihutubia katika hafla hiyo, Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe amesema msaada wa China utachangia katika kuhimiza kazi ya kinga na udhibiti wa maambukizi ya virusi nchini Zimbabwe. |
![]() 2020-06-04 Mkutano wa tatu wa Bunge la 13 la Umma la China hivi karibuni umepitisha Muswada wa Kujenga na Kukamilisha Mfumo wa Sheria wa Kulinda Usalama wa Taifa Katika Mkoa wenye Utawala Maalumu wa Hong Kong na Utekelezaji wa Mfumo huo. Nchi za Afrika zimeunga mkono hatua hiyo, zikisema ni hatua imara iliyopigiwa na China katika kutunga sheria ya usalama wa taifa mkoani Hong Kong, na itatoa uhakikisho kwa ustawi na utulivu wa muda mrefu wa mkoa huo. |
Afrika CDC yafuatilia kwa karibu mlipuko mpya wa Ebola nchini DRC 2020-06-03 |
![]() Jengo jipya la Taasisi ya mafunzo ya lugha ya kichina katika barabara ya Aboretum jijini Nairobi limekabidhiwa rasmi kwa Chuo Kikuu cha Nairobi. Hafla hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliongozwa na Balozi wa China nchini Kenya Wu Peng na Waziri wa Elimu Kenya,Profesa George Magoha. Jengo hilo lilijengwa na serikali ya China kwa gharama ya Ksh1.4bn. |
![]() Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat amelaani vikali mauaji ya George Floyd nchini Marekani akiwa mikononi mwa polisi, na kuwapa mkono wa pole familia na wapendwa wake. |
![]() Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi hivi karibuni alisema, China na Afrika ni ndugu wakubwa wanaopumua kwa pamoja na wenye hatma ya pamoja. Kauli hiyo imefuatiliwa na nchi za Afrika. Katibu mkuu wa chama tawala cha Kenya Jubilee Bw. Raphael Tuju alipohojiwa na mwandishi wa habari wa Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG amesema, China imepata mafanikio makubwa katika kutokomeza umaskini na kukabiliana na mlipuko wa virusi vya Corona, na uzoefu wake unastahili kuigwa na nchi za Afrika. |
![]() Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amedokeza kuwa nchi hiyo huenda ikafunguliwa hivi karibuni na kuondolewa vikwazo vilivyowekwa ili kudhibiti ueneaji wa maambukizi ya virusi vya Corona. Akizungumza jumamosi katika hotuba yake ya 7 kwa taifa tangu kutangazwa kwa kisa cha kwanza cha Corona nchini humo,Rais Kenyatta alisema ni muhimu kwa wananchi wa Kenya kurejelea shughuli zao za kiuchumi na kuongeza kuwa taifa haliwezi kuendelea kufungwa kwa muda mrefu. |
![]() Licha ya kuwa ni taifa lenya idadi ya juu zaidi ya watu duniani, ambayo ni takriban bilioni 1.3, China imejitahidi na kuhakikisha kwamba robo tatu ya wananchi wake hawako katika hali ya umaskini. Kila mwaka, China imekuwa ikiwaondoa mamilioni ya raia wake katika umaskini. Haya ni kwa mujibu wa bwana Muthiora Kariara, kinara wa chama cha The Great Nationhood Party, na pia mchambuzi wa masuala ya siasa na uchumi kutoka Kenya. |
![]() Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta jumamosi alitoa agizo la kufungwa kwa mipaka ya nchi hiyo na Tanzania na Somalia kutokana na kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya Corona mipakani. Pia aliongeza muda wa zuio la kuingia na kutoka ndani ya kaunti za Nairobi,Mombasa,Kwale,Kilifi na Mandera kwa siku 21 zaidi ili kudhibiti maambukizi ya corona kutoka kaunti moja kwenda nyingine |
![]() Mkurugenzi wa kituo hicho Bw. John Nkengasong amesema wataalamu wa matibabu kutoka nchi 32 za Afrika hivi karibuni walifanya kongamano kwa njia ya mtandao wa Internet na wenzao wa China kuhusu namna ya kupambana na virusi vya Corona barani humo, na kujadili matibabu ya wagonjwa wa COVID-19 mjini Wuhan na dawa za jadi za China zikiwa tiba mbadala. |
![]() Wakati visa vya maambukizo vikiendelea kuongezeka nchini Kenya raia wa Kenya wanaonekana kuchukua tahadhari huku wengine wakiongeza juhudi za kibinafsi katika kukabiliana na virusi hivyo nchini Kenya. |
![]() Kamati ya uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa (ECA) imetoa ripoti ikisema, zuio kamili la mwezi mmoja kwa Afrika litagharimu asilimia 2.5 ya pato la jumla kwa mwaka barani humo, ambayo ni sawa na dola za kimarekani bilioni 65.7. |
![]() Tangu agizo la kutoingia na kutoka katika mtaa wa Eastleigh mjini Nairobi na mji wa kale Mombasa kwa siku 15 zijazo, wengi wa watu kutoka mitaa hiyo wametorokea kwa jamaa zao. Jambo ambalo serikali imetaja kama njia moja ya kuhatarisha maisha ya wengi, hata hivyo Serikali imetoa onyo kali kwa wale wanaendelea kukaribisha watu kutoka maeneo yaliofungwa. |
![]() |
![]() Serikali mbalimbali barani Afrika zinaendelea na jitihada za kutekeleza sera ya kukabiliana na ugonjwa wa Corona.Nchi zinaendelea kufuata maagizo yaliyotolewa na Shirika la Afya Duniani ya kujikinga na Corona pia nchi hizo zikiweka mikakati mengine ya kuzuia kuenea kwa maambukizi ya virusi hivyo. |
![]() Katika mikakati ya kupambana na virusi vya Corona duniani, nchi tofauti zimeweka mikakati tofauti ya kuzuia kuenea kwa virusi hivyo. Nchini Kenya kaunti ya Mombasa Gavana Hassan Joho amezindua kituo cha Matibabu ya virusi vya Corona na imeanza na vitanda 300, lakini inawezo wa vitanda 500. |
![]() Utafiti umeonesha kuwa karibu asilimia 42 ya biashara nchini Afrika Kusini haziwezi kuendelea kutokana na zuio la taifa linalolenga kudhibiti kuenea kwa virusi vya Corona. |
![]() Kaunti ya Mombasa nchini Kenya chini ya uongozi wake Gavana Hassan Ali Joho ni miongoni mwa majimbo yanayomulikwa kwa kila sababu nzuri wakati jimbo hilo likikabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona. |
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |