• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • • Rais wa Zimbabwe asema hatateua mwenyekiti ajaye wa Chama cha ZANU-PF 2017-02-26

  Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe aliyetimiza umri wa miaka 93 hivi karibuni ambaye pia ni katibu mkuu wa chama tawala cha ZANU-PF, amesema kwa sasa hatateua mwenyekiti ajaye wa chama hicho, na kwamba uteuzi huo utafanyika kwenye mkutano wa chama utakaofanyika mwaka 2019.

  • Jeshi la Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo lapambana na kuwaua wapiganaji wa kundi la M23 2017-02-24
  Waasi wa M23 huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wanaripotiwa kusambazwa na jeshi la serkali ya nchi hiyo kupitia mapambano makali yaliyoshuhudiwa wiki hii maeneo ya MATEMBE na KIRINGA wilayani RUTSHURU, mkoani KIVU YA KASKAZINI.
  • Umoja wa Afrika wasisitiza kupinga askari watoto barani Afrika 2017-02-24
  Kamati ya amani na usalama ya Umoja wa Afrika imefanya mkutano wa mawaziri kuhusu utumikishaji wa watoto jeshini.
  • Kampuni ya China yawafadhili wanafunzi wa Kenya kusoma nchini China 2017-02-23
  Serikali ya Kenya na Ubalozi wa China nchini Kenya wamefanya hafla ya kuwaaga wanafunzi 55 wa kikundi cha pili wanaokuja China kuendelea na masomo. Wanafunzi hao watasoma kozi ya reli kwa miaka minne katika chuo kikuu cha mawasiliano cha Beijing chini ya ufadhili wa kampuni ya reli ya China CRBC.
  • Somalia kuimarisha usalama kabla ya kuapishwa kwa rais mpya 2017-02-22
  Serikali ya Somalia imeimarisha usalama mjini Mogadishu na sehemu za karibu, kabla ya rais mpya wa nchi hiyo Mohamed Abdullahi Mohamed kuapishwa leo.
  • Umoja wa Mataifa wasema ukosefu wa chakula umewaathiri wakimbizi milioni 2 barani Afrika 2017-02-21
  Mashirika ya chakula na wakimbizi ya Umoja wa Mataifa yameeleza wasiwasi juu ya ukosefu mkubwa wa chakula unaowakabili wakimbizi wapatao milioni 2 katika nchi 10 barani Afrika.
  • Watu wasiopungua 30 wameuawa kwenye shambulizi la bomu lililotegwa kwenye gari nchini Somalia 2017-02-20
  Watu wasiopungua 30 wameuawa katika shambulizi la bomu lililotegwa kwenye gari lilitokea jana katika soko moja lenye watu wengi Mogadishu.
  • Mjumbe maalum wa rais Xi Jinping wa China ahudhuria sherehe ya kuapishwa kwa rais Adama Barrow wa Gambia 2017-02-19
  • Benki ya Maendeleo ya China yamesaidia maendeleo ya uchumi wa Cote d'Ivoire 2017-02-17

  Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya China Bw Zhang Zhijie amesema, biashara zinazofanywa na Benki hiyo nchini Cote d'Ivoire zitahimiza ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Cote d'Ivoire, na pia kusaidia maendeleo ya uchumi wa nchi hiyo.

  • Sudan Kusini na Uganda kupambana na mafua ya ndege 2017-02-16

  Sudan Kusini na Uganda zimekubaliana kuunda tume ya pamoja ya kusimamia mpaka, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kupambana na kuenea kwa homa ya mafua ya ndege iliyoripotiwa Kampala mwezi Januari.

  • Burundi yawataka wakimbizi wake kurudi nyumbani 2017-02-15

  Serikali ya Burundi imeanzisha kampeni ya kuwataka raia wake kurudi nyumbani licha ya hali ya kisiasa nchini humo kutotulia.

  • China na Msumbiji zaahidi kupanua ushirikiano 2017-02-15
  China na Msumbiji zimeahidi kupanua ushirikiano wa kunufaishana katika maeneo mbalimbali. Ahadi hiyo imetolewa wakati mwenyekiti wa Baraza la mashauriano ya kisiasa la China Bw. Yu Zhengsheng alipokutana na spika wa bunge la Msumbiji Bibi Veronica Macamo ambaye yuko kwenye ziara ya siku tano nchini China.
  • Benki ya dunia yaidhinisha dola milioni 25 kwa ajili ya miradi ya kilimo nchini Kenya 2017-02-14

  Benki ya dunia imepitisha mkopo wa dola za kimarekani milioni 250 kwa ajili ya miradi ya kilimo na kuwasaidia wakulima wadogo wadogo na jamii za wafugaji nchini Kenya.

  • Shirika la ndege la Ethiopia lachukua nafasi ya juu kwa kutochelewesha safari za ndege 2017-02-14
  Shirika la ndege la Ethiopia ambalo ni shirika kubwa zaidi la ndege barani Afrika limechukua nafasi ya 11 duniani kwenye hali ya kutochelewesha safari za ndege katika mwezi wa Januari.
  • Benki za Kenya zalazimika kufunga matawi na kupunguza wafanyakazi kutokana na matumizi ya njia za kidigitali. 2017-02-13

  Benki za Kenya zinafunga baadhi ya matawi yake na kupunguza wafanyakazi, kutokana na kufuata mkakati wa kutimiza njia za kutoa huduma kidigtali na kupunguza gharama za utendaji, baada ya serikali kuweka ukomo kwenye riba.

  • Balozi Tian Xuejun wa China nchini Afrika Kusini apewa tuzo ya Oliver Tambo ya Ubuntu 2017-02-13
  Balozi wa China nchini Afrika Kusini Bw. Tian Xuejun amepewa tuzo ya Oliver Tambo ya Ubuntu ya mafanikio kwenye mambo ya dilpomasia.
  • Watu 17 wafa kwa kukanyagana kaskazini mwa Angola 2017-02-11

  Watu wasiopungua 17 wamefariki na makumi ya wengine wamejeruhiwa kwa kukanyagana jana usiku katika uwanja wa soka mjini Uige, kaskazini mwa Angola.

  • Mahakama kuu ya Kenya yaamua kuwa kufunga kambi ya Dadaab kunakiuka katiba 2017-02-10
  Mahakama Kuu ya Kenya imetoa hukumu kuwa amri ya kufunga kambi ya wakimbizi ya Dadaab iliyotolewa na wizara ya mambo ya ndani ya Kenya inakiuka katiba.
  • Waziri mkuu wa zamani achaguliwa kuwa rais mpya wa Somalia 2017-02-09
  Waziri mkuu wa zamani wa Somalia Bw. Mohamed Abdullahi Farmajo amechaguliwa kuwa rais mpya wa nchi hiyo baada ya kushinda uchaguzi waliokuwa na ushindani mkali uliofanywa huko Mogadishu.
  • Shirika la kulinda wanyamapori Afrika Mashariki laadhimisha miaka 60 tangu lianzishwe 2017-02-08
  Shirika la kuhifadhi wanyama pori la Afrika Mashariki EAWLS limeadhimisha miaka 60 tangu libuniwe. Wakati wa maadhimisho hayo yalioleta pamoja wadau kadhaa wa kulinda mazingira na wanyama pori, waziri wa mazingira nchini humo Judi Wakhungu aliishukuru China kwa hatua yake ya kupiga marufuku uuzaji wa pembe za ndovu.
  prev 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 next
  SearchYYMMDD  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  Maoni yako