• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • • Reli ya SGR ya Kenya yasafirisha abiria elfu 12 katika wiki ya kwanza 2017-06-09

  Kampuni ya reli ya Kenya imesema, hadi kufikia tarehe 7, kwa muda wa wiki moja reli ya SGR iliyojengwa na kampuni ya China imesafirisha abiria karibu elfu 12.

  • Rais wa Zambia akutana na mjumbe wa taifa la China 2017-06-08

  Rais Edgar Lungu wa Zambia jana huko Lusaka amekutana na mjumbe wa taifa wa China Bw. Wang Yong ambaye yuko ziarani nchini humo.

  • China yatoa msaada wa dola milioni tano kwa wakimbizi wa Kakuma Kenya 2017-06-08

  Balozi wa China nchini Kenya Bw Liu Xianfa amesema serikali ya China itaendelea kutoa msaada wa kibinadamu ili kuboresha maisha ya wakimbizi kwenye maeneo mbalimbali nchini Kenya.

  • Mgomo wa manesi watishia sekta ya afya nchini Kenya 2017-06-07

  Siku moja tu baada ya chama cha wauguzi nchini Kenya kutangaza mgomo wakenya ambao walifika kwenye hospitali mbali mbali wameelezea kusikitishwa kwao na hatua ya wauguzi hao na kuitaka serikali kufanya kila iwezalo kuhakikisha wanapata matibabu. Katika hospitali ya Samburu wagonjwa walionekana kutaabika huku wasijue watakalofanya baada ya kukosa huduma za wauguzi. John Lepere ambaye anaugua ugonjwa wa Malaria anaonekana akisaidiwa na mke wake baada ya wauguzi kugoma.

  • Rais wa Niger akutana na mjumbe wa taifa wa China 2017-06-04

  Rais Mahamadou Issoufou wa Niger amekutana na mjumbe wa taifa wa China Bw. Yang Yong mjini Niamey.

  • Rwanda yatafuta uwekezaji kwenye nyumba za bei nafuu 2017-06-02
  Wizara ya miundombinu ya Rwanda imesema Rwanda inatafuta wawekezaji wa nje na wa ndani kwenye sekta ya nyumba za bei nafuu kutokana na ongezeko la watu wa mjini.
  • Treni ya SGR ya kutoka Mombasa-Nairobi iliyojengwa kwa msaada wa China yazinduliwa rasmi 2017-05-31

  Siku moja tu baada ya kuzindua treni ya mizigo rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amezindua tena treni ya kisasa ya abiria iliyojengwa kwa msaada wa China.

  • Shirika la reli la Kenya lasaini makubaliano na kampuni ya China kuhusu uendeshaji wa reli 2017-05-31

  Shirika la reli la Kenya KRC na kampuni ya CRBC ya China wamesaini makubaliano ya usimamizi, ukarabati na huduma kuhusu reli iliyozunduliwa ya Mombasa-Nairobi.

  • Kampuni ya ujenzi ya China inayoshughulikia ujenzi wa SGR nchini Kenya yatangaza ripoti ya majukumu ya jamii 2017-05-30
  Wakati Reli ya SGR ya kutoka Mombasa-Nairobi nchini Kenya inakaribia kuanza kazi rasmi, kampuni ya ujenzi ya China iliyoshughulikia ujenzi wa reli hiyo iliandaa mkutano na kutoa ripoti ya majukumu ya jamii ya mwaka 2016 na ya mradi wa reli ya SGR mjini Nairobi, Kenya. Hii vilevile ni mara ya kwanza kwa kampuni ya China kuandaa mkutano kama huu nje ya China.
  • Wakenya wajiandaa kwa uzinduzi wa reli ya Mombasa Nairobi 2017-05-30

  Reli ya SGR kutoka Mombasa hadi Nairobi itazinduliwa kesho, uzinduzi utakaohudhuriwa na Rais Uhuru Kenyatta na mjumbe wa taifa wa China Bw Wang Yong.

  • Ushirikiano kati ya China na Kenya waingia kwenye njia ya kasi 2017-05-29

  Reli ya SGR kutoka Mombasa kwenda Nairobi, ambayo ni reli ya kwanza iliyojengwa tangu Kenya ipate uhuru, inatarajiwa kuzinduliwa mwishoni mwa mwezi huu. Reli hiyo inayoitwa na wakenya "ujenzi wa milenia" imejengwa kwa kufuata vigezo vya kichina, na inabeba ndoto ya watu wa vizazi vilivyopita vya Kenya, na kusaidia kuhimiza maendeleo ya uchumi na jamii ya Afrika Mashariki kuingia kwenye njia ya kasi.

  • Polisi nchini Kenya yawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kuhusika na mashambulizi 2017-05-25
  Vikosi vya usalama nchini Kenya vinawahoji watu wawili muhimu wanaotuhumiwa kuhusika na matukio ya kigaidi yaliyotokea hivi karibuni katika kaunti za Garissa na Mandera, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo wiki mbili zilizopita.
  • Bw. Tedros Adhanom wa Ethiopia achaguliwa kuwa mkuu mpya wa WHO 2017-05-24
  Bw. Tedros Adhanom kutoka Ethiopia amechaguliwa kuwa mkurugenzi mkuu wa Shirika la afya duniani WHO.
  • Kongamano la maonesho ya biashara na viwanda Afrika Mashariki laanza mjini Kigali,Rwanda 2017-05-23

  Kongamano la pili la maonesho ya Biashara ya Viwanda Afrika Mashariki (East Africa Manufacturing Business Summit-EAMBS) limeanza rasmi hii leo tarehe 23 katika hoteli ya Serena jijini Kigali,Rwanda. Kongamano hili linawaleta pamoja wamiliki wa viwanda,wafanyabiashara na wawekezaji kwa lengo la kukuza biashara kati ya mataifa ya Afrika Mashariki.

  • Shule ya Mwatate  Sino-Africa yatoa matumaini kwa mtoto wa kike Taita 2017-05-22
  Kwa mwaka wa  pili sasa shule ya ya  Mwatate  Sino-Africa iliojengwa kwa msaada wa China nchini Kenya imeendelea kupokea wanafunzi zaidi wa kike.
  Shule hii imekuwa ni ishara ya kuendeleza urafiki wa tangu jadi wa Kenya na China kwenye sekta ya elimu.
  • Waziri wa mambo ya nje wa China akutana na mwenzake wa Mali huko Bamako 2017-05-22
  Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi ambaye yuko ziarani nchini Mali, jana mjini Bamako alikutana na mwenzake wa Mali Bw. Abdoulaye Diop.
  • Rais na waziri mkuu wa Cape Verde wakutana na waziri wa mambo ya nje wa China 2017-05-21

  Rais Jorge Carlos Fonseca wa Cape Verde na waziri mkuu Jose Ulisses Correia e Silva tarehe 20 kwa nyakati tofauti walikutana na waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi mjini Praia.

  • Kenya kuagiza mahindi kutoka nje ili kupunguza uhaba wa chukula 2017-05-19
  Waziri wa kilimo, mifugo na uvuvi wa Kenya Dkt Richard Lesiyampe amesema, jumamosi wiki hii mahindi hayo yatafikishwa kwenye wilaya ya Moyale kwenye mpaka kati ya Kenya na Ethiopia.
  • Kampuni za China zafungua nafasi za ajira Kenya 2017-05-18
  Kuendelea kuongezeka kwa uwekezaji wa kampuni za China nchini Kenya kumesaidia kupunguza ukosefu wa ajira hasa kwa vijana. Kulingana na taakwimu hadi sasa nchini Kenya kuna zaidi ya kampuni 300 za China kwenye sekta za ujenzi, utengenezaji bidhaa, na utoaji huduma zote zikitoa ajira kwa wakenya. Taakwimu zinaonyesha kwamba karibu kila kampuni ya China inaajiri asilimia 70 ya wenyeji.
  • WHO yasema iko tayari kutoa chanjo ya ebola DRC 2017-05-17
  Shirika la afya duniani WHO limesema linafanya uchunguzi na tathmini kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa ebola nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, ili kuamua kama litatumia au la chanjo mpya kudhibiti ugonjwa huo.
  prev 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 next
  SearchYYMMDD  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako