![]() 2020-04-19 Hivi karibuni, licha ya vikundi vya madaktari vilivyotumwa na China katika nchi za Afrika, misaada ya vifaa vya matibabu dhidi ya ugonjwa wa COVID-19 iliyotolewa na China pia imefurahiwa na nchi za Afrika. |
![]() Waziri wa mambo ya nje wa Nigeria Geoffrey Onyeama na Balozi wa China nchini humo Zhou Pingjian jana walikutana na waandishi wa habari kwa pamoja, na kufafanua hali halisi kuhusu kile kinachoitwa "Wanigeria kutendewa vibaya mjini Guangzhou", na kutoa taarifa ya hali ilivyo sasa ya raia wa Nigeria waliowekwa karantini huko Guangzhou. |
![]() Hivi karibuni, taarifa nyingi zilizagaa kuhusu ubaguzi wa rangi dhidi ya raia wa Afrika mjini Guangzhou, mji wenye idadi kubwa ya Waafrika, wakati China ikizingatia sana kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona kutoka nje. |
Uchambuzi:Maambukizi ya virusi vya Corona yaathiri vibaya uchumi wa Afrika 2020-04-07 Nchi mbalimbali za Afrika zimepunguza makadirio ya ongezeko la uchumi la mwaka huu kwa kiasi kikubwa kutokana na athari mbaya ya uenezi wa kasi wa virusi vya Corona kwa uchumi wa Afrika. Wachambuzi wanaona kuwa, mfumo wa afya na matibabu barani Afrika ni dhaifu, muundo wa uchumi ni rahisi na usio na unyumbufu , hivyo maambukizi ya virusi hivyo yataleta changamoto kubwa kwa uchumi wa Afrika. |
![]() Serikali za kaunti nchini Kenya zinachukua hatua mbalimbali za tahadhari ili kukabiliana na athari za maambukizi ya virusi vya Corona. Serikali ya kaunti ya Nandi imezindua matrekta kwa ajili ya wakulima kufanya upanzi ili kuwa na chakula cha kutosha wakati huu wa maambukizi ya virusi vya Corona. Khamis Darwesh anaripoti. |
![]() Vifaa vingi vya matibabu vilivyochangiwa na Mfuko wa Jack Ma na Mfuko wa Alibaba kutoka China, ikiwemo mask, vitendanishi, nguo na miwani ya kujikinga, vinasambazwa kwa nchi zote za Afrika. |
![]() Sekta ya biashara ya maua nchini Kenya imeathirika kutokana na kukosekana kwa soko la bidhaa hiyo kufuatia mlipuko wa maambukizi ya virusi vya CORONA CORONA. |
![]() Mradi wa kukarabati hospitali ya kutibu virusi vya Corona ya Wilkins ya Zimbabwe uliofadhiliwa na kutekelezwa na kampuni ya China umekamilika na kukabidhiwa rasmi jana Jumatatu. |
![]() Wakati nchi za Afika zinafunga mipaka kutokana na hofu ya athari ya maambukizi ya virusi vya Corona, bilionea wa China ambaye ni mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Alibaba ya China, Bw. Jack Ma ameahidi kutoa vifaa vya upimaji zaidi ya milioni moja kwa bara hilo. |
![]() Siku hizi, kuna watoa maoni wengi wametumia methali ya Kiswahili ya "Tembo mbili wakipigana zinazoumia ni nyasi" kueleza wasiwasi wao kuwa kama China na Marekani zinapopambana, nchi za Afrika zitaumia. |
![]() Habari kutoka kituo cha kinga na udhibiti wa ugonjwa cha Afrika, zinasema kuwa mpaka sasa wagonjwa karibu 640 wameripotiwa katika nchi 34 za Afrika. |
Tiba ya jadi ya kichina inapata umaarufu barani Afrika wakati wa mlipuko wa COVID-19 2020-03-19 Sekta ya afya nchini Namibia imetoa kibali kwa tiba ya jadi ya kichina (TCM) nchini humo. Ilimchukua Peng Wang, raia wa China anayetibu kwa kutumia dawa za asili za China mjini Windhoek, Namibia, miaka mitatu kwa tiba hiyo kusajiliwa na sekta ya afya nchini humo. Machi 6 mwaka huu, Shirikisho la Mfuko wa Msaada wa Afya nchini Namibia lilitoa kibali hicho, na kuifanya Namibia kuwa nchi ya karibuni katika mlolongo wa nchi za Afrika ambazo zinachanganya tiba ya jadi ya kichina katika mfumo wao wa afya. Uamuzi huo umekuja wakati tiba za jadi zikidhihirisha uwezo wake kuwatibu watu walioambukizwa virusi vya korona (COVID-19) nchini China. |
![]() Wakati Kenya imethibitisha mtu wa nne kuambukizwa virusi vya Korona, ambaye aliwasili Kenya tarehe 9 Machi kutoka Uingereza, Balozi wa China nchini Kenya Bw. Wu Peng amesema China itachangia uzoefu na vifaa kwa nchi za Afrika katika kupambana na maambukizi ya COVID-19. |
![]() Idadi ya maambukizi ya nimonia ya COVID-19 inayosababishwa na virusi vya korona imezidi 100 katika Eneo la Afrika Kusini mwa Sahara, ambako nchi zaidi ya 20, zikiwemo Afrika Kusini, Nigeria na Ethiopia, zimeripoti visa vya maambukizi na kuchukua hatua kupambana na ugonjwa huo. |
![]() Rais Uhuru Kenyatta amethibitisha kupatikana kwa visa vingine viwili vya maambukizi ya virusi vya Korona nchini Kenya. Akihutubia Taifa jana Rais Kenyatta amesema watu hao wamethibitishwa baada uchunguzi uliofanywa kwa 27 waliokaribiana na mgonjwa wa kwanza wa virus hivyo nchini Kenya. Rais Kenyatta amesema vikundi vya madaktari vinawafuatilia kwa karibu watu waliokaribiana na mtu huyo. |
![]() Wakati dunia inakabiliwa na maambukizi ya ugonjwa wa nimonia inayosababishwa na virusi vipya vya korona COVID-19, uzoefu wa China wa kukinga na kutibu ugonjwa huo umekuwa msaada mkubwa. Waziri wa afya na ustawi wa watoto wa Zimbabwe Bw. Obediah Moyo amesema, nchi hiyo inaiga uzoefu wa China, ili kuzuia ugonjwa wa COVID-19 usienee nchini Zimbabwe. |
![]() Cameroon leo imethibitisha kuwa na kesi ya kwanza ya virusi vya korona (COVID-19), na kuifanya kuwa nchi ya nne baada ya Nigeria, Senegal na Afrika Kusini kuripoti kesi ya ugonjwa huo hii leo katika kanda ya Afrika kusini mwa Sahara. |
![]() Maambukizi ya ugonjwa wa nimonia inayosababishwa na virusi vipya vya korona COVID-19 yameanza kuenea katika nchi za Afrika, na jana, Senegal, Morocco na Tunisia kwa nyakati tofauti zimeripoti mgonjwa kwa kwanza wa COVID-19. Nchi za Afrika zinajiandaa kupambana na maambukizi hayo. |
![]() Umoja wa Mataifa umeonya kuwa serikali ya Ethiopia inashindana na wakati kudhibiti uvamizi wa nzige wa jangwani unaoendelea, wakati msimu wa mavuno wa kuanzia Februari hadi Mei ukianza. |
![]() Meneja mkuu wa uendeshaji wa reli ya SGR wa kampuni ya Afistar Bw. Li Jiuping, amesema reli ya SGR ya Kenya imeleta manufaa kwa jamii na uchumi wa Kenya. |
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |