![]() Takribani wanafunzi 400 kutoka Afrika wanaosoma vyuo vikuu vya China wamejitokeza kwenye maonyesho ya nafasi za ajira kwenye makampuni ya China yanayofanya kazi zake katika mataifa mbalimbali barani Afrika. |
![]() 2017-11-15 Saa saba usiku wa kuamkia leomilipuko imesikika mjini Harare, Zimbabwe. Baadaye jeshi la nchi hiyo lilitoa taarifa kwa njia ya televisheni, likikanusha kuwa limefanya uasi, na kusema rais Robert Mugabe yuko salama, na kuwataka raia wote wadumishe utulivu. |
![]() 2017-11-14 Somalia imeahidi kuzidisha operesheni za kijeshi dhidi ya wapiganaji wa kundi la Islamic State (IS) na Al Shabaab ili kuleta utulivu nchini humo. |
![]() Watu wasiopungua 34 wamefariki na wengine zaidi ya 26 kujeruhiwa baada ya treni moja yenye mabehewa 13 kuanguka kusini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). |
![]() Huu ni mwaka wa pili tangu shirika la ndege la China Southern Airlines kuzindua safari zake nchini Kenya. Shirika hili la ndege ambalo linaongoza katika ukanda wa Asia kwa usalama kwenye usafiri, una safari kwa zaidi ya maeneo 40, barani Afrika. Nchini Kenya, shirika hili limeshuhudia ongezeko la abiria wakenya na idadi hii inazidi kuongezeka. |
![]() Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amemfuta kazi makamu wake Bw Emmerson Mnangagwa kwa kile alichodai ni utovu wa nidhamu.Akitangaza uamuzi wa Rais Mugabe, waziri wa habari wa nchi hiyo, Bw Simon Moyo, amesema katiba ya Zimbabwe inampa Rais madaraka ya kufanya hivyo. |
![]() Ubalozi mdogo wa China uliopo Zanzibar jana umefanya hafla ya kutoa msaada wa vitu kwa kituo cha watoto yatima. Watu zaidi ya 100 wakiwemo mke wa balozi mdogo wa China Bibi Liu Jie, mke wa rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, maofisa wa idara za serikali ya Zanzibar zinazoshughulikia mambo ya wanawake, afya na michezo, madaktari wa China wanaotoa msaada huko, walimu na wanafunzi wa Chuo cha Confucius, walimu na watoto wa kituo cha watoto yatima wamehudhuria hafla hiyo. |
![]() Rais Uhuru Kenyatta ametangazwa mshindi katika marudio ya uchaguzi mpya wa urais uliofanyika tarehe 26 Oktoba nchini Kenya. |
![]() Licha Ya juhudi zinazoendeshwa na serikali Ya jamhuri Ya kidemokrasia Ya kongo kuhakikisha eneo la mashariki mwa nchi hiyo linakuwa salama, makundi korofi bado yanaendelea kuhatarisha usalama wa watu na mali zao. Jana kundi la waasi kutoka Uganda ADF lilifanya mashambulizi mawili tofauti mjini Beni. Moja kwenye Hospitali, na la pili kwenye kambi ya jeshi maeneo ya mjini, na kuleta taharuki iliyofanya baadhi ya watu kukimbia makazi yao |
![]() Kenya leo imeandaa uchaguzi mpya wa urais ambao umesusiwa na upinzani. Wafuasi wa upinzani wamekuwa wakifanya maandamano kupinga uchaguzi huo huku polisi wakiimarisha doria katika maeneo mengi nchini humo. |
![]() Shirika linalosimamia biashara ya wanyama na mimea yenye hatari ya kutoweka (CITES) limesema ujangili wa tembo barani Afrika umepungua kwa miaka mitano mfululizo, na kupungua huko kwenye nchi za Afrika kumefikia kiwango cha kabla ya mwaka 2008. |
![]() Zimbabwe imelaani hatua ya hivi karibuni ya Shirika la Afya Duniani WHO ya kumvua ubalozi wa heshima Rais wa nchi hiyo Robert Mugabe, na kusema kama angeambiwa mapema kuhusu kuteuliwa huko angekataa. |
![]() Mkutano wa 7 wa kimataifa wa viongozi wa eneo la maziwa makuu la Afrika ulifunguliwa jana Brazaville nchini Jamhuri ya Kongo, viongozi waliohudhuria mkutano huo walifuatilia hali ya usalama ya sehemu ya mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, na kuitaka jumuiya ya kimataifa isaidie kutimiza mchakato wa amani wa nchi hiyo na kuondoa matishio yote ya makundi haramu yenye silaha kwenye sehemu ya mashariki mwa nchi hiyo. |
![]() Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ya Kenya Bw Wafula Chebukati, amesema ni vigumu kuhakikisha kuwa uchaguzi mkuu wa Kenya uliopangwa kufanyika tarehe 26 Oktoba kuwa utakuwa huru na wa haki. |
![]() Ofisa wa Tume Huru ya Uchaguzi ya Kenya IEBC Bibi Roselyn Akombe amejiuzulu, huku akitoa wito kusimamisha uchaguzi wa urais utakaofanyika wiki ijayo. |
![]() Awamu ya kwanza ya tamasha la kimataifa la filamu lza China na Afrika lilifunguliwa jana usiku huko Cape town nchini Afrika Kusini. Watu wa sekta ya filamu kutoka China, Afrika Kusini, Boswana, Tanzania, Ghana, Namibia na Nigeria walikusanyika na kuonesha mafanikio ya sekta ya filamu na kubadilishana uzoefu wa utengenezaji wa filamu. |
![]() Mke wa rais wa Sierra Leone Bibi Sia Nyama Koroma akishirikiana na Shirika la utengenezaji wa bidhaa za watoto la China Beingmate wamekabidhi maziwa ya unga ili kuwapatia virutubisho watoto zaidi ya elfu 20 wenye umri wa mwaka 1 hadi miaka 5 na mama wanaonyonyesha wa huko. |
![]() Waziri wa ulinzi wa Somalia Abdirashid Abdullahi Mohamed na mkuu wa jeshi la nchi hiyo Ahmed Mohamed Jimale wamejiuzulu jana. Waziri wa habari wa Somalia Abdirahman Omar Osman amethibitisha kujiuzulu kwao na kusema waziri wa ulinzi alijiuzulu kwa sababu binafisi, lakini hakudokeza sababu ya kujiuzulu kwa mkuu wa jeshi, miezi sita tu baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo. |
![]() Maelfu ya wafuasi wa upande wa upinzani nchini Kenya NASA wamerudi tena katika mitaa ya jiji la Nairobi na miji mingine mikubwa katika maandamano ya kupinga Tume ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya (IEBC) kabla ya marudio ya uchaguzi wa rais utakaofanyika tarehe 26 mwezi huu. |
![]() Takriban watu 40,miongoni mwao watoto wanne kutoka kaunti 5 nchini Kenya wamethibitishwa kufariki kutokana na Ugonjwa wa malaria. |
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |