![]() Kampeni ya fasihi ya China "China Shelf" imewasili Afrika jumatano, ambapo ujumbe wa China katika Tamasha la Kimataifa la Vitabu la Nairobi ulifanya hafla ya kusaini makubaliano ya ushirikiano na upande wa Kenya, huku mamia ya vitabu vinavyoeleza mafanikio ya China vikionyeshwa. |
![]() Msemaji wa serikali ya Kenya Cyrus Oguna amesema serikali itagharamia matibabu ya wanafunzi waliojeruhiwa baada ya shule yao kuporomoka katika mji mkuu Nairobi. Wanafunzi 7 walifariki kwenye mksasa huo wa Jumatatu, huku wengine 57 wakijeruhiwa. |
![]() Shirika la Afya Duniani (WHO) limezitaka mamlaka nchini Tanzania kutoa taarifa za matokeo ya vipimo vilivyofanywa hivi karibuni kuhusu kile kilichoelezwa kuwa ugonjwa wa ajabu uliosababisha vifo vya watu wawili nchini humo. |
![]() Mwanasiasa wa Zimbabwe, ambaye alikuwa waziri wa elimu ya msingi na waziri wa ajira wa Zimbabwe Bibi Fay Chung hivi karibuni alisema kutokana na China kushikilia na kuendeleza utaratibu wa ujamaa wenye umaalumu wa China na kupata njia ya kujiendeleza inayoifaa, China imekuwa na sura mpya ambayo imeonyesha uhai mkubwa wa maendeleo. |
![]() Habari kutoka Mkutano wa 5 wa baraza la uwekezaji barani Afrika uliofanyika mjini Brazzaville, Jamhuri ya Kongo zinasema kuwa, mfuko wa maendeleo ya China na Afrika umewekeza dola za kimarekani bilioni 5 katika nchi 36 za Afrika, na kuhimiza kampuni za China kuwekeza zaidi ya dola za kimarekani bilioni 24 barani humo. |
![]() China imetoa mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa nchi ya Tanzania kupitia uwekezaji, msaada na ujenzi wa miradi mbali mbali ya maendeleo. Mfano wa hivi karibuni wa mchango wa Uchina kwa Tanzania ni maktaba kubwa zaidi ya katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam. |
![]() Mwili wa Rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe, aliyekufa nchini Singapore Ijumaa iliyopita akiwa na umri wa miaka 95, umefika Zimbabwe jana Jumatano alasiri kabla ya mazishi yake yaliyopangwa kufanyika Jumapili. Wanasiasa akiwemo rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe na mamia ya raia wamepokea mwili wa Mugabe kwenye uwanja wa ndege. |
![]() Rais wa zamani wa Zimbabwe Robet Mugabe amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 95. Tangu Mugabe aingie madarakani mwaka 1980, Zimbabwe imeiunga mkono kithabiti China katika masuala mbalimbali yakiwemo Taiwan, Tibet na haki miliki, na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili umeendelea vizuri katika uchumi, biashara, elimu, utamaduni, sayansi na sekta nyinginezo. Bw. Mugabe aliwahi kusema wazimbabwe hawatasahau msaada wa dhati wa China katika mchakato wa kupigia ukombozi wa Zimbabwe. Yafuatayo ni baadhi ya mambo wanayojua wachina kuhusu Bw. Mugabe. |
![]() Waziri wa Mkuu wa Sudan Bw. Abdalla Hamdok ametangaza uundaji wa baraza la mawaziri la mpito, ambalo ni la kwanza tangu rais Omar al-Bashir kuondolewa madarakani. Bw. Hamdok ametangaza uundaji huo katika mkutano na wanahabari uliofanywa huko Khartoum, huku akinukuu amri ya katiba iliyotolewa na mwenyekiti wa baraza la utawala. |
![]() Kwa mujibu wa Ripoti ya Ushindani wa usafiri na utalii TTCR, Afrika Kusini imekuwa moja ya nchi zinazoshika nafasi za mwanzo kwenye sehemu ya kusini mwa Sahara barani Afrika. |
![]() Mtaalamu wa mazingira wa Afrika Kusini Marian Nieuwoudt jana alisema, miji kando ya bahari ikiwemo Cape Town imeathiriwa na kuongezeka kwa kiwango cha bahari kutokana na mabadiliko ya tabia nchi, na wakazi wa sehemu kadhaa wanalazimika kupanga kuhamia kwenye sehemu za juu zaidi katika siku za baadaye. |
![]() Watu wanaoishi na ulemavu wa ngozi nchini Kenya, wameomba kutambuliwa katika zoezi la kuhesabu watu linaloendelea nchini humo. Wakingozwa na mwenyekiti wao Ddt. Isaac Mwaura watu hao wamesema pia kuhesabiwa kwao kutakisaida chama chao kuwafuatilia na kuhakikisha wanapata nafasi na huduma za serikali kama raia wengine. |
Uhusiano na China utachangia mafanikio ya AfCFTA 2019-08-26 Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara nchini Ghana (GUTA) Bw. Joseph Obeng amesema, uhusiano wa kimakakti na China utachangia mafanikio ya Eneo la Biashara Huria barani Afrika (AfCFTA). |
![]() Kutokana na mwaliko wa wizara ya afya ya Zimbabwe, timu ya 17 ya madaktari ya kuisaidia Zimbabwe ya China imeweka kibanda cha maonyesho ya dawa za jadi za Kichina kwenye Maonyesho ya Kilimo ya Zimbabwe ya mwaka 2019, ikiwa ni mara ya kwanza kwa bidhaa hizo kuonyeshwa kwenye maonyesho hayo. |
![]() China imeanzisha taasisi 59 na madarasa 41 ya Confucious katika nchi 44 za Afrika hadi kufikia mwezi Juni mwaka huu, na kutoa nafasi za kujifunza lugha ya kichina kwa watu wa nchi hizo. Taasisi ya Confucious iliyopo katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya ilianzishwa mwezi Disemba mwaka 2005, na katika miaka 14 iliyopita imeandikisha wanafunzi zaidi ya elfu 15. |
![]() Polisi wa Sudan na Sudan Kusini wamesaini makubaliano ya ushirikiano ili kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili. |
![]() Rais John Magufuli wa Tanzania amesema taifa lake siyo maskini na nlitaendelea kufanya maamuzi katika kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo bila kuwategemea wahisani. Rais Magufuli amesema hayo katika uzinduzi wa jengo la tatau la abiria katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere uliofanyika jana. |
![]() Ofisa wa jeshi la Polisi la Somalia ambaye hakutaka kutaja jina lake amesema, maofisa sita wameuawa na wengine saba akiwemo meya wa mji wa Mogadishu wamejeruhiwa katika shambulizi la bomu la kujitoa mhanga lililotokea kwenye makao makuu ya manispaa ya mji wa Mogadishu. |
![]() Maofisa afya nchini Somalia wamethibitisha kuwa, idadi ya vifo vilivyotokana na mlipuko wa bomu lililotegwa kwenye gari huko Mogadishu, imeongezeka na kufikia 17, na watu wengine 28 kujeruhiwa. |
![]() Baraza la mpito la kijeshi la Sudan na kundi la upinzani wamesaini makubaliano ya awali kuhusu azimio la kisiasa, linalotaja miundo ya kipindi cha mpito. |
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |