• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • • Wasichana 82 waachiliwa na wapiganaji wa Boko Haram 2017-05-07

  Wasichana 82 wa Chibok wameachiliwa na wapiganaji wa Boko Haram na wanatarajiwa kupokelewa na Rais Muhamadu Buhari wa Nigeria.

  • Watu 32 wafariki katika ajali ya barabarani nchini Tanzania 2017-05-06

  Wanafunzi 29 wa shule ya Lucky Vincent wamefariki katika ajali ya barabarani wakielekea mjini Karatu nchini Tanzania kwa ziara ya kimasomo. Vyombo vya habari nchini humo vinaripoti kwamba ni watoto walimu 2 na dereva wa basi hilo la shule wamefariki pia.

  • Mauritus yatarajia kuwa jukwaa la China katika kuwekeza barani Afrika 2017-05-05
  Waziri mkuu wa Mauritus Bw. Pravind Jugnauth hivi karibuni alisema kuwa pendekezo la Ukanda mmoja na Njia moja limeziletea nchi nyingi fursa ya maendeleo
  • China yasisitiza ahadi ya kulinda wanyamapori Afrika 2017-05-04

  Ofisa wa China amesema China itaendelea kutoa uungaji mkono kwa ulinzi wa wanyamapori barani Afrika.

  • Kenya na Somalia kuimarisha ushirikiano katika mapambano dhidi ya ugaidi 2017-05-03
  Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amesema uhusiano wa karibu kati ya Kenya na Somalia utaziwezesha nchi hizo mbili kukabiliana kwa pamoja na tishio la ugaidi na changamoto nyingine.
  • Kenya yaongeza mshahara wa kima cha chini kwa asilimia 18 2017-05-02
  Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ametangaza kuongeza kima cha chini cha mshahara kwa asilimia 18, ili kuwapunguzia watu wenye mapato ya chini athari zinazotokana na mfumuko wa bei uliofikia asilimia 11.5 katika miezi 57 iliyopita.
  • Umoja wa Afrika wazitaka pande zinazopigana Sudan Kusini ziache kuchochea vurugu 2017-05-01

  Umoja wa Afrika umezitaka pande zinazopambana za Sudan Kusini ziache kuchochea ghasia na vurugu nchini humo. Mwenyekiti wa kamati ya Umoja huo Bw. Moussa Faki Mahamat ameeleza wasiwasi wake kuhusu ongezeko la mapambano ya kijeshi hasa katika eneo la Upper Nile.

  • Rais wa Sierra leone aahidi kukabidhi madaraka kwa amani kwa mrithi wake mwaka ujao 2017-04-28

  Rais Ernest Bai Koroma wa Sierra Leone amesema kuwa mwaka ujao ataondoka madarakani na kukabidhi madaraka kwa amani kwa mrithi wake.

  • Upinzani Kenya wamteua mgombea wa urais 2017-04-28
  Vyama vya upinzani nchini Kenya ambavyo viko chini ya muungano wa National Super Alliance (NASA) vimemteua aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga kuwa mgombea wa urais katika uchaguzi mkuu Agosti 8 mwaka huu.
  • Naibu waziri mkuu wa China atoa wito kwa vijana wa China na Afrika kuendeleza urafiki kati ya pande hizo 2017-04-27

  Naibu waziri mkuu wa China Bibi Liu Yandong amehudhuria na kutoa hotuba kwenye ufungaji wa tamasha la pili la vijana wa China na Afrika lililofanyika mjini Pretoria, Afrika Kusini.

  • Bibi Liu Yandong ahudhuria ufunguzi wa mazungumzo ya ngazi ya juu kati ya China na Afrika kusini 2017-04-26
  Naibu waziri mkuu wa China Bibi Liu Yandong amehudhuria ufunguzi wa mazungumzo ya ngazi ya juu kati ya China na Afrika kusini uliofanyika jana mjini Pretoria, Afrika Kusini.
  • China na Afrika Kusini zaanzisha ushirikiano wa maeneo ya sayansi na teknolojia 2017-04-25
  China na Afrika Kusini zimezindua rasmi ushirikiano wa maeneo ya sayansi na teknolojia, ikiwa ni juhudi za kuimarisha ushirikiano wa pande mbili wa sayansi na teknolojia.
  • Wanafunzi wa Uganda waliosoma nchini China na wajumbe wa makampuni ya China nchini Uganda wafanya mkutano 2017-04-24

  Wanafunzi karibu 100 wa Uganda waliorejea baada ya kumaliza masomo yao nchini China na wajumbe wa makampuni ya China nchini Uganda wamekutana jana katika ofisi za ubalozi wa China nchini Uganda.

  • Kenya yasema iko mbioni kuweka mafunzo ya lugha ya kichina kwenye mtaala wa elimu ya shule za msingi 2017-04-21

  Naibu mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya maendeleo ya elimu ya Kenya KICD anayeshughulikia elimu ya msingi Bw. David Njeng'ere amesema, wizara ya elimu ya Kenya inakamilisha taratibu za kuweka mafunzo ya kichina kwenye mtaala wa masomo nchini Kenya.

  • Tanzania kuboresha majukwaa na bandari kwenye maziwa makubwa matatu 2017-04-20

  Tanzania inapanga kuyafanyia ukarabati majukwaa na bandari kwenye maziwa Viktoria, Tanganyika na Nyasa kwa mwaka ujao wa fedha, ili kuboresha usafiri kwenye maziwa hayo.

  • Tanzania yapanga kuonyesha nyayo mpya za binadamu kwenye majumba ya makumbusho 2017-04-18

  Tanzania inapanga kuonyesha nyayo za binadamu wa kale, zilizogunduliwa hivi karibuni katika eneo la Laetoli kwenye hifadhi ya Ngorongoro.

  • Rais wa Afrika Kusini akataa kuondoka madarakani 2017-04-17
  Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini amekataa mwito wa kumtaka aondoke madarakani, akisema hatma yake inatakiwa kuamuliwa na wananchi.
  • Rais wa Rwanda ashukuru China kwa kuchangia maendeleo ya nchi hiyo 2017-04-14

  Rais Paul Kagame wa Rwanda amesema urafiki kati ya nchi yake na China ni wa muda mrefu, na serikali na wananchi wake wanashukuru China kwa kuchangia maendeleo ya taifa hilo.

  • China yatoa wito kwa nchi za Maziwa Makuu kushirikiana kiusalama 2017-04-13

  Naibu balozi wa China kwenye Umoja wa Mataifa Wu Haitao amesema China inazipongeza nchi za Maziwa Makuu kwa kushirikiana katika kukabiliana na tishio linalotokana na makundi yenye silaha, na kuhamasisha nchi za kanda hiyo kuongeza ushirikiano katika sekta ya usalama.

  • Msanii wa Zimbabwe ashirikiana na wasanii kutoka nchi nyingine ikiwemo China kutengeneza wimbo 2017-04-12

  Msanii wa kimataifa wa Zimbabwe Bw. Abraham Matuka atatoa wimbo wa ushirikiano wa kimataifa mwezi huu, wenye lengo la kuhimiza utalii wa Zimbabwe na maelewano ya kiutamaduni kati ya nchi mbalimbali.

  prev 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10
  SearchYYMMDD  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako