• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • • Miradi 19 ya mpango wa nishati mbadala yazindua barani Afrika 2017-03-06
  Waziri wa mazingira, nishati na bahari wa Ufaransa Bibi Segolene Royal amesema, miradi 19 ya mpango wa nishati mbadala imezinduliwa hivi karibuni barani Afrika.
  • Ukame na mvua kubwa kuathiri maisha mashariki na kusini mwa Afrika. 2017-03-03

  Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) limesema karibu nchi 37 zinahitaji msaada wa chakula toka nje, zikiwemo nchi 28 za Afrika, kutokana na kuenea kwa athari za mvua za El-nino za mwaka jana ambazo zimesababisha ukame kwenye sekta ya kilimo .

  • Kenya, Uganda na Rwanda zapanga kuunganisha soko la utalii 2017-03-02

  Kenya, Uganda na Rwanda zimeanzisha mradi wa mtandao wa Internet unaolenga kuunganisha soko la utalii la nchi hizo ili kuvutia zaidi watalii kutoka nje.

  • Walinzi wa amani wa China wakamilisha majukumu yao nchini Liberia 2017-03-02
  Jumla ya askari 99 wa kulinda amani wa China wamekamilisha majukumu yao ya miezi mitano nchini Liberia na wamewasili Beijing jana usiku.
  • "Napenda kuiona China wala sio kuisikia tu" 2017-03-01
  Theopista Nsanzugwanko kutoka gazeti la Habarileo mjini Dar es Salaam, Tanzania atatumia muda wa miezi kumi ijayo hapa China kujionea sura halisi ya nchi hii ambayo labda inasikika kila siku, lakini ni vigumu kupata nafasi ya kuitembelea kutokana na sababu mbalimbali.
  • Kenya yamaliza sensa maalum ya wanyamapori 2017-02-28

  Shirika la Huduma kwa Wanyamapori nchini Kenya KWS limemaliza sensa maalum ya wanyamapori waishio katika mpaka wa Kenya na Tanzania.

  • Ukame watishia maisha ya watu milioni 1.5 Somalia 2017-02-28
  Shirika la Afya Duniani WHO limesema kwa sasa ukame nchini Somalia unatishia maisha ya watu milioni 1.5 na kati ya hao, ni nusu tu ndio wanaweza kupata huduma ya afya ya kimsingi. Watu wa Somalia wanaathiriwa na ukame mkali unaosababisha uhaba mkubwa wa chakula na kueneza maradhi kama vile kipindupindu na surua.
  • Wajerumani waliotekwa nyara nchini Nigeria waachiwa huru 2017-02-27
  Mtafiti wa mambo ya kale wa Ujerumani na mwenzake waliotekwa nyara Jumatano wiki iliyopita na watu wenye silaha wasiojulikana katika kijiji cha Jenjela, jimbo la Kaduna kaskazini mwa Nigeria, wameachiwa huru.
  • Rais wa Zimbabwe asema hatateua mwenyekiti ajaye wa Chama cha ZANU-PF 2017-02-26

  Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe aliyetimiza umri wa miaka 93 hivi karibuni ambaye pia ni katibu mkuu wa chama tawala cha ZANU-PF, amesema kwa sasa hatateua mwenyekiti ajaye wa chama hicho, na kwamba uteuzi huo utafanyika kwenye mkutano wa chama utakaofanyika mwaka 2019.

  • Jeshi la Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo lapambana na kuwaua wapiganaji wa kundi la M23 2017-02-24
  Waasi wa M23 huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wanaripotiwa kusambazwa na jeshi la serkali ya nchi hiyo kupitia mapambano makali yaliyoshuhudiwa wiki hii maeneo ya MATEMBE na KIRINGA wilayani RUTSHURU, mkoani KIVU YA KASKAZINI.
  • Umoja wa Afrika wasisitiza kupinga askari watoto barani Afrika 2017-02-24
  Kamati ya amani na usalama ya Umoja wa Afrika imefanya mkutano wa mawaziri kuhusu utumikishaji wa watoto jeshini.
  • Kampuni ya China yawafadhili wanafunzi wa Kenya kusoma nchini China 2017-02-23
  Serikali ya Kenya na Ubalozi wa China nchini Kenya wamefanya hafla ya kuwaaga wanafunzi 55 wa kikundi cha pili wanaokuja China kuendelea na masomo. Wanafunzi hao watasoma kozi ya reli kwa miaka minne katika chuo kikuu cha mawasiliano cha Beijing chini ya ufadhili wa kampuni ya reli ya China CRBC.
  • Somalia kuimarisha usalama kabla ya kuapishwa kwa rais mpya 2017-02-22
  Serikali ya Somalia imeimarisha usalama mjini Mogadishu na sehemu za karibu, kabla ya rais mpya wa nchi hiyo Mohamed Abdullahi Mohamed kuapishwa leo.
  • Umoja wa Mataifa wasema ukosefu wa chakula umewaathiri wakimbizi milioni 2 barani Afrika 2017-02-21
  Mashirika ya chakula na wakimbizi ya Umoja wa Mataifa yameeleza wasiwasi juu ya ukosefu mkubwa wa chakula unaowakabili wakimbizi wapatao milioni 2 katika nchi 10 barani Afrika.
  • Watu wasiopungua 30 wameuawa kwenye shambulizi la bomu lililotegwa kwenye gari nchini Somalia 2017-02-20
  Watu wasiopungua 30 wameuawa katika shambulizi la bomu lililotegwa kwenye gari lilitokea jana katika soko moja lenye watu wengi Mogadishu.
  • Mjumbe maalum wa rais Xi Jinping wa China ahudhuria sherehe ya kuapishwa kwa rais Adama Barrow wa Gambia 2017-02-19
  • Benki ya Maendeleo ya China yamesaidia maendeleo ya uchumi wa Cote d'Ivoire 2017-02-17

  Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya China Bw Zhang Zhijie amesema, biashara zinazofanywa na Benki hiyo nchini Cote d'Ivoire zitahimiza ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Cote d'Ivoire, na pia kusaidia maendeleo ya uchumi wa nchi hiyo.

  • Sudan Kusini na Uganda kupambana na mafua ya ndege 2017-02-16

  Sudan Kusini na Uganda zimekubaliana kuunda tume ya pamoja ya kusimamia mpaka, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kupambana na kuenea kwa homa ya mafua ya ndege iliyoripotiwa Kampala mwezi Januari.

  • Burundi yawataka wakimbizi wake kurudi nyumbani 2017-02-15

  Serikali ya Burundi imeanzisha kampeni ya kuwataka raia wake kurudi nyumbani licha ya hali ya kisiasa nchini humo kutotulia.

  • China na Msumbiji zaahidi kupanua ushirikiano 2017-02-15
  China na Msumbiji zimeahidi kupanua ushirikiano wa kunufaishana katika maeneo mbalimbali. Ahadi hiyo imetolewa wakati mwenyekiti wa Baraza la mashauriano ya kisiasa la China Bw. Yu Zhengsheng alipokutana na spika wa bunge la Msumbiji Bibi Veronica Macamo ambaye yuko kwenye ziara ya siku tano nchini China.
  prev 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 next
  SearchYYMMDD  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako