• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • • Wasichana wa Maolan wanaosuka mwanzi
    Hifadhi ya Msitu wa Kikarst iko katika tarafa ya Maolan, wilayani Libo, mkoani Guizhou, kusini magharibi mwa China. Mwaka 2007, hifadhi hiyo iliwekwa katika Orodha ya Urithi wa Dunia. Katika hifadhi hiyo, kuna shirika moja la utengenezaji wa sanaa ya mwanzi, ambapo wasichana wanaweza kutumia mwanzi wenye thamani ya yuan 10, na kuubadilisha kuwa kitu cha sanaa ambacho kinaweza kuuzwa kwa yuan elfu 4 hadi 5.
    • Kupeana upendo
    Siku chache zilizopita, kijana Jia Xiaodong kutoka mji wa Shenyang, mkoani Liaoning, kaskazini mashariki mwa China na Li Yao kutoka mji wa Benxi mkoani humo walifunga ndoa. Vijana hao wawili walikutana na kupendana kupitia mtoto mmoja kutoka Mianyang, Sichuan, mkoa uliopo mbali na Liaoning...
    • Msichana wa kazi nchini China
    Katika siku za hivi karibuni, familia nyingi za mjini hapa China zinapenda kupata wafanyakazi wa nyumbani ili kusaidia shughuli zao nyumbani, lakini kuna malalamiko kuwa si rahisi kupata msichana mzuri wa kazi na gharama za kuwaajiri zinapanda..
    • Makampuni kujitangaza katika vyuo vikuu
    Wanafunzi watakaohitimu katika vyuo vikuu mwakani nchini China wameanza kutafuta kazi, baadhi yao wanashiriki katika shughuli za kujitangaza kwa makampuni katika vyuo vikuu mbalimbali na kutuma maelezo yao binafsi kwenye mtandao wa internet, na wengine wameamua kupumbuzika kwa mwaka mmoja kabla ya kuanza kutafuta kazi.
    • Tarishi mwenye ulemavu anayefanya kazi katika sehemu za mlimani
    Katika sehemu za milimani za magharibi mwa mkoa wa Liaoning, kaskazini mashariki mwa China, kuna tarishi mmoja ambaye ni kiziwi na bubu. Kila siku anapanda pikipiki kupeleka barua, magazeti na mizigo kwa familia zipatazo elfu 5, na kwa wastani kila mwaka anasafiri kwa kilomita elfu 25 kupeleka maelfu ya barua, lakini hajawahi kufanya makosa yoyote, na anachukuliwa kuwa ni ndugu wa wanakijiji hao..
    • Daktari wa wafugaji wa kabila la Wakazakh Li Zhenxi
    Katika sehemu ya Mlima Tianshan wilayani Urumqi katika mkoa wa Xinjian, kaskazini magharibi mwa China, kuna daktari mmoja anayependwa sana na wafugaji wa kabila la Wakazakh. Daktari huyo ameishi sehemu ya ufugaji kwa zaidi ya miaka 30, na anawatibu na kuwapelekea dawa wafugaji hao, hivyo wanamchukulia kuwa ni ndugu yao. Daktari huyo Li Zhenxi, ni mkuu wa kituo cha afya cha Kata ya Tuoli, wilayani Urumqi.
    • Mahesabu ya gharama ya talaka nchini China yawazuia baadhi ya wanandoa kuachana
    Kuna wakati unaweza kuwa umefunga ndoa, umemchoka mwenzio na huwezi kumvumilia tena. Kwa mujibu wa sheria za China, ikiwa wanandoa wakikubaliana, tena hawana mtoto, wanaweza kuachana ndani ya siku moja tu. Wanaingia, wanatoka, wanalipa yuan 20 (sawa na tsh 5,000) tu, kasha wanaachana kabisa. Lakini hebu tujiulize je, ni wakati gani maisha yanakuwa rahisi namna hiyo?
    • Mwimbaji wa Afrika aliyetimiza ndoto yake ya muziki nchini China
    Siku hizi video moja inatazamwa sana kwenye mtandao wa internet nchini China. Kwenye video hiyo, kijana mmoja kutoka Afrika anaimba nyimbo za kichina kwa shauku kubwa. Wiki moja baada ya video hiyo kuwekwa kwenye mtandao wa Internet, tovuti nyingi kubwa za kichina pia ziliionesha, idadi ya watazamaji wa video hiyo imezidi milioni moja..
    • Kama una baa iitwayo "If"
    Kama una pesa na wakati wa kutosha, ungefanya nini? Kama unapenda pombe, na una kipaji cha kutengeneza cocktails, ungefungua baa? Yang Jun ni mtu aliyeamua kufanya hivyo. Yeye ni mmiliki wa baa ndogo iliyopo kwenye mtaa mwembamba uitwao Beiluoguxiang jijini Beijing. Yang amekuwa mmiliki wa baa kwa miaka 10, ndoto yake kubwa ni kubuni vinywaji vyake mwenyewe vitakavyobakia kichwani kwa kila mteja. Sasa hebu tuambatane naye ili tuangalie siku moja kwenye maisha yake ikoje?..
    • Siku ya kawaida ya mmiliki wa mgahawa
    Wang Jun mwenye umri wa miaka 32, anamiliki mgawaha mmoja uitwao Sky in Line uliopo Beijing, mji mkuu wa China. Ingawa ameishi Beijing kwa miaka mitano, lakini anajivunia sana kila wakati anapozungumzia maskani yake, mkoa wa Yunnan, kusini mwa China. Lakini maisha ya Wang Jun akiwa kazini kila siku yakoje? Tufuatane naye pamoja na mwandishi wetu wa habari kupata hisia ya siku nzima ya kazi za mmiliki wa mgahawa.
    prev 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 next
    SearchYYMMDD  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako