• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • • Mahusiano mema na mwajiri wa nyumbani kutasiaidia kupunguza matukio ya watoto kuteswa.

    Hivi karibuni matukio ya yaya kuwatesa watoto yalionyeshwa kwenye runinga za Afrika mashariki. Matukio hayo mbali na kuzua hisia tofauti miongoni mwa jamii yaliwafanya wazazi haswa kina mama kufikiria upya ni nani wa kuajiri kama yaya.

    • Nguvu mpya ya umoja wa mataifa huenda ikasaidia kumaliza upashaji tohara kwa wanawake.

    Takwimu za shirika la Umoja wa mataifa la kuwahudumia watoto la Unicef zinaonyesha kwamba zaidi ya wasichana milioni 30 wako katika hatari ya kukeketwa katika kipindi cha chini ya miaka kumi ijayo.

    • Kushirikisha jamii kwenye uhifadhi nchini Kenya kwatambuliwa kimataifa
    Kenya ni miongoni mwa nchi nane kote duniani ambazo zimetunikiwa tuzo la Green list ambalo linatolewa na shirikisho la kimataifa la kuhifadhi mazingira na mali asili IUCN. Kenya pia imekuwa ya kwanza barani Afrika kupata tuzo hilo lililotolewa Mjini Sydney Australia.
    • Ndoa iliyojaa mahaba kati ya mchina na mwafrika

    Ni safari ya maisha aliyokuwa akiyataka tokea utotoni. Akiwa amembega mwanae Emannuela wa miezi 10, Edwin Ata Rasiliamali kutoka Tanzania anaonekana mwenye furaha mpwito mpwito . Katika nyumba yake mjini Beijing, Edwin na mke wake mchina wanakumbuka jinsi walivokutana na kupendana mara ya kwanza wakiwa chuoni. Kwa Edwin, mapenzi hayachagui rangi wala dini.

    • Shule ya msingi ya bweni mlimani
    Tarafa ya Maryang iko kusini mashariki mwa wilaya ya Tashkurgan Tajik, mkoani Xinjiang, China, ambapo ni sehemu yenye mwinuko wa mita elfu 3.1 kutoka usawa wa bahari, na. Tarafa ya Maryang imezungukwa na milima, na mto Yarkant na tawi lake Maryang unapita ndani yake...
    • Maua yanachanua katika uwanda wa juu wa Qinghai-Tibet
    Uwanda wa juu wa Qinghai-Tibet una mwinuko mkubwa kutoka usawa wa bahari, ambapo nyuzi joto ziko tofauti sana kati ya usiku na mchana, nuru ya miali isiyoonekana Ultraviolet ni mikali, ambapo hali ya huko ni ya ukame na yenye uhaba wa mvua, hali hii ambayo haifai kwa kazi ya kilimo. Watu wanasema, watu wanaoishi kwenye uwanda wa juu wanapenda sana maua kutokana na uchache wake katika uwanda huo, hivyo unapotembea mitaani mbalimbali katika uwanda huo, utaona maua ya aina mbalimbali kwenye vyungu yakichanua vizuri katika roshani ya nyumba za wakazi wa huko..
    • Ren Qiang na gita yake
    Hiki ni kibwagizo cha gita cha sehemu ya mwanzo ya wimbo maarufu uitwao"California Hotel". Kwa vijana wengi, gita ni ala ya muziki ambayo ni rahisi kuiona na kuipata. Katika majira ya mchipuko, huwa tunawaona vijana wamekaa chini ya miti wakipiga gita huku wakiimba nyimbo mbalimbali.
    • Napenda maskani yangu
    Bw. Zhu Xianmin ni mkurugenzi wa Shirikisho la Wapiga picha wa China. Lakini baada ya kufanya kazi ya kupiga picha kwa karibu nusu karne hapa China, Zhu anasema kamwe moyo wake haujawahi kwenda mbali na maskani yake. Anatumia upigaji picha kuonyesha mandhari ya kupendeza na watu wazuri wa maskani yake. Anatarajia kuwa watu wanaoangalia picha alizopiga wanaweza kupata kumbukumbu kuhusu hali halisi ya China na sura halisi ya Wachina..
    • Sauti ya Radio yasikika daima
    Katiku siku za zamani, huenda redio ilikuwa ndio njia muhimu ya mawasiliano. Redio iligusia nyanja mbalimbali za maisha, kutoka usafiri wa baharini na angani, pamoja na kutoa habari, burudani na elimu. Mfumo huo wa mawasiliano kati ya mtu na mtu ulifungua dunia ya mawasiliano kati ya mtangazaji na msikilizaji.
    • Maisha mapya kwa watu waliohamishwa kutoka makazi yao
    Mwaka 2001, China ilizindua mradi wa kuwahamisha watu walioishi kwenye mazingira ya asili ya hali mbaya katika mikoa ya Sichuan, Yunnan, na mikoa mingine iliyo magharibi mwa China, ambapo watu hao wamehamia sehemu ambazo huduma za usafiri, maji na umeme zinapatikana kirahisi, ili kuwawezesha kuondokana na umasikini mapema na kujiendeleza.
    1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 next
    SearchYYMMDD  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako