![]() Mkoa wa Tibet uko katika uwanda wa juu wa Qinghai-Tibet. Mkoani humo si kama tu kuna mandhari nzuri ya asili, bali pia kuna mabaki mengi ya utamaduni. Tangu mageuzi ya demokrasia yafanyike mwaka 1959 mkoani Tibet, serikali kuu ya China na serikali ya mkoa wa Tibet zimefanya juhudi kubwa za kuhifadhi mabaki ya kale ya utamaduni mkoani humo. |
![]() Maonesho ya kimataifa ya mwaka 2010 yatakayofanyika huko Shanghai, mji uliopo mashariki ya China yatafanyika kwa siku 184 kuanzia tarehe 1 Mei hadi tarehe 31 Oktoba,. inakadiriwa kuwa maonesho hayo yatavutia watembezi wapatao milioni 70 kote duniani, na kauli mbiu ya maonesho hayo ni "Miji bora zaidi, maisha bora zaidi". Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa China kuandaa maonesho ya kimataifa, na kauli mbiu hiyo ina umuhimu mkubwa katika hali halisi kwa hivi sasa. ![]() |
![]() Kuanzia kipindi cha majira ya joto mwaka jana, sehemu tano za kusini magharibi mwa China zilikumbwa na maafa ya ukame ambayo hayakutokea hapo awali. Wilaya inayojiendesha ya makabila ya Wamiao na Wabuyi ya Qianxinan mkoani Guizhou ilikumbwa na ukame zaidi, kuanzia mwezi Agosti mwaka 2009 mvua haikunyesha kabisa. ![]() |
![]() Bibi Susan Osman alikuwa mtangazaji mwanamke maarufu wa Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC, hivi sasa anafanya kazi katika Radio China Kimataifa, na kuwa mtangazaji wa kipindi kipya cha habari Beijing Hour. |
![]() Mwaka jana wanafunzi wapatao laki 2.3 wa China walikwenda nje kuendelea na masomo yao, idadi ambayo imeongezeka kwa asilimia 30, na kati ya wanafunzi hao wahitimu wa shule za sekondari walichukua asilimia kubwa. |
![]() Kutokana na misaada ya "mikopo midogo" na "kituo cha kusaidia biashara" inayotolewa na Shirikisho la wanawake la Tianjin, wanawake wengi mjini Tianjin wamepata ajira na hata wameanzisha shughuli zao kwa mafanikio. |
![]() Kama tujuavyo, maonesho hayo yatakayofunguliwa tarehe 1 Mei yanatazamiwa kuwavutia watalii milioni 70 kutoka nchi mbalimbali duniani. Je, watalii wakikumbwa na ajali au kusumbuliwa na tatizo la kiafya wakati wanapotembelea maonesho ya kimataifa, watasaidiwa vipi? Katika kipindi cha leo, tutawaelezea jinsi huduma za afya zitakazotolewa na upande wa tatu wakati wa maonesho hayo zitakavyowasaidia watalii. |
Wajumbe wa baraza la mashauriano ya kisiasa watoa mapendekezo kuhusu maendeleo ya uchumi katika sehemu za makabila madogo madogo yenye watu wachache Mkutano wa baraza la mashauriano ya kisiasa umefungwa hivi karibuni nchini China. Kwenye mkutano huo wajumbe kutoka sehemu za makabila madogo madogo yenye watu wachache walitoa mapendekezo mbalimbali kuhusu maendeleo ya uchumi katika sehemu hizo. Nchini China kati ya makabila 55 madogo madogo, kuna makabila 22 yenye watu wasiofikia laki moja, na makabila hayo yanajulikana kuwa makabila madogo madogo yenye watu wachache. ![]() |
![]() Mikopo midogo inatatua suala la fedha kwa wanawake wanaoanzisha shughuli zao, lakini mwanzoni wakati wanaanzisha shughuli zao, huwa wanakabiliwa na changamoto nyingine mbalimbali. Ili kuwasaidia wanawake hao kukabiliana na changamoto hizo, "kituo cha kusaidia biashara" kilianzishwa, ambacho lengo lake ni kuyasaidia makampuni ambayo yako katika hatua ya mwanzo, ili ndoto ya wanawake kuhusu kuanzisha shughuli zao itimizwe. ![]() |
![]() Katika mkoa unaojiendesha wa Xinjiang Uyghur ulioko kaskazini magharibi mwa China, kuna wakazi wa makabila 13 yakiwemo makabila ya Wauyghur, Wakazakh, Wamongolia, Wahui, Wahan na Waman. Tokea zamani, watu wa makabila hayo tofauti wameishi pamoja kwa urafiki na mshikamano... ![]() |
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |