• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • • Mikopo midogo yawasaidia wanawake kuanzisha shughuli zao
    Duka la bibi He Jianchun liko karibu na kituo cha mabasi kilichopo katika sehemu ya Hedong mjini Tianjin. Duka hilo lenye mita 6 za mraba linauza sigara, pombe na vitu mbalimbali. Bibi He Jianchun anaanza kufanya kazi mapema asubuhi, anauza kifungua kinywa, kadi za kuongeza pesa kwenye simu za mkononi na vitu vingine.
    • Kujenga matumaini mapya ya maisha
    Mwaka mmoja na nusu umepita tangu tetemeko kubwa la ardhi lilipotokea tarehe 12 Mei mkoani Sichuan. Hivi sasa ujenzi wa baadhi ya miradi ya ukarabati wa sehemu zilizokumbwa na tetemeko la ardhi umekamilika, na ujenzi wa miradi mingine unaendelea bila matatizo. Katika sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China, ambayo ni sikukuu kubwa zaidi ya Wachina, watu wa sehemu hizo walisherehekea sikukuu hiyo kwa furaha.
    • Waluoluo wa kabila la Wayi wakaribisha mwaka wa chui
    Wachina wanaona kuwa chui ni alama ya ushujaa na haki, na anaweza kuleta bahati nzuri, hata watu wa baadhi ya makabila madogo madogo nchini China wanaabudu chui.
    • Bw. John Rabe, mtu aliyeshuhudia historia ya China
    Mjerumani Bw. John Rabe aliheshimiwa na Wachina, na alichaguliwa kuwa ni mmoja kati ya "marafiki kumi wakubwa wa kigeni" kwa kura zaidi ya milioni 4.
    • Maonesho ya ngoma ya Liyoresisi ya kabila la Wabuyi
    Kabila la Wabuyi lina watu zaidi ya milioni 2.5, na wengi wao wanaishi katika mkoa wa Guizhou ulioko kusini magharibi mwa China. Wabuyi ni hodari katika kuimba nyimbo na kucheza ngoma, na wanaweza kuonesha historia, utamaduni, mila na desturi zao kwa kupitia maonesho mbalimbali ya nyimbo na ngoma.
    • Moyo wa uzalendo wa watu wa Macau kwa taifa la China
    Watu wakizungumzia kazi za usanii za China kuhusu Macau, inayojulikana zaidi ni Wimbo wa Macau uliotungwa na Wen Yiduo, mshairi mzalendo wa China. Kupitia wimbo huo, watu wengi kwa mara ya kwanza walisikia jina la "Macau" kwa Kireno, pia kwa kupitia wimbo huo, watu wengi wamefahamu zaidi uhusiano kati ya Macau na China na hisia kubwa walizonazo watu wa Macau kwa taifa la China.
    • Shule ya msingi ya kabila la Wajinuo iliyoko chini ya mlima Jinuo
    Kabila la Wajinuo ni kabila dogo lenye historia ndefu, na ni kabila la mwisho kuwekwa katika orodha ya makabila madogo madogo nchini China. Watu wengi wa kabila hilo wanaishi katika sehemu ya Mlima Jinuo iliyoko katika wilaya ya Xishuangbanna mkoani Yunnan. Kila asubuhi, watoto wa vijiji mbalimbali vya kabila la Wajinuo wanakwenda kusoma kwenye shule yao ya msingi iliyoko chini ya Mlima Jinuo. Katika shule hiyo maalumu iliyoanzishwa kwa ajili ya wanafunzi wa kabila la Wajinuo, wanafunzi wanasoma kwa furaha.
    • Bw. Israel Epstein, mwandishi wa habari maarufu aliyejionea maendeleo ya China
    Bw. Epstein alizaliwa mwaka 1915 katika familia ya Wayahudi iliyofuata Umarx huko Warsaw, Poland. Wazazi wake waliwahi kukamatwa na kufukuzwa kutokana na kushiriki kwenye mapinduzi. Alipokuwa na umri wa miaka miwili, aliambatana na wazazi wake kuja China kupitia Japan.
    • Mchezo wa sarakasi ya Dawaz wa kabila la Wauyghur
    Dawaz ni usanii wa jadi wa mchezo wa sarakasi wa kabila la Wauyghur. Maana ya "Dawaz" katika lugha ya Kiuyghur ni "kutembea kwenye kamba iliyofungwa juu". Mchezo wa Dawaz una historia zaidi ya miaka 2,000, na unapendwa sana na watu wa makabila mbalimbali wanaoishi katika mkoa unaojiendesha wa Xinjiang Wauyghur.
    • Mwandishi wa habari wa Ujerumani ashuhudia mabadiliko ya China katika miaka 30 iliyopita
    Bw. Martin Kummer alipokuwa na umri wa miaka 27 mwaka 1976  alikuja nchini China akiwa mwandishi wa habari wa gazeti la Hamburg la Ujerumani, ambapo alitumia macho yake kuiona China yenye historia ndefu; mwaka 2006 yeye na mkewe waliitembelea tena China, na kutumia kamera kurekodi mabadiliko ya China na watu wa China katika miaka 30 iliyopita.
    prev 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 next
    SearchYYMMDD  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako