![]() Bondia Arnel Tinampay wa Philippines amemtaka Hassan Mwakinyo, bondia wa Tanzania, kujiandaa kwa kipigo kwa kuwa anafahamu ubora na udhaifu wake. |
![]() Kocha wa zamani wa Arsenal, Mfaransa Arsene Wenger, ameramba dili nono kwa kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa maendeleo ya Soka Duniani. |
![]() Real Madrid wanaangalia uwezekano wa kutoa malipo makubwa kuwahi kushuhudiwa ya pauni milioni 340 kwa ajili ya mchezahi wa safu ya ushambulizi wa Paris St Germain mwenye umri wa miaka 20 Kylian Mbappe. |
![]() Nyanja ya mieleka imepata pigo kubwa kufuatia kifo cha ghafla cha mwanamieleka chipukizi Matt Travis. |
![]() Wakati timu ya Simba ikiongoza katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, kocha mkuu wa timu hiyo Patrick Aussems amesema anafurahia kuona ushindani uliopo katika ligi hiyo msimu huu umeongezeka, hivyo kuongeza umakini wa timu yake. |
![]() Cristiano Ronaldo ameripotiwa kuondoka kwenye Uwanja wa Allianz kabla ya kipenga cha mwisho kwenye mechi ambayo Juventus ilijipatia ushindi mwembaba wa 1-0 dhidi AC Milan ya Serie A iliyochezwa Jumapili, baada ya kubadilishwa katika mechi ya pili kwa wiki. |
![]() Kipa raia wa Tanzania, David Kisu Mapigano, ameonyesha kiwango kizuri na kuisaidia Gor Mahia kuwafunga watani zao wa jadi AFC Leopards mabao 4-1 katika mchezo wa Ligi Kuu Kenya iliyochezwa jana Jumapili Novemba 10 kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Moi Kasarani jijini Nairobi. |
![]() Kufanya vizuri kwa nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta katika mechi ya Ligi ya Mabingwa kati ya timu yake Genk dhidi ya Liverpool, kumezidi kumsafishia njia mshambuliaji huyo. |
![]() Afisa wa polisi ameshtakiwa wa mauaji ya mchezaji soka wa zamani Dalian Atkinson ambaye alikufa baada ya kupigwa na nguvu ya umeme. Mshambuliaji huyo wa zamani wa Aston Villa mwenye umri wa miaka 48, alikamatwa katika nyumba ya baba yake katika eneo la Telford, Shropshire, tarehe 15 Agosti 2016. |
![]() Timu ya mpira wa magongo ya wanawake nchini Kenya Lakers inatafuta ushindi baada ya kufungwa mechi mbili zilizopita dhidi ya USIU na Sliders mwezi uliopia, ushindi uliofuta rekodi ya Lakers ya kutofungwa katika Mashindano ya Ligi ya Mpira wa Magongo kwa Wanawake nchini humo. |
![]() Mashabiki watakaofika uwanjani Kasarani kushabikia vipusa wa Harambee Starlets, katika mchuano wa kufuzu kwa Michezo ya Olimpiki Tokyo, hawatatozwa kiingilio. |
![]() Baada ya mchezo wake wa kwanza dhidi ya Liverpool na KRC Genk kuchezwa katika uwanja wa Luminus nchini Ubelgiji, huku mtanzania Mbwana Samatta akifunga goli na kukataliwa dhidi ya Liverpool, usiku wa November 5, 2019 kiu ya Tanzania ilikatwa rasmi na Mbwana Samatta ya kuona anafunga goli dhidi ya Liverpool, ili aweke rekodi ya kuwa Mtanzania pekee wa kwanza kuwahi kuwafunga Liverpool. |
![]() Mwanariadha Joyciline Jepkosgei amefichua azma ya kuvunja rekodi ya dunia katika mbio za kilomita 42 baada ya kuibuka mshindi wa New York Marathon, Amerika mnamo Jumapili. |
![]() Bondia Anthony Joshua anatarajiwa kuongeza mamilioni ya fedha baada ya pambano lake dhidi ya Andy Ruiz Jr litakalofanyika Desemba 7, mwaka huu nchini Saudi Arabia. |
![]() Lewis Hamilton ametia kibindoni taji lake la sita la udereva duniani akimaliza nafasi ya pili kwenye mbio za United States Grand Prix. Matokeo hayo yanamaanisha Hamilton anakuwa dereva wa pili wa Formula 1 mwenye mafanikio zaidi katika muda wote akimsogelea kwa karibu mno bingwa wa muda wote anayeshika rikodi Michael Schumacher, ambaye amekwaa mataji saba. |
![]() Upepo mbaya ambao ulianza kuvuma ndani ya Shirikisho la Soka Zanzibar (ZFF) na Shrikisho la Soka Tanzania (TFF) hivi sasa umeonekana kuanza kutulia. |
![]() Bingwa wa zamani wa uzito wa juu Tyson Fury sasa amekuwa Superstar asiyeshindikana wa WWE, baada ya pambano lake jana. Mazoezi yake ya wiki nne ya kujenga misuli na kujiandaa na pambano lake dhidi ya jitu la miraba saba Braun Strowman almaarufu kama 'Monster Among Men' yamelipa baada ya kumpatia kichapo cha mbwa kwenye pambano la Crown Jewel lililofanyika jana huko Riyadh, Saudi Arabia. |
![]() Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar imeandaa mashindano maalum la michezo wa soka la kuvuta kamba yatakayoanza Novemba 2. |
![]() Mwanasoka mashuhuri wa Cameroon Samuel Eto'o amesema yeye ni mwanasoka bora wa muda wote wa Afrika na sasa analenga kupata mafanikio zaidi kama kocha. |
![]() Wakati mashabiki wa soka wa klabu ya Simba wakiwa na kiu ya kuona Meddie Kagere anaendeleza kasi yake ya kucheka na nyavu katika mechi ya leo dhidi ya Mwadui FC, mshambuliaji huyo aliyefunga mabao katika mechi tano mfululizo amesema, anachotazama kwanza ni ushindi wa timu na si yeye kufunga. |
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |