• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • • Kocha Antonio Conte akiri michezo miwili ya siku za hivi karibuni ni migumu kwa upande wao 2017-04-27
  Meneja wa klabu ya Chelsea, Antonio Conte, amekiri michezo miwili waliyocheza siku za hivi karibuni imekua michezo migumu kwa upande wao na imekua muhimu kuhakikisha wanapata alama tatu zitakazowasaidia kujikuta kileleni mwa ligi hiyo ya EPL.
  • Lionel Messi ajitapa kwa mechi yao dhidi ya Real Madrid 2017-04-25

  Juzi usiku FC Barcelona walikuwa katika uwanja wa wapinzani wao Real Madrid kucheza mchezo wao wa marudiano wa Ligi Kuu Hispania, katika mchezo huo FC Barcelona walifanikiwa kupata ushindi wa magoli 3-2 dhidi ya Real Madrid.

  • N'golo Kante ashinda tuzo ya PFA 2017-04-24
  Nyota wa kimataifa wa Ufaransa anayeichezea Chelsea ya England N'golo Kante amefanikiwa kushinda tuzo ya PFA ya mchezaji bora wa mwaka wa England kwa kuwashinda Eden Hazard, Harry Kane, Romelu Lukaku, Zlatan Ibrahimovic na Alexis Sanchez kwa kupata kura nyingi.
  • Man United yaibuka kidedea dhidi ya Anderletch Europa League 2017-04-21

  Man United ni miongoni mwa timu zilizocheza mchezo wake wa marudiano wa robo fainali ya Europa League dhidi ya Anderletch jana usiku katika uwanja wake wa Old Trafford. Man United walicheza mechi hiyo na kukutana na upinzani mkubwa uliopelekea kuongezwa dakika 120.

  • Mbwana Samatta anyemelewa na Fenerbahce ya Uturuki 2017-04-20

  Habari za usajili barani Ulaya zimeanza kuchukua nafasi wakati huu ambao Ligi Kuu mbalimbali barani humo zinakaribia kumalizika, mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Samatta ameanza kuhusishwa na Fenerbahce ya Uturuki.

  • UEFA Champions ligi: Ronaldo apiga Hat Trick na kuipeleka Madrid nusu fainali. 2017-04-19

  Hat Trick za Christiaono Ronaldo zimeiwezesha Real Madrid kutinga nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya kwa kuifunga Bayern Munich mabao 4-2. Madrid inakwenda nusu fainali kwa jumla ya mabao 6-3 baada ya ushindi wa mabao 2-1 mjini Munich.

  • Wakenya watawala mbio za Boston Marathon 2017-04-18
  Wanariadha wa Kenya wameendelea kupeperusha vyema bendera ya nchi yao na Afrika Mashariki kwa kushinda mashindano ya mbio ya Boston.
  • AC Milan yanunuliwa na kampuni ya China 2017-04-14

  Timu ya soka ya AC Milan ya Italia imeuziwa kampuni ya China na kufikia kikomo umiliki wake na aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo na tajiri Silvio Berlusconi.

  • Stephen Curry aongoza kwa mauzo ya jezi mpira wa kikapu Marekani 2017-04-13

  Mchezaji wa klabu ya Golden State Warriors, Stephen Curry kwa mara nyingine amefanikiwa kuongoza kwa mauzo ya jezi kwa wachezaji wote wanaoshiriki ligi kuu ya mpira wa kikapu nchini Marekani - NBA. Hii ni mara ya pili mfululizo kwa mchezaji huyo.

  • Borussia Dortmund yashambuliwa ikielekea kucheza na Monaco 2017-04-12
  Milipuko mitatu imelikumba basi la timu ya Borussia Dortmund lililokuwa likielekea kwenye mchezo wake wa kwanza wa robo fainali ya ligi ya mabingwa wa Ulaya dhidi ya Monaco.
  • Hamilton aibuka na ubingwa wa Chinese Grand Prix 2017-04-11
  Dereva wa Mercedes Lewis Hamilton ambaye ametawala katika mashindano ya Chinese Grand Prix amefanikiwa kuchukua taji lake la kwanza kwa mwaka huu, baada ya kumshinda Dereva wa Ferrari Sebastian Vettel.
  • UEFA yamtabiria makubwa Mbwana Samatta. 2017-04-10

  Shirikisho la soka Ulaya (UEFA) limemtaja mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta kama mmoja wa wachezaji wa kutazamwa kwa sasa barani humo.

  • Peter Odemwingie ajiunga na klabu ya Madura United ya Indonesia 2017-04-06

  Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Nigeria Peter Odemwingie amejiunga na klabu ya Madura United ya Indonesia. Mchezaji huyo ambaye hivi sasa ana umri wa miaka 35 na ameichezea timu ya taifa ya Nigeria Super Eagles katika mashindano ya kombe la dunia mwaka 2010 na 2014 ametia saini mkataba wa mwaka mmoja ambao unaweza kuongezwa.

  • Tetesi za Zlatan Ibrahimovic kuhamia LA Galaxy zazidi kuwa kubwa 2017-04-05
  Nyota wa kimataifa wa Sweden ambaye anaichezea Man United ya England Zlatan Ibrahimovic kwa wiki kadhaa sasa amekuwa akihusishwa kuwa na mpango wa kujiunga na LA Galaxy ya Ligi Kuu Marekani, Zlatan hadi sasa ameichezea Man United michezo 41 na kuifungia magoli 26 akitoa usaidizi mara 9 katika mashindano yote.
  • Bastian Schweinsteiger atambulishwa rasmi na klabu yake mpya Chicago Fire 2017-03-31
  Mchezaji Bastian Schweinsteiger ametambulishwa rasmi na klabu yake mpya ya Chicago Fire ya Marekani.
  • Uwanja wa ndege wa Madeira wapewa jina la Cristiano Ronaldo 2017-03-30
  Moja kati ya vitu ambavyo vinaingia katika historia ya maisha ya nyota wa soka wa kimataifa wa Ureno anayeichezea Real Madrid Cristiano Ronaldo ni uwanja wa ndege wa kimataifa wa Madeira kubadilishwa jina na kupewa jina lake.
  • FIFA yamfungia Messi mechi 4 kwa utovu wa nidhamu. 2017-03-29

  Shirikisho la soka ulimwenguni FIFA jana limetangaza kumfungia mechi nne kapteni wa Argentina Lionel Messi kufuatia kosa alilolitenda Machi 24 wakati wa mchezo dhidi ya Chile, Messi amefungiwa kutokana na utovu wa nidhamu wa kumtolea lugha isiyo ya kiungwana refa wa mchezo huo.

  • Kuelekea Kombe la Dunia 2018 Russia: Ubelgiji yaponyeka, wadachi hoi, Ronaldo aibeba Ureno 2017-03-27
  • England yakubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Ujerumani 2017-03-24
  Timu ya taifa ya England imekubali kichapo cha bao 1-0 ugenini dhidi ya timu ya taifa ya Ujerumani katika mchezo wa kirafiki.
  • Usain Bolt awaalika David Rudisha na Mo Farah kushiriki shindano lake la mwisho 2017-03-23
  Mwanariadha mwenye kasi zaidi duniani Usain Bolt amemwalika mfalme wa mbio za mita 800 duniani David Rudisha na yule wa mita 5,000 na 10,000 Mo Farah, kushiriki kwenye shindano lake la mwisho la kumuaga anapojiandaa kustaafu riadha mwaka huu.
  prev 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 next
  SearchYYMMDD  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako