• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • • Ligi kuu Tanzania Bara (TPL) Simba yabadilisha matokeo dakika za majeruhi 2019-05-01
  • SOKA: Dijk, mchezaji bora wa mwaka wa PFA, Vivianne ashinda kwa wanawake. 2019-04-30

  Beki wa Livepool Virgil Van Dijk ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa chama cha wachezaji wa kulipwa Uingereza (PFA).

  • SOKA: AFCON U-17- Cameroon mabingwa wapya wa AFCON 2019 2019-04-29
  • SOKA: Mchezaji wa Burundi, Papy Faty afariki dunia Eswatini 2019-04-26
  Kiungo wa kimataifa wa Burundi, Papy Faty amefariki ikiwa ni miezi mitatu kabla nchi yake ya Burundi kushiriki fainali zake za kwanza za kombe la mataifa ya Afrika (AFCON 2019).
  • SOKA: Ligi Kuu Uingereza (EPL)- Vita dhidi ya Ubingwa yapamba moto, Man City yakamata uongozi wa ligi, Arsenal yapigwa 2019-04-25
  Kupitia migoli mitamu iliyofungwa na Bernardo Silva dakika ya 54 na la Leroy Sane dakika ya 66 imeiwezesha Manchester City jana kukwaa uongozi wa ligi kuu ya Uingereza na kufanya vita ya ubingwa wa ligi hiyo kuendelea kuwa ngumu.
  • Mashindano ya Pikipiki: Uganda yaitambia Kenya kibabe, yabeba  ubingwa 2019-04-24
  Mashindano ya ubingwa wa kuendesha pikipiki Afrika Mashariki na kati yamefanyika katika uwanja wa Busiika nchini Uganda, na kushuhudiwa Mganda Maxime Pevan akiibuka bingwa baada ya kukusanya alama 1,395 huku mkenya akiambulia alama 252 tu.
  • NDONDI: Pambano la Miller na Joshua, hati hati 2019-04-23
  Pambano la ngumi kati ya mabondia Jarrell Miller na Anthony Joshua limeingia katika utata wa kufanyika, mashabiki wao wanaendelea kutupiana vijembe.
  • SOKA: Ligi Kuu ya Uingereza (EPL): Mashetani wekundu waangukia pua 2019-04-22
  Ligi kuu ya Uingereza imeendelea jana kwa michezo mitatu kupigwa katika viwanja tofauti nchini Uingereza. Everton imedhihirisha kuwa soka si majina makubwa tu bali namna ya kutandaza kabumbu uwanjani, na kuifunga Manchester United mabao 4-0.
  • RIADHA: Mtanzania mwanafunzi ashinda mbio kwa miaka miwili mfululizo nchini China 2019-04-19

  Mtanzania Dennis Chinamo, anayesoma kozi ya uhandisi wa petroli katika chuo kikuu cha Southwest Petroleum katika Jimbo la Sichuan, mjini Chengdu China, amefanikiwa kuibuka mshindi kwenye mashindano ya mbio fupi yaliyofanyika chuoni hapo.

  • GOFU: Wood ashinda taji la 15 baada ya miaka 11 2019-04-18

  Mkongwe wa mchezo wa gofu duniani Tiger Woods, ameshinda taji la 15 kwenye michuano mikubwa baada ya juzi kutwaa ubingwa wa michuano ya Masters iliyokuwa ikifanyika katika Mji wa Augusta Marekani.

  • SOKA: Eto'o apewa ubalozi wa Kombe la Dunia 2022 Qatar 2019-04-17

  Mshambuliaji wa zamani wa Cameroon, Samuel Eto'o amepata heshima zaidi baada ya kutambulishwa kuwa Balozi wa fainali za kombe la dunia zitakazofanyika mwaka 2022 nchini Qatar.

  • RIADHA: Mbio za Boston- Kenya ileeee, inaendelea kuwa juu 2019-04-16

  Mwanariadha wa Kenya Lawrence Cherono ametwaa taji la mbio za Boston zilizofanyika nchini Marekani, Cherono amempiku Lelisa Desina wa Ethiopia akitumia saa 2:07:57, nafasi ya tatu, nne na tano zimetwaliwa na Wakenya wengine.

  • RAGA: Michuano ya Raga ya wachezaji 7 kila Upande jijini London, Shujaa uso kwa uso na Fiji na Samoa 2019-04-16
  • RAGA: Shujaa itang'aa michuano ya Singapore, kocha awatoa matumaini 2019-04-12
  Kocha wa timu ya taifa ya Raga ya Kenya ya wachezaji 7 kila upande (Shujaa) Paul Murunga amesema ana matumaini na kikosi cha timu hiyo na kwamba kikosi chake kitafanya vizuri katika michuano ijayo ya raga ya dunia itakayofanyika jijini Singapore, Malaysia mwishoni mwa wiki hii.
  • MIELEKA: Batista astaafu mieleka rasmi, apoteza pambano lake la mwisho 2019-04-11
  Juzi ilikuwa mwisho kwa mashabiki wa Dave Batista na mchezo wa mieleka kwa ujumla kumshuhudia tena uliongoni mkongwe huyo akipambana baada ya kutangaza rasmi kustaafu kushiriki mchezo huo wa mieleka.
  • SOKA: Ligi ya Mabingwa Ulaya- Liverpool yaichezesha mchakamchaka Porto, Spurs yaipiga Man City 2019-04-10
  Ligi ya mabingwa barani Ulaya hatua ya robo fainali imerejea jana kwa michezo miwili kupigwa, Liverpool ya Uingereza imekutana na FC Porto na kuendeleza ubabe uliofanya msimu uliopita kwa kuibamiza Porto goli 2-0.
  • Raga: Serikali ya Kenya yaahidi kuwasaidia Chipu wa Kenya baada ya kuibuka mabingwa wa Afrika U-20 2019-04-09
  Serikali ya Kenya imeahidi kusaidia timu ya Chipu ya Kenya kushiriki raga ya dunia ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 20 ya daraja ya pili baada ya kuichabanga Namibia kwa alama 21-18 katika fainali ya mchezo huo wa bingwa wa Afrika jijini Nairobi.
  • SOKA: Klabu bingwa Afrika-Simba, Mazembe shoo ya kibabe, Mamelodi yatoa dozi nzito kwa Al Ahly 2019-04-08
  • SOKA: Derby ya Der Klassiker kupigwa Jumamosi hii dimba la Allianz Arena. 2019-04-05

  Katika ulimwengu wa soka kuna mechi chache sana zinazoweza kuamsha hisia kama derby ya Der Klassiker ambayo itapigwa Jumamosi hii katika dimba la Allianz Arena nyumbani kwa Bayern Munich. Ni bonge moja la mechi ambayo ni zaidi ya derby ya kawaida kwa sababu timu zote mbili zinawania ubingwa wa Bundesliga.

  • SOKA: Aussems na Bocco watwaa tuzo ya mwezi Machi 2019-04-04

  Kocha wa timu Simba ya Dar es Salaam Patrick Aussems sambamba na mshambuliaji ambaye pia ni nahodha wa timu hiyo John Bocco wametwaa tuzo ya mwezi Machi inayotolewa na shirikisho la soka Tanzania (TFF).

  prev 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 next
  SearchYYMMDD  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako