• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • • Bastian Schweinsteiger atambulishwa rasmi na klabu yake mpya Chicago Fire 2017-03-31
  Mchezaji Bastian Schweinsteiger ametambulishwa rasmi na klabu yake mpya ya Chicago Fire ya Marekani.
  • Uwanja wa ndege wa Madeira wapewa jina la Cristiano Ronaldo 2017-03-30
  Moja kati ya vitu ambavyo vinaingia katika historia ya maisha ya nyota wa soka wa kimataifa wa Ureno anayeichezea Real Madrid Cristiano Ronaldo ni uwanja wa ndege wa kimataifa wa Madeira kubadilishwa jina na kupewa jina lake.
  • FIFA yamfungia Messi mechi 4 kwa utovu wa nidhamu. 2017-03-29

  Shirikisho la soka ulimwenguni FIFA jana limetangaza kumfungia mechi nne kapteni wa Argentina Lionel Messi kufuatia kosa alilolitenda Machi 24 wakati wa mchezo dhidi ya Chile, Messi amefungiwa kutokana na utovu wa nidhamu wa kumtolea lugha isiyo ya kiungwana refa wa mchezo huo.

  • Kuelekea Kombe la Dunia 2018 Russia: Ubelgiji yaponyeka, wadachi hoi, Ronaldo aibeba Ureno 2017-03-27
  • England yakubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Ujerumani 2017-03-24
  Timu ya taifa ya England imekubali kichapo cha bao 1-0 ugenini dhidi ya timu ya taifa ya Ujerumani katika mchezo wa kirafiki.
  • Usain Bolt awaalika David Rudisha na Mo Farah kushiriki shindano lake la mwisho 2017-03-23
  Mwanariadha mwenye kasi zaidi duniani Usain Bolt amemwalika mfalme wa mbio za mita 800 duniani David Rudisha na yule wa mita 5,000 na 10,000 Mo Farah, kushiriki kwenye shindano lake la mwisho la kumuaga anapojiandaa kustaafu riadha mwaka huu.
  • Ronaldo mwanasoka bora wa mwaka Ureno 2017-03-22
  Cristiano Ronaldo anayechezea Real Madrid ya Hispania jana ametangazwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa Urenoi akiwashinda beki wa Read Madrid Pepe na kipa wa Sporting Lisbon, Rui Patricio.
  • FIFA yamfungia refa kutojihusisha na soka maisha 2017-03-21
  Shirikisho la soka ulimwenguni FIFA jana limetangaza maamuzi kwa refa Joseph Lamptey aliyechezesha mchezo wa kuwania kufuzu kucheza Kombe la Dunia 2018 Urusi kati ya Afrika Kusini dhidi ya Senegal.
  • Ndondi: Golovkin amchakaza Jacob 2017-03-20
  Gennady Golovkin ameonyesha anaweza baada ya kumtwanga mpinzani wake Daniel Jacobs na kuendelea kutetea ubingwa wake.
  • Shirikisho la Soka Barani Afrika CAF lapata rais mpya 2017-03-17
  Mkutano wa 39 wa shirikisho la soka barani Afrika CAF ulifanyika jana Addis-Ababa Ethiopia. Katika mkutano huo uliojadili mambo kadhaa, pia ulifanyika uchaguzi wa Rais wa shirikisho hilo. Wagombea wa nafasi za Urais walikuwa ni Rais wa sasa wa shikisho hilo Issa Hayatou na Ahmad Ahmad wa Madagascar, katika uchaguzi huo Ahmad Ahmad amemshinda Issa Hayatou kwa kura 34 wakati Hayatou akiambulia kura 20.
  • Ander Herrera athibitika kufungiwa michezo miwili na chama cha soka cha England FA 2017-03-16
  Kiungo wa kimataifa wa Hispania anayeichezea Man United ya England Ander Herrera amethibitika kufungiwa michezo miwili na chama cha soka cha England FA.
  • Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA): Leicester City yatinga robo fainali 2017-03-15
  Leicester City imeweka rekodi baada ya kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, (UEFA) kwa mara ya kwanza.
  • Kombe la FA: Manchester United yaaga FA Cup Stamford Bridge 2017-03-14
  Vinara wa ligi ya EPL, Chelsea jana wameifunga Manchester United kwa goli 1-0 katika nusu fainali iliyochezwa kwenye uwanja wa Stamford Bridge.
  • La Liga: Ronaldo, Ramos waipaisha Madrid kileleni na mechi 1 mkononi 2017-03-13
  Real Madrid usiku wa leo wametoka nyuma kwa Bao 1-0 na kuiwasha Real Betis 2-1 Uwanjani Santiago Bernabeu Jijini Madrid nchini Hispania na kutwaa uongozi wa La Liga kutoka kwa Mahasimu wao Barcelona.
  • Mbwana Samatta wa KRC Genk aondoa ukame wa magoli 2017-03-10
  Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Mbwana Samatta akiwa na timu yake ya KRC Genk walikuwa ugenini kucheza mchezo wao wa kwanza hatua ya 16 bora wa UEFA Europa League dhidi ya KAA Gent, kutoka Ubelgiji.
  • Barcelona wafanya maajabu dhidi ya Paris Saint Germain Klabu Bingwa Ulaya 2017-03-09
  Barcelona wamebirua matokeo ya kutinga nusu fainali kwa kuichakaza Paris Saint Germain mabao 6-1 katika mchezo wa marudiano wa Klabu Bingwa Ulaya. Sergi Roberto alifunga bao la 6 kwa mkwaju wa mwisho wa mchezo, na hivyo kufanya matokeo ya jumla kuwa 6-5 kwenye mchezo uliocharazwa kwenye dimba la Nou Camp.
  • UEFA Champions Ligi: Leo Arsenal itaweza kusonga mbele? 2017-03-07
  Mechi za Pili za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA Champions Ligi zinaanza kuchezwa Leo Jumanne Machi 7 kwa Mechi 2.
  • La Liga: Barca yapiga 5, huku Real wafunga 4 2017-03-06
  Mabingwa Watetezi wa La Liga Barcelona jana usiku waliitwanga Celta Vigo 5-0 uwanjani Nou Camp na kurejea kileleni mwa Ligi hiyo baada ya mapema hiyo Jana Real Madrid kuifunga Eibar 4-1 na kukalia kiti hicho.
  • Jeraha la kichwa la Fernando Torres lashtua mashabiki na wachezaji wa Atletico Madrid 2017-03-03
  Staa wa soka wa kimataifa wa Hispania anayeichezea Atletico Madrid Fernando Torres jana usiku aliwawacha kinywa wazi mashabiki wa soka na wachezaji wenzake kufuatia kupata jeraha la kichwa na kufanya kila mchezaji aliyepo uwanjani kushituka kwa jeraha hilo.
  • Yanga yapoza machungu yake kwa kuipigisha kwata Ruvu Shooting 2017-03-02
  Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara, Yanga imefanikiwa kupoza machungu ya kufungwa na Simba mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya jana kuwapigisha kwata maafande wa Ruvu Shooting kwa kipigo cha mabao 2-0. Mabao ya Yanga yalifungwa na Saimon Msuva dakika ya 31 kwa mkwaju wa penati uliopatikana baada ya beki wa Ruvu kuunawa mpira katika eneo la hatari, huku la pili likifungwa kwa ustadi mkubwa na Emmanuel Martin kwa kichwa akimalizia kros ya Saimon Msuva.
  prev 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 next
  SearchYYMMDD  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako