• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • • Davis aweka rekodi mpya katika NBA All-Star Game 2017-02-21
  Nyota wa timu ya Pelicans, Anthony Davis mwenye umri wa miaka 23, ameweka rekodi ya kufunga pointi 52 na kuisaidia timu yake ya upande wa Magharibi kupata ushindi wa pointi 192 kwa 182 dhidi ya timu ya Mashariki katika mchezo maalum.
  • Kombe la FA: Manchester United sasa kutua Stamford Bridge kuivaa Chelsea 2017-02-20
  Manchester United sasa wataenda Stamford Bridge kupambana na vinara wa ligi kuu ya Uingereza Chelsea. Man U imefanikiwa kusonga katika droo ya raundi ya 6 ya kombe la Emirates FA baada ya kuing'oa Blackburn kwa kuichapa mabao 2-1
  • Aureruya ashinda medali ya shaba katika michuano ya mabara 2017-02-17
  Mwanariadha wa Rwanda, Joseph Areruya jana aliwezesha nchi yake kushinda medali ya shaba kwenye mashindano ya riadha ya mabingwa bara la Afrika yanayoendelea mjini Luxor Misri.
  • Siasia apewa nafasi kubwa kuinoa Amavubi ya Rwanda 2017-02-16
  Nyota wa zamani wa Nigeria Samson Amson Siasia pamoja na kocha mkongwe Winfred Schafer wanaongoza kwenye orodha ya makocha 8 wanaopewa nafasi ya kuifundisha timu ya Taifa ya Taifa ya Rwanda -Amavubi.
  •  PSG yaituliza Barcelona, Di Maria atupia mbili 2017-02-15
  PSG imefanikiwa kuilaza Barcelona kwa mabao 4-0 katika mechi ya kwanza ya hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
  • Klabu bingwa Ulaya (UEFA Champions League) kupigwa leo 2017-02-14
  Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA Champions League, inaanza leo usiku kwa Mechi mbili na Jumatano pia zipo Mechi mbili na kuendelea Wiki ijayo, zote zikiwa ni Mechi za Kwanza za Raundi hiyo.
  • Ligi kuu ya England EPL: Chelsea ngoma droo na Burnley 2017-02-13

  Vinara wa ligi kuu ya Uingereza EPL, Chelsea wamelazimishwa sare na Burnley katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza EPL.

  • Mataifa 102 kushiriki Ras Khaiman Half Marathon 2017-02-10
  Kivumbi kinatarajiwa leo Ijumaa katika mbio za Ras Khaimah Half Marathon, ambazo zimevutia mataifa 102.
  • Allan Nyom asema hajutii kuikana Cameroon- AFCON 2017 2017-02-09
  Beki wa West Brom, Allan Nyom amesema hajutii kukataa kwenda kuichezea Cameroon na kubaki na klabu yake, West Brom.
  • Urusi yasimamishwa kushiriki michuano ya kimataifa ya riadha 2017-02-08

  Nchi ya Urusi imesimamishwa kushiriki michuano ya kimataifa ya Riadha baada ya kubainika kwa wanamichezo wake kujihusisha na utumiaji wa madawa ya kusisimua misuli.

  • Refa Andre Marrier kuchezesha fainali ya Manchester United dhidi ya Southampton 2017-02-07
  Refa Andre Marriner amethibitishwa kuwa ndie Refa wa Fainali ya Kombe la Ligi huko England, EFL CUP, kati ya Manchester United na Southampton ambayo itachezwa Uwanjani Wembley Jijini London hapo Jumapili Februari 26.
  • Manchester United yaichapa Leicester City Kwao 2017-02-06
  Manchester United imewatandika Mabingwa wa England Leicester City 3-0 wakiwa nyumbani kwao King Power Stadium kwenye Mechi ya EPL, Ligi Kuu England.
  • Ndugu wawili wakutana fainali Australian Open 2017-01-27
  Ndugu wawili raia wa Marekani Serena na Venus Williams watakutana kwenye fainali ya grand slam kwa mara ya tisa kunako michuano ya wazi ya Australia kufuatia wanadada hao kushinda mechi zao za nusu fainali.
  • Usain Bolt kupokonywa dhahabu moja 2017-01-26
  Bingwa wa mbio za mita 100 upande wa wanaume Usain Bolt atalazimika kurudisha dhahabu moja miongoni mwa dhahabu tisa alizoshinda baada ya mwanariadha mwenza Nesta Carter kupatikana alitumia dawa za kusisimua misuli.
  • Droo ya fainali kombe la dunia - Russia 2018 kufanyika Desemba 1 Kremlin 2017-01-25
  FIFA imethibitisha kuwa Droo za kupanga Makundi na Mechi za Fainali za Kombe la Dunia la Mwaka 2018 huko Russia itafanyika Ijumaa Desemba 1 huko Kremlin Jijini Moscow.
  • Konta uso kwa uso na Serena michuano ya wazi ya Tenisi (Australian Open) 2017-01-24
  Mcheza tenisi wa Uingereza, Johanna Konta ametinga robo fainali ya mashindano ya wazi ya Australia, baada ya kumtoa Mrusi Ekaterina Makarova kwa jumla ya 6-1 6-4, huko Melbourne Park, mjini, Melbourne.
  • Ligi ya Uingereza (EPL) imeendelea jana Arsenal yashinda 2017-01-23
  Arsenal wakiwa kwao Emirates wamefanikiwa kushinda 2-1 kwa penalty dakika za majeruhi wakati wakiwa wachezaji 10 tu uwanjani baada ya kiungo wao Xhaka kulimwa kadi nyekundu, na baadae kocha wao Arsene Wenger kutolewa je ya uwanja.
  • Vivian Cheruiyot awa mwanaspoti bora nchini Kenya mwaka 2016 2017-01-20
  Mshindi wa medali ya dhahabu ya mbio za mita 5,000 na medali ya fedha ya mbio za mita 10,000 za Olimpiki, Vivian Cheruiyot ndiye mwanaspoti bora nchini Kenya mwaka 2016. Cheruiyot, ambaye amejishindia Sh milioni 1 za Kenya, alishinda taji hili mwaka 2011. Katika tuzo ya mwaka 2016, amembwaga bingwa wa marathon za London na Olimpiki, Eliud Kipchoge na wachezaji walemavu Samuel Muchai na Nancy Koech.
  • Van Gaal asema hajastaafu kufunza soka 2017-01-19
  Aliyekuwa meneja wa Manchester United Louis Van Gaal amesema hajastaafu na kwamba anachukua likizo ya mda. Van Gaal mwenye umri wa miaka 65 hajajiunga na timu nyengine tangu aondoke Old Trafford mnamo mwezi Mei.
  • Kombe la FA kuendelea leo, Liverpool ugenini 2017-01-18
  Wakati Droo ya Raundi ya 4 ya Kombe kongwe Duniani, FA CUP, imeshafanyika, Leo Jumatano zipo Mechi za Marudiano za Raundi ya 3 kwa zile Timu zilizoenda Sare.
  prev 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10
  SearchYYMMDD  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako