• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • • SOKA: Victor Wanyama atawazwa mchezaji bora wa mtanange wa MLS 2020-08-03
  Nahodha wa timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars, Victor Wanyama anaonekana kuwa amerejesha makali yake miezi michache baada ya kuhamia Major League Soccer.
  • Bondia mkorofi wa Marekani Floyd Mayweather anafikiri kurudi ulingoni 2020-07-31
  Bondia matata Floyd Mayweather anatajwa kufikiria kurudi ulingoni mwaka huu akiwa na umri wa miaka miaka 43, kwa kinachodaliwa kufuja dola bilioni moja alizopata kutoka kwenye mchezo wa ndondi.
  • Baada ya kufukuzwa Tanzania, SAFA yamfutia vibali vya kazi aliyekuwa kocha wa Yanga Luc Eymael 2020-07-29
  Shirikisho la Soka la nchini Afrika Kusini (SAFA) limemfutia vibali vya kazi Luc Eymael aliyekuwa Kocha Mkuu wa timu ya Yanga kufanya kazi ndani ya nchi Afrika Kusini.
  • Eymael aeleza sababu za kukasirika na kutoa lugha chafu dhidi ya Yanga na mashabiki wake 2020-07-28
  Kocha mbelgiji ambaye jana alitimuliwa na Yanga kutokana na matumizi ya lugha chafu na lugha ya kibaguzi, amesema alifanya hivyo kutokana na hasira, hasa baada ya kuona kuwa timu yake imeshindwa kupata ushindi dhidi ya timu ya Mtibwa sugar, na kulazimishwa sare ya goli moja kwa moja.
  • Wapenzi wa soka Tanzania kuendelea kumfuatilia Samatta lihi kuu ya Uingereza 2020-07-27
  Wapenzi wa soka nchini Tanzania wataendelea kumwona kijana mtanzania Mbwana Ally Samatta akiwa na kikosi cha Aston Villa kilichoinusuru timu hiyo kushuka daraja, baada ya sare ya 1-1 na wenyeji West Ham United Uwanja wa London.
  • SOKA: Baada ya kutemwa na Arsenal Unai Emery sasa aenda kuifunda Villarreal 2020-07-24
  Kocha wa zamani wa klabu ya Arsenal Unai Emery sasa ametangaza rasmi kurejea kufundisha soka nchini Hispania kama kocha mkuu wa klabu ya Villarreal, baada ya klabu hiyo leo kumtambulisha rasmi kama kocha wao mkuu toka afutwe kazi na Arsenal.
  • SOKA: Kyliane Mbappe hana mpango wa kuihama Paris Saint Germain 2020-07-23
  Nyota wa klabu ya Paris Saint Germain ya Ufaransa Kyliane Mbappe amethibitisha kuwa ataendelea kuwa katika klabu hiyo kwa msimu ujao tena licha ya kwamba amekuwa akihusishwa kuwa katika rada za Real Madrid kwa muda mrefu na sasa Mabingwa hao wa Hispania wanadaiwa kuongeza nia.
  • SOKA: Klabu ya Fenerbahce yamkodolea macho Mbwana Samatta 2020-07-22
  Kwa mujibu wa gazeti la habari za michezo la Nchini Uturuki la Takvim limeripoti kuwa klabu ya Fenerbahce ya Uturuki inavutiwa na mshambuliaji mpya wa Aston Villa ya England, Mbwana Samatta.
  • TUZO: Ballon d'Or yafutwa mwaka huu wa 2020 2020-07-21
  Tuzo ya Ballon d'Or inayohusu wanasoka bora wa mwaka haitatolewa mwaka huu wa 2020 kutokana na janga la corona. Waandaaji wa tuzo hiyo, France Football wametangaza uamuzi huo wakidai kwamba hakutakuwa na usawa kutokana na ukweli kwamba janga la corona limesababisha ligi mbalimbali za soka kufutwa ndani ya msimu.
  • SOKA: Kibarua cha kocha Nigel Pearson Watford chaota mbawa 2020-07-20
  Watford wamemtimua kocha Nigel Pearson zikiwa zimesalia mechi mbili pekee kabla ya kampeni za Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) msimu huu kutamatika rasmi.
  • SOKA: Ligi Kuu ya Kenya KPL kubadili jina baada ya kupata ufadhili mpya 2020-07-17
  Ligi Kuu ya Kenya imepata nguvu mpya baada ya kampuni ya Bahati Nasibu ya Nigeria Bet King, kukubali kuifadhili Ligi hiyo kuanzia msimu ujao. Hatua hiyo imekuja baada ya Shirikisho la Soka la Kenya (FKF) kufikia makubaliano na kampuni hiyo hapo jana.
  • SOKA: Harry Kane apitisha idadi ya mabao 200 akicheza soka katika kiwango cha klabu 2020-07-16
  Mshambuliaji Harry Kane alifikisha zaidi ya mabao 200 katika taaluma yake ya soka kwenye ngazi ya klabu baada ya kutikisa wavu mara moja na kusaidia Tottenham Hotspur kuwapepeta Newcastle United 3-1 katika Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) hapo jana.
  • RIADHA: Mwanariadha Alex Korio apigwa marufuku na IAAF 2020-07-15
  Kitengo cha Maadili (AIU) cha Shirikisho la Riadha Duniani (IAAF) kimempiga marufuku mtimkaji Alex Korio Oloitiptip kushiriki mashindano kwa miaka miwili kwa kukiuka kanuni zinazodhibiti matumizi ya pufya.
  • SOKA: Manchester City waponea adhabu baada ya CAS kubatilisha maamuzi ya UEFA 2020-07-14
  Imekuwa afueni kubwa kwa Manchester City baada ya Mahakama ya Kimataifa ya Migogoro katika Michezo (CAS) kubatilisha maamuzi ya awali ya UEFA ambao wamewapiga miamba hao wa soka Uingereza marufuku ya kushiriki kipute cha Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) kwa kipindi cha misimu miwili.
  • CHESS: Kocha wa Chess avutiwa na shindano la vijana wadogo la Afrika 2020-07-13
  Kocha wa mchezo wa Chess nchini Tanzania, Kara Louis ameelezea mashindano ya mchezo huo yaliyofanyika kwa njia ya mtandao yajulikanayo kama African Juniors 11 Team Battle yaliyohusisha nchi sita, kuwa ni mashindano mazuri yatakayowatangaza wachezaji wadogo.
  • Mchezaji Morrison awataka mashabiki waende uwanja wa taifa jumapili 2020-07-10

  BAADA ya kuifungia timu yake bao pekee kwenye ushindi walioupata dhidi ya Kagera Sugar juzi, kiungo mwenye 'mbwembwe' wa klabu ya Yanga, Bernard Morrison amesema hizo ni salamu kwa wapinzani wao

  • 'TUNAWAJUA SIMBA, TUTAWAMALIZA' – Nahodha wa Yanga 2020-07-06
  Wakati mechi ya michezo ya hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Federation (FA) inakaribia nahodha wa Yanga, Juma Abdul, amewatoa hofu mashabiki wa Yanga na kuwataka kuwa na furaha kwenye kipindi hiki ambacho wanafanya maandalizi makubwa kuelekea kwenye mchezo dhidi ya watani wao wa jadi Simba.
  • SOKA: Nembo ya namba tatu iliyopo katika jezi mpya za Chelsea inaonekana kuwa nuksi 2020-07-03
  Nembo ya namba tatu iliyopo katika jezi mpya za Chelsea, zinaweza kutafsiriwa kama ni mkosi baada ya timu hiyo kuchapwa mabao 3-2 na West Ham ikizitumia kwa mara ya kwanza juzi.
  • UHAMISHO: Leroy Sane kuibukia Bayern Munich msimu ujao 2020-07-02
  Kiungo wa Manchester City Leroy Sane, inaelezwa kuwa amemaliza utaratibu wote na Klabu ya Bayern Munich ili aitumikie timu hiyo msimu ujao.
  • SOKA: Lionel Messi afikisha mabao 700, Barcelona wagawana pointi na Atletico Madrid 2020-07-01
  Nyota wa ndani ya Klabu ya Barcelona Lionel Messi, usiku wa kuamika leo alifunga bao moja kwenye sare ya kufungana mabao 2-2 na Atletico Madrid Uwanja wa Nou Camp kwenye La Liga na kufikisha jumla ya mabao 700.
  1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 next
  SearchYYMMDD  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako