• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • • Venus Williams afika hatua ya nusu fainali ya michuano ya wazi ya Marekani 2017-09-07
  Mcheza tenis raia wa Marekani, Venus Williams amefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya wazi ya Marekani (US Open) baada ya kumshinda mpinzani wake Petra Kvitov.
  • Ligi Kuu Uingereza: Drinkwater atua rasmi Chelsea na kuanza mazoezi 2017-09-06
  Kiungo mpya wa Chelsea, Danny Drinkwater ameanza kazi rasmi. Drinkwater amesajiliwa na Chelsea kutoka Leicester City na tayari ameanza mazoezi na kikosi hicho.
  • Michuano ya wazi ya Tennis nchini Marekani, Pliskova atinga robo fainali 2017-09-05
  Karolina Pliskova aamefanikiwa kutinga robo fainali ya michuano ya wazi ya tennis inayoendelea nchini Marekani kwa kumshinda Jennifer Brady marekani kwa jumla ya seti 6-1 na 6-0 mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Arthur Ashe.
  • Serena Williams ajifungua mtoto wa kike, huku dada yake Venus atinga robo fainali mashindano ya wazi ya tennis 2017-09-04
  Bingwa wa tennis Serena Williams amejifungua mtoto wa kike katika hospitali moja ya mjini Florida Marekani. Mwanamama huyo aliweka rekodi ya kushinda kinyanganyiro cha Australian Grand Slam kwa mara ya 23 mwaka huu January, japo alishindana akiwa mja mzito.
  • Chirwa, Kaseke na Msuva wapewa onyo kali na TFF 2017-09-01

  Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imemruhusu kiungo mshambuliaji wa Yanga, Mzambia Obrey Chirwa kuendelea kucheza Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara baada ya kumpa onyo kali kwa kosa la kumghasi refa. Hayo yamefikiwa katika kikao cha kamati hiyo na uamuzi huo unamnufaisha pia kiungo mpya wa Singida United, Deus Kaseke.

  • Liverpool yazungumza na Arsenal kuhusu uhamisho wa Alex Oxlade-Chamberlain 2017-08-31
  Liverpool wameanza mazungumzo na Arsenal kuhusu uhamisho wa kiungo wa kati Alex Oxlade-Chamberlain. Mchezaji huyo mwenye miaka 24 alikataa kuhamia Chelsea Jumanne hata baada ya klabu hizo kuafikiana kuhusu uhamisho wake wa pauni milion 40.
  • PSG yaafikiana na AS Monaco kumsajili Mbappe 2017-08-29
  Timu ya Paris Saint-German (PSG) imefikia makubaliano na AS Monaco kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji kinda Kylian Mbappe kwa mkopo wa mwaka mmoja ambapo hapo baadaye wanaweza wakamsajili moja kwa moja kwa ada ya pauni 166 milioni katika majira ya joto mwakani.
  • Cristiano Ronaldo atangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa Ulaya 2017-08-25

  Baada ya Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA jana mjini Monaco Ufaransa kuchezesha droo ya hatua ya makundi ya UEFA Champions League msimu wa 2017/2018, walitangazwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa Ulaya 2016/2017.

  • Neymar kwenda mahakamani kupinga mashtaka yaliowasilishwa na klabu ya Barcelona. 2017-08-24

  Mshambuliaji wa Paris St-Germain Neymar amesema kuwa ataenda mahakamani kupinga mashtaka yaliowasilishwa na klabu yake ya zamani Barcelona.

  • Barcelona yapanga kumshtaki Neymar, yataka ilipwe Pauni milioni 7.8 2017-08-23
  Klabu ya Barcelona imepanga kumshitaki Neymar ikidai ilipwe pauni milioni 7.8. Klabu hiyo inaamini kuwa Neymar alikiuka makubaliano ya mkataba wakati akihamia PSG aliyojiunga nayo kwa kitita cha pauni milioni 198.
  • Rooney afunga bao la 200, Everton yaivuta shati Man City 2017-08-22
  Mshambuliaji Wayne Rooney wa Everton amefunga bao lake la 200 katika ligi kuu ya Uingereza (EPL) wakati timu yake ikitoka sare ya mabao 1-1 dhidi ya Manchester City.
  • Mechi za kwanza za ligi kuu Hispania-La Liga: Ramos alimwa kadi nyekundu 2017-08-21
  Nahodha wa Real Madrid, Dergio Ramos amepigwa kadi nyekundu katika mechi ya kwanza ya ligi kuu ya Uhispania (La Liga) wakati Madrid walipomenyana na Derpotivo la Coruna.
  • Ibrahimovic kupewa majukumu ya ukocha Manchester 2017-08-18
  Mshambuliaji wa Manchester United, Zlatan Ibrahimovic mwenye umri wa miaka 35 anatarajiwa kukabidhiwa majukumu mapya akikamilisha kusaini mkataba wake na Manchester United
  • Usain Bolt aitwa kujiunga timu ya soka Burton Albion 2017-08-17
  Mwanariadha wa Jamaica Usain Bolt amepewa ofa kujiunga na klabu ya Ligi Daraja la Kwanza England ya Burton Albion, baada ya kutangaza kustaafu akiwa kwenye mashindano ya Riadha ya Dunia yaliyomalizika London jumapili.
  • Neymar asema amezaliwa upya ndani ya PSG 2017-08-16
  Baada ya kupata tuzo la mchezaji bora wa mechi kwa kutengeneza mabao mawili na kufunga moja dhidi ya Guingamp, Neymar ameanza kufurahia maisha ndani ya Paris Saint-Germain, akisema ameanza maisha Ufaransa huku kukiwa na shutuma kuhusu uamuzi wake wa kuondoka Barcelona.
  • Diego Costa asema Chelsea hawamtaki tena 2017-08-15
  Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uispania Diego Costa amesema Chelsea wamekuwa wakimchukulia kama mhalifu na akathibitisha kwamba bado anataka kurejea Atletico Madrid kwani kulingana naye klabu hiyo haimtaki tena.
  • Shirikisho la Kandanda la Tanzania TFF yapata rais mpya 2017-08-14
  Aliyekuwa makamu wa Rais na kaimu wa Rais wa TFF Wallace Karia ametangazwa rasmi kuwa Rais mpya wa TFF kwa kupata jumla ya kura 95 na kuwashida Ally Mayay, Emmanuel Kimbe, Shija Richard, Iman Madegana Fredrick Mwakalebela.
  • Shirikisho la soka Tanzania TFF kuandaa uchaguzi Jumamosi 2017-08-11
  KAMATI ya rufani ya uchaguzi wa TFF iliyoketi juzi Jumanne, imewarejesha baadhi ya wagombea waliokuwa wameenguliwa awali wakiwemo wanne waliotuhumiwa kujihusisha na vitendo vya rushwa. Kikao hicho kilichofanyika Ukumbi wa St. Gasper kilifanya uamuzi mgumu.
  • Roger Federer apaa Montreal 2017-08-10
  Roger Federer alianza vyema maandalizi yake ya mashindano ya US Open katika mashindano ya ATP Montreal Masters siku ya Jumatano, kwa kumshinda mchezaji wa Canada Peter Polansky kwa seti mtawalia na kufuzu kwa raundi ya tatu.
  • Rais wa Barcelona alalamikia uhamisho wa Neymar 2017-08-08

  Rais wa klabu ya Barcelona Josep Maria Bartomeu amemkashifu Neymar kwa njia ambayo aliondoka klabu hiyo na kuingia Paris Saint Germain ya Ufaransa.

  prev 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 next
  SearchYYMMDD  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako