• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • • VOLIBOLI: Malkia Strikers yajikatia tiketi ya kuingia kwenye mashindano ya Olimpiki ya Tokyo 2020-01-10
  Timu ya taifa ya mpira wa voliboli kwa akina dada, Malkia Strikers, wamejikatia tiketi ya kuingia kwenye mashindano ya Olimpiki mwaka huu yatakayofanyika mjini Tokyo, Japan.
  • SOKA: Nafasi ya Zahera Yanga yachukuliwa na Mbelgiji 2020-01-09
  Mabingwa wa kihistoria wa ligi kuu soka Tanzania Bara Young Africans wanatarajia kumpa kazi ukocha Mbelgiji, Luc Eymael ambaye anarithi mikoba ya Mkongo Mwinyi Zahera.
  • SOKA: Sadio Mane atawazwa mchezaji bora Bara Afrika 2020-01-08
  Mshambuliaji wa Liverpool Sadio Mane amembwaga mwezake Mohamed Salah na staa wa Man City Riyad Mahrez kutawazwa mchezaji bora Bara Afrika wa mwaka 2019.
  • Sadio Mane atwaa tuzo za CAF na kuwashinda MO Salah na Riyad Mahrez 2020-01-08
  Usiku wa tuzo za CAF ziolizotolewa nchini Misri katika jiji la Cairo umemalizika kwa kushuhudia watu mbalimbali wakishinda tuzo. Sadio Mane wa Liverpool na timu ya taifa ya Senegal ndio aliibuka mshindi wa tuzo ya mchezaji bora Afrika mwaka 2019 kwa kuwashinda MO Salah wa Liverpool na Riyad Mahrez wa Man City.
  • SOKA: Lukaku akoleza moto wa manao Inter Milan 2020-01-07
  Mshambuliaji nyota Romelu Lukaku amefunga mabao mawili katika mchezo wa Ligi Kuu Italia na kufikisha mabao 14 tangu alipojiunga na Inter Milan akitokea Manchester United ambako alishindwa kung'ara chini ya kocha Ole Gunnar Solskjaer.
  • Cristiano Ronaldo aanza mwaka kwa kishindo kwa kupata hat-trick yake ya kwanza kwenye ligi ya Serie A 2020-01-07
  Cristiano Ronaldo jana alifunga hat-trick yake ya kwanza katika mwaka huu kwenye ligi ya Serie A na kuipaisha juu Juventus kwenye msimamo wa ligi baada ya kupata ushindi wa 4-0 dhidi ya Cagliari huku Zlatan Ibrahimovic mambo yakimwendea kombo kwani alionekana kutotosha mboga katika klabu yake ya AC Milan kwa kuanza mechi yake ya kwanza akiondoka kapa ambapo walitoka sare ya bila kufungana dhidi ya Sampdoria.
  • Vituko vya ubaguzi wa rangi vyaendelea kwenye viwanja vya soka Italia 2020-01-06
  Vituko vya ubaguzi wa rangi dhidi ya wachezaji wa wasio wazungu vinaendelea kuonekana kwenye ligi ya Italia, lakini jibu la mwanasoka mkorofi Mario Balloteli limeleta machungu kwenye suala hilo.
  • Sanamu ya Zlatan Ibrahimovic sasa yaangushwa chini 2020-01-06
  Sanamu la mshambuliaji wa klabu ya AC Milan Zlatan Ibrahimovic lililopo nje ya uwanja wa klabu yake ya zamani iliyomlea Malmo huko chini Sweden lakatwa hadi kuanguka chini.
  • RIADHA: Mwanariadha Cheruiyot kufukuzia rekodi ya dunia 2020 2020-01-03
  Timothy Cheruiyot, nyota anayejitahidi kurithi mikoba ya Asbel Kiprop ambaye ni bingwa wa mbio za mita 1,500 aliyefungiwa kwa miaka minne kwa kutumia dawa za kuongeza nguvu, ametangaza kuwa mwaka huu utakuwa wa kukimbizana na rekodi ya dunia katika mita hizo.
  • Michael Sarpong akamilisha uhamisho naa kuja kucheza kwenye klabu ya China 2020-01-03
  Mshambuliaji wa Rayon Sports Michael Sarpong amekuwa mwanasoka ghali zaidi kusainiwa katika ligi kuu ya Rwanda baada ya kukamilisha hatua yake ya kuhamia kwenye timu ya daraja la pili ya China Changchun Yatai.
  • Ubaguzi wamtesa kipa wa Cameroon 2020-01-02
  Kipa wa Ajax Amsterdam Andre Onana ambaye ni raia wa Cameroon amesema makipa wenye asili ya Afrika hawana nafasi katika klabu kubwa kutokana na rangi. Kipa huyo mwenye miaka 23 amesema licha ya ubora wa makipa kutoka Afrika, lakini klabu kubwa haziwapi nafasi kwa sababuya ubaguzi
  • TUZO: Kombora la Victor Wanyama katika tuzo ya bao bora 2020-01-02
  Huku Victor Wanyama akizidi kuhusishwa na tetesi za kuondoka klabu yake ya Tottenham Hotspur katika kipindi kifupi cha uhamisho kilichoanza jana Jumatano, kombora la nahodha huyo wa timu ya taifa ya Kenya dhidi ya Liverpool msimu uliopita linawania bao la mwongo.
  • Wapongeza ununuzi kilo 250,000 tumbaku 2020-01-01

  Wakulima wa Chama cha Msingi Ngokolo, Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga, wameipongeza kampuni ya Petrobena kwa kununua tumbaku kilo 250,000 iliyokuwa imebaki na kugawa pembejeo za kilimo hicho kwa msimu ujao kwa wakati.

  • Simba yaingia 2020 na salamu kwa Yanga 2020-01-01
  Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara Simba Sports Club wameukaribisha mwaka wa 2020 kwa kutuma salamu za ushindi kwa watani zao, Yanga, baada ya kuichapa Ndanda FC mabao 2 – 0 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana.
  • SOKA: Arturo Vidal aishtaki Barcelona akidai hajalipwa pauni milioni 2 za posho mbalimbali 2020-01-01
  Kiungo wa Barcelona, Arturo Vidal, amechukua hatua ya kushangaza dhidi ya klabu yake hiyo. Ameamua kuishtaki akidai hajalipwa pauni milioni 2 za posho mbalimbali
  • SOKA: Samatta, Salah, katika kikosi cha Waafrika waliotisha 2019 2019-12-31
  Zikiwa zimebaki saa kadhaa kuumaliza mwaka huu wa 2019, nikufahamishe tu mastaa wa Kiafrika waliofanya vizuri mwaka huu katika ligi mbalimbali za mataifa makubwa barani Ulaya.
  • Man United yamgeukia kinara wa mabao Lyon 2019-12-30
  Pamoja na kuwa Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer amekosa saini ya kinda Erling Haaland, lakini hajakata tamaa ya kuisuka timu hiyi, na sasa anatupia jicho kusajili mshambuliaji na kiungo.
  • SOKA: David Moyes akabidhiwa tena mikoba ya West Ham 2019-12-30
  David Moyes ameteuliwa kuwa meneja mpya wa West Ham na atarejea kwa mara ya pili kwenye klabu hiyo. Mscotland huyo mwenye miaka 55 amesaini mkataba wa miezi 18 na ataanza na mechi ya nyumbani ya siku ya mwaka mpya dhidi ya Bournemouth.
  • SOKA: Simba yapanga hesabu Ligi Kuu 2019-12-27
  Zikiwa zimesalia siku chache kabla ya watani wa jadi kukutana kwa mara ya kwanza katika msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Kocha Msaidizi wa Simba Selemani Matola amesema kuwa bado kikosi chake hakijaanza kuufikiria mchezo huo utakaochezwa Januari 4 mwakani.
  • SOKA: Coutinho afikiria kurudi England 2019-12-26
  Staa raia wa Brazil, Phillipe Coutinho amefungua mlango wa kurudi kwenye Ligi Kuu England mwakani kama Bayern Munich watagoma kumchukua moja kwa moja wakati muda wake wa mkopo utakapokamilika.
  prev 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 next
  SearchYYMMDD  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako