• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • • Ronaldo ashinda tuzo ya mwanasoka bora wa FIFA, Ranieli achukua tuzo ya kocha bora 2017-01-10
  Mshambuliaji Cristiano Ronaldo ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) mwaka 2016 baada ya kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya na Real Madrid na kuiwezesha Ureno kutwaa Kombe la Euro.
  • Mbio za Dunia za Nyika 2017 kufanyika Kampala Uganda 2017-01-09
  Mashindano ya Dunia ya Mbio za Nyika yanatarajiwa kufanyika nchini Uganda mwezi Machi mwaka huu huku timu mbalimbali za Afrika Mashariki ni miongozi mwa nchi zinazotarajia kupeleka timu katika mpambano huo.
  • Paul Clement awa kocha mpya wa Swansea City 2017-01-06
  Klabu ya soka ya Swansea City imemtangaza rasmi Paul Clement kuwa ndio kocha wao mpya. Swansea City imempa kocha huyo mkataba wa miaka miwili na nusu.
  • Timuatimua ya makocha: Hull City yamfukuza Mike Phelan 2017-01-05
  Katika ule mwendelezo wa timuatimua ya makocha klabu ya ligi kuu ya soka nchini Uigereza, Hull City imemfukuza kocha wake mkuu Mike Phelan, kutokana na mwenendo mbaya wa timu hiyo, kwenye ligi.
  • Guardiola akaribia kustaafu kufundisha soka 2017-01-04

  Kocha wa Man City Pep Guardiola amesema kuwa klabu hiyo inawezakuwa klabu yake ya mwisho kuifundisha baada ya kukasirishwa na maamuzi ya mwamuzi wa mchezo wa jana dhidi ya Bournemouth.

  • Hillary Ojwang mfungaji bora KPL Under 20 2017-01-03
  Kinda wa Gor Mahia, Hillary Ojwang ndiye mshindi wa tuzo ya mfungaji bora wa soka ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 20 ya wavulana ya KPL
  • Ligi kuu ya Uingereza imeendelea juzi na jana 2017-01-02

  Liverpool imemaliza Mwaka 2016 kwa ushindi mtamu kwao Anfield walipoitungua Manchester City 1-0 na kubaki nafasi ya Pili kwenye ligi kuu ya Uingereza (EPL), wakiwa Pointi 6 nyuma ya Vinara Chelsea.

  • Maafisa wa Urusi wakiri kuwepo kwa mipango ya matumizi ya dawa za kuongeza nguvu Urusi 2016-12-29

  Kwa mara ya kwanza, Maafisa wa Urusi wamekiri kuwepo kwa mipango ya matumizi ya dawa zilizopigwa marufuku ambayo imeathiri mashindano makubwa duniani.

  • Wilfred Ndindi aripotiwa kukaribia kujiunga na Leicester City 2016-12-28
  Kiungo wa kimataifa wa Nigeria anayeichezea KRC Genk ya Ubelgiji Wilfred Ndindi ameripotiwa kukaribia kujiunga na Leicester City January 1 2017. Habari kutoka express.co.uk zinasema Ndindi tayari amekamilisha uhamisho wake wa kujiunga na Leicester City na kinachosubiriwa ni kutangazwa rasmi January 1 2017.
  • Chelsea yapeta kileleni, Man U mambo safi, Wakati Arsenal 2016-12-27
  Chelsea wamepaa Pointi 9 juu kwenye, Ligi Kuu England EPL baada kuichapa Bournemouth 3-0 kwa Bao za Pedro, Bao 2, na Penati ya Eden Hazrad huko Stamford Bridge na kujizatiti kileleni mwa ligi hiyo.
  • Wenger: Ozil atawashangaza wakosoaji wake 2016-12-26
  Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger anasema kuwa kiungo wa kati wa timu hiyo Mesut Ozil atawashangaza wakosoaji wake katika mechi inayofuata.
  • Kibarua cha Alan Pardew chaota mbawa Crystal Palace 2016-12-23
  Klabu ya Crystal Palace imemfuta kazi mkufunzi wake Alan Pardew wakati ambapo klabu hiyo iko katika nafasi ya 17 katika ligi ya Uingereza.
  • Andre Ayew ajitapa timu ya taifa ya Ghana inaweza kutwaa taji la Kombe la Mataifa la Afrika 2016-12-22
  Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ghana Andre Ayew amejinasibu kuwa timu yake hiyo ya taifa inaweza kutwaa taji la Kombe la Mataifa la Afrika mwakani nchini Gabon.
  • Petra Kvitova ashambuliwa kwa kisu 2016-12-21
  Bingwa wa zamani wa mchezo wa Tennis Wimbledon, Petra Kvitova, amefanyiwa upasuaji kwenye mkono wake kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya kushambuliwa kwa kisu katika moja ya miji ya Jamhuri ya Chekslovakia.
  • Barcelona yapiga Espanyol 4-1 Ligi ya La Liga 2016-12-20
  Luis Suarez amepiga Bao 2 wakati Barcelona ikiwachapa Mahasimu wao Espanyol 4-1 katika Dabi yao na kupanda hadi Nafasi ya 2 kwenye La Liga.
  • Bernard Hopkins apigwa knockout pigano la mwisho 2016-12-19
  Bondia Bernard Hopkins ameshindwa katika pigano lake la mwisho baada ya bingwa huyo wa ndondi mwenye umri wa miaka 51 kupigwa kwa njia ya knockout katika raundi ya 8 na Joe Smith Jr.
  • Carlos Tevez akana kustaafu soka 2016-12-16
  Mchezaji wa zamani wa vilabu vya Manchester City na Manchester United, Carlos Tevez ambaye hivi sasa ana miaka 32 amefunguka kuhusu uzushi ambao ume enea kuwa amestaafu soka.
  • Chelsea na Manchester City wapigwa faini 2016-12-15
  Chelsea wamepigwa faini ya £100,000 na Manchester City wakapigwa faini ya £35,000 baada ya wachezaji wao kuhusika katika vurugu uwanjani wakati wa mechi ya Ligi ya Premia.
  • Messi akutana na mtoto aliyevaa jezi ya karatasi Afghanistan 2016-12-14
  Murtaza Ahmad mtoto mwenye umri wa miaka 6 kutoka nchini Afghanistan aliyepata umaarufu sana kwenye mitandao duniani mwezi Januari mwaka huu baada ya kupigwa picha akiwa amevalia mfuko wa nailoni aliotengeneza kama jezi ya Lionel Messi hatimaye amefanikiwa kukutana na Lione Messi.
  • Cristiano Ronaldo ashinda tuzo ya Ballon d'Or 2016, huku Riyad Mahrez ashinda tuzo ya BBC ya mchezaji bora Afrika 2016-12-13

  Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo amemshinda mpinzani wake Lionel Messi na kupata tuzo ya mchezaji bora wa dunia Ballon d'Or hii ikiwa ni kwa mara ya nne.

  Ronaldo mwenye miaka 31 sasa anahitaji tuzo moja tu kumfikia Messi ambaye mwaka jana alipata tuzo ya tano.

  prev 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 next
  SearchYYMMDD  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  Maoni yako