• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • • Mwanariadha wa Ethiopia Feyisa Lilesa ahofia usalama wake 2016-08-23

  Mwanariadha wa Ethiopia Feyisa Lilesa ametajwa kama mwanariadha mkakamavu kwenye michezo ya olimpiki ya mwaka huu iliyokamilika mjini Rio , Brazil baada ya kuonyesha ishara za upinzani dhidi ya serikali.

  • Olimpiki yakamilika 2016-08-22

  Michezo ya Olimpiki imekamilika nchini Brazil kwenye shererehe ya kufunga mashindano hayo iliofanyika katika uwanja wa Maracana mjini Rio de Janeiro.

  • Conseslus Kipruto avunja rikodi ya Olimpiki ya mita 3000 kuruka viunzi 2016-08-18
  Jana mchana Wakenya walijumuika pamoja kumshangilia mwanariadha aliyeshiriki kwenye mbio za kuruka viunzi mita 3000, Conseslus Kipruto baada ya kuimarisha nguvu ya Kenya na kuvunja rikodi ya zamani ya Olimpiki ya dakika 8 sekunde 5 na nukta 51 ambayo iliwekwa na Julius Kariuki mwaka 1988 kwenye Olimpiki ya Seoul na sasa ameandika muda wa dakika 8 sekunde 3 na nukta 29.
  • Aliyekuwa rais wa FIFA Joao Havelange afariki 2016-08-17

  Aliyekuwa rais wa zamani wa FIFA Joao Havelange amefariki akiwa na umri wa miaka 100.

  • Chelsea yailaza west ham 2-1 2016-08-16
  • Yanga yaipiga MO Bejaia 1-0 2016-08-15

  Klabu ya Yanga ya Dar es Salaam imefufua matumaini ya kutinga hatua ya nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kuichapa MO Bejaia ya Algeria.

  • Michael Phelps ajichukulia medali ya 21 kwenye michezo ya Olimpiki 2016-08-11
  Muogeleaji wa Marekani, Michael Phelps, ameweka rekodi ya kushinda medali ya dhahabu ya 21, kwenye michezo ya Olimpiki, huko Rio, Brazil usiku wa kuamkia jana.
  • Usain Bolt kustaafu riadha mwaka ujao 2016-08-10
  Mwanariadha Usain Bolt amedokeza kustaafu riadha ifikapo Februari mwaka 2017 baada ya michuano ya Mabingwa wa Dunia, na kuongeza kuwa hii itakuwa ni michuano yake ya mwisho ya Olimpiki kushiriki.
  • Simba yaiadhibu AFC Leopard 4-0 2016-08-09
  Simba wameibuka na ushindi wa goli 4-0 katika mchezo wa kirafiki dhidi ya AFC Leopard ya Kenya uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
  • Liverpool yaitandika Barcelona mabao 4-0 2016-08-08

  Liverpool imeitandika Barcelona mabao 4-0 kwenye michuano ya ubingwa wa kimataifa ICC iliochezewa uwanja wa Wembley mjini London.

  • Tyson Fury, afunguliwa mashtaka kwa kutumia dawa za kuongeza nguvu 2016-08-05
  Bingwa wa dunia uzito wa juu Tyson Fury, amefunguliwa mashtaka ya kutumia dawa zilizopigwa marufuku michezoni, na chama cha kupambana na dawa hizo Uingereza, Ukad. Ukad, ilimsimamisha Fury Juni 24 mwaka huu, siku ambayo Bondia huyo alitangaza kufuta pambano lake la marudiano na Wladimir Klitschko kwa sababu ya majeruhi, lakini Fury alikata rufaa na hukumu hiyo ikaondolewa.
  • Kocha wa Yanga Hans van Pluijm aahidi makubwa dhidi ya MO Bejaia 2016-08-04
  Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga, Hans van Pluijm, amepanga kurejesha imani na furaha iliyopotea kwa mashabiki wa timu hiyo kwa kuhakikisha wanawafunga MO Bejaia katika mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika.
  • Kevin Prince Boateng asajiliwa na Klabu ya Las Palmas 2016-08-03
  Kiungo wa kimataifa wa Ghana Kevin Prince Boateng Amesajiliwa na Klabu ya Las Palmas ya nchini Hispania kwa mkataba wa Mwaka Mmoja
  • Rubin Kazan ya Russia yamsaini kiungo wa kati wa Barcelona Alex Song 2016-08-02
  Klabu ya Rubin Kazan ya Russia imemsaini kiungo wa kati wa Barcelona Alex Song lakini ni uhamisho usiokuwa na ada yoyote.
  • Lewis Hamilton atwaa ushindi wa German Grand Prix 2016-08-01
  Mwendesha langalanga Lewis Hamilton alizimiliki mbio za German Grand Prix akitwaa ushindi kwa pointi 19 na kunshinda mwenzake wa timu ya Mercedes Nico Rosberg.
  • Juventus yakamilisha usajili wa Gonzalo Higuain 2016-07-28

  Klabu ya Juventus imekamilisha usajili wa mshambuliaji wa Argentina, Gonzalo Higuain kutoka klabu ya Napoli kwa pauni milioni 75.5. Mchezaji huyo mwenye miaka 28 amesaini mkataba wa miaka mitano baada ya Juventus kukubali kutoa kitita hicho kinachokaribia Euro milioni 90 ambazo watazilipa kwa awamu.

  • Yanga yaadhibiwa 3-1 na Medeama ya Ghana 2016-07-27

  Klabu ya Yanga ya Dar es salaam Tanzania leo imejiweka katika mazingira magumu zaidi ya kufuzu kuingia katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika baada ya kuchapwa bao 3-1 na Medeama ya Ghana.

  • Uganda yapaa hadi nafasi ya 42 kwa raga duniani 2016-07-26

  Uganda imepaa nafasi nane katika viwango vipya vya raga duniani, ambavyo vimetangazwa Jumatatu.

  • Kikosi cha Stars dhidi ya Nigeria kutajwa kesho 2016-07-25

  Kocha MkuuTaifa Stars Charles Mkwasa wiki ijayo anatarajia kutangaza kikosi kwa ajili ya kambi ya awali ya wiki moja ikiwa ni maandalizi ya kucheza na Nigeria katika mchezo wa kukamilisha ratiba ya kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika.

  • Simba na Yanga kukutana Oktoba Mosi mwaka huu 2016-07-20

  Watani wa jadi Simba na Yanga watakutana Oktoba 1 mwaka huu katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

  prev 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 next
  SearchYYMMDD  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako