Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
 
Mji wa kale wa Fenghuang 2006/10/16
Mji wa Fenghuang uko katika sehemu ya milimani ya jimbo linalojiendesha la makabila ya watujia na wamiao ya magharibi ya mkoa wa Hunan, China.
Matembezi kwenye sehemu ya vijiji na mapumziko kwa shughuli za kiutamaduni yapendwa zaidi na watalii wakati wa sikukuu  2006/10/02
Tarehe 1 mwezi Oktoba mwaka huu ni siku ya kutimia miaka 57 tangu Jamhuri ya watu wa China iasisiwe, ambapo watu wa China wanapata likizo ya wiki moja, hivyo sehemu mbalimbali zimeanzisha shughuli mbalimbali za utalii zikiwemo za masafa ya wastani na mafupi
Haiyang mkoani Shandong, China 2006/09/18
Baada ya kupita siku za joto, upepo mwanana wa majira ya mpukutiko unawafurahisha watu zaidi, katika majira hayo shughuli za kuwafuata wavuvi kwenda baharini kuvua samaki na kujionea maisha ya wavuvi zimekuwa shughuli za utalii zinazopendwa na watu wengi.
Hekalu la Chongsheng mkoani Yunnan  2006/09/04
Hekalu la Chongsheng la sehemu inayojiendesha ya kabila la wabai la Dali mkoani Yunnan, kusini magharibi ya China ni hekalu la kale lililojengwa zaidi ya miaka elfu moja iliyopita.
Mji wa Liye 2006/08/21
Magharibi mwa Mkoa wa Hunan, katikati ya China ni sehemu inayowavutia sana watalii. Katika sehemu hiyo, kuna miji mingi ya kale ya makabila mbalimbali iliyojengwa katika sehemu yenye milima na mito yenye sura ajabu na ya kuvutia, miji hiyo ya kale ina mvuto mkubwa wa kikabila. Mji wa Liye ni moja ya miji hiyo.
Xidi na Hongcun 2006/08/07
Mlima Huangshan wa China unajulikana nchini na duniani, hivyo kila mwaka watalii wengi kutoka sehemu mbalimbali nchini China na nchi za nje huenda huko kutalii.
Mandhari nzuri ya sehemu ya Magenge Matatu yavutia watu zaidi 2006/07/24
Ujenzi wa Boma kubwa la Magenge Matatu kwenye Mto Changjiang nchini China umekamilika, ambapo kiwango cha maji kwenye Bwawa la Magenge Matatu kimeinuka na kufikia mita 135, hivyo bonde hilo kubwa ni bonde pekee linaloweza kuwawezesha watalii kupanda meli kuangalia mandhari, ni bonde linalowavutia zaidi watalii.
Reli ya kutoka mkoa wa Qinghai hadi mkoa wa Tibet, China 2006/07/10
Reli ya kutoka mkoa wa Qinghai hadi mkoa wa Tibet, China imezinduliwa kuanzia tarehe 1 Julai mwaka huu. Reli hiyo imejengwa kwenye Uwanda wa Juu wa Qinghai-Tibet wenye mwinuko mkubwa kutoka usawa wa bahari. Ili kuwawezesha watalii wanaopanda garimoshi wapate raha na usalama kwenye safari yao, idara husika zilifanya usanifu maalum wa garimoshi linalopita kwenye reli hiyo.
Vichochoro mjini Beijing 2006/06/26
Mjini Beijing kuna msemo unaosema kuwa, "Huwezi kuijua Beijing bila kuingia kwenye vichochoro mjini humo, na utasikitika sana kama utashindwa kutembelea vichochoro mjini Beijing
Sehemu ya Lao Cheng Huang Miao mjini Shanghai  2006/06/12
Katika sehemu ya katikati mjini Shanghai, kuna sehemu moja maalum iitwayo Laochenghuangmiao, ambapo kuna bustani yenye hali tulivu, maduka mengi yaliyoanzishwa zaidi ya miaka 100 iliyopita, na pia kuna mikahawa mingi ya chakula na chai. Sehemu hiyo imekuwa kama alama moja ya mji wa Shanghai.
1 2 3 4 5 6 7 8 9 10