Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
 
Yibin, Mji wa kwanza kwenye eneo la mtiririko wa mto Changjiang 2008/11/17
Huenda bado mnakumbuka Sinema iitwayo "Corouching Tiger, Hidden Dragon", ambayo iliteuliwa kuwa ni sinema nzuri kabisa ya sinema za lugha za kigeni mwaka 2001 na kupewa tuzo ya Academy. Katika sinema hiyo "mapigano kwenye msitu wa mianzi" ni Sehemu inayopendeza zaidi. Mabingwa wawili wa kike na kiume wenye Wushu wa kiwango cha juu walipigana kwenye msitu huo wa mianzi, na kuonesha vilivyo sifa za Wushu wa China. Msitu wa mianzi unaoonekana kwenye sinema hiyo ni msitu wa mianzi wa Shunan ulioko kusini mashariki mwa mji wa Yibin, mkoani Sichuan, ambao unasifiwa kama moja kati ya misitu mizuri kabisa ya nchini China.
Kutembelea sehemu za peponi  2008/10/20
Wasikilizaji wapendwa, sasa tunawaletea makala ya kwanza ya Mashindano ya chemsha bongo kuhusu ujuzi wa Vivutio vya Sichuan". Kabla ya kusoma makala hii tunatoa maswali mawili: 1, Bonde la Jiuzhaigou lilipata jina hilo kutokana na kuwepo kwa vijiji 9 vya watu wa kabila la watibet ndani ya sehemu hiyo au la? 2. Je, Bonde la Jiuzhaigou na Sehemu ya vivutio ya Huanglong zote zimeorodheshwa kuwa mali ya urithi wa mazingira ya asili duniani ? Tafadhali sikilizeni kwa makini makala tunayowasomea ili muweze kupata majibu.
Vyakula vitamu vya Kiislamu katika mtaa wa Niujie mjini Beijing 2008/10/06
Vyakula vya Kibeijing viko vya aina nyingi, na miongoni mwa vyakula hivyo, vingi ni vya Kiislamu. Vyakula vya Kiislamu vya aina nyingi vinapikwa kwa nyama ya ng'ombe au mbuzi. Katika mtaa wa Niujie mjini Beijing wanakoishi Waislamu wengi, vyakula vya Kiislamu vinajulikana zaidi.
Msitu wa mawe nchini China  2008/07/28
Sehemu yenye mandhari ya msitu wa mawe mkoani Yunnan, kusini magharibi mwa China ni sehemu ya utalii ya mjini Kunming toka miaka mingi iliyopita, sehemu hiyo inajulikana sana duniani kwa kuwa na mawe mengi makubwa ya chokaa yenye maumbo ya ajabu yanayojitokeza kwenye ardhi.
Kutalii kwenye kijiji cha Shifo cha mji wa Zhengzhou 2008/07/07
Katika miji mingi mikubwa ya China kuna sehemu moja yenye wakazi wengi wasomi na wachoraji wa michoro ya sanaa. Kwa mfano kiwanda No. 958 cha Beijing na sehemu ya wasanii iliyoko kando ya mto Suzhou mjini Shanghai.
"Mahekalu manane ya sehemu ya nje" ya mji wa Chengde 2008/06/23
Hekalu la Puning lililoko mji Chengde, mkoani Hebei, China ni hekalu maarufu ya dini ya kibudha ya kitibet kwenye sehemu ya kaskazini ya China. Hekalu hilo lilijengwa kwenye utawala wa Qianlong wa enzi ya Qing katika karne ya 18.
Shughuli za utalii mkoani Hunan zarejeshwa katika hali ya kawaida 2008/06/09
Maafa ya baridi kali na theluji yaliyotokea mwanzoni mwa mwaka huu yalisababisha hasara kubwa kwa uchumi wa mkoa wa Hunan, China, na pia kwa shughuli za utalii ya huko. Kutokana na takwimu zisizokamilika, hasara iliyosababishwa na maafa hayo kwenye shughuli za utalii mkoani Hunan ilifikia Yuan milioni 600.
Mto unaopendeza waunganisha vivutio vyote vya mkoa wa Guangxi  2008/05/27
Mkoa unaojiendesha wa kabila la wazhuang la Guangxi una mandhari nzuri na vivutio vingi vya utalii, ambapo watu wa makabila madogo mbalimbali wanaishi huko, kila kabila lina mvuto wake kipekee. Kama mnapenda kujua mengi zaidi kuhusu mkoa huo, karibuni msikilize kipindi maalum cha chemsha bongo kuhusu ujuzi wa vivutio vya utalii mkoani Guangxi...
Mtaa wenye mikahawa inayouza vyakula vitamu vya aina mbalimbali  2008/05/26
Mkoa wa Qinghai uko kwenye sehemu ya kaskazini magharibi ya China, na unajulikana kutokana na kuwa na mandhari nzuri ya maumbile. Katika kipindi hiki cha leo tunawafahamisha kuhusu mtaa mmoja wenye mikahawa inayouza vyakula vitamu vya aina mbalimbali, ulioko katika mji wa Xining, mji mkuu wa mkoa wa Qinghai, pamoja na utamaduni wa vyakula wa uwanda wa juu.
Jumba la makumbusho la Hanyangling  2008/05/05
Kwenye sehemu ya kaskazini ya mji wa Xian, mji mkuu wa mkoa wa Shanxi, kuna makaburi mengi ya wafalme wa enzi ya kale ya Han ya Magharibi, kati ya makaburi hayo makaburi ya Hanyangling yamekuwa na historia ya zaidi ya miaka 1,200. Hivi sasa kwenye makaburi ya Hanyangling ya enzi ya Han, limejengwa jumba la makumbusho, ambalo ni jumba la kwanza la kisasa lililojengwa chini ya ardhi nchini China.
1 2 3 4 5 6 7 8 9 10