Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
 
v Wazee wanastahili maisha ya raha mustarehe 2007/01/18
China ni nchi yenye watu bilioni 1.3, na ni moja kati ya nchi ambazo idadi ya wazee inaongezeka kwa kasi. Hivi sasa wananchi wa China wenye umri wa zaidi ya miaka 60 wamefikia watu milioni 144, idadi ambayo ni nusu ya wazee wa bara zima la Asia. Inakadiriwa kuwa hadi kufikia mwaka 2020, idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka kwa watu milioni 100. Namna ya kuwahakikisha wazee waishi kwa raha mustarehe ni suala linalofuatiliwa na jamii ya China.
v Mashujaa wanaopenda kuogelea maziwani wakati wa siku za baridi 2007/01/04
Mji wa Changchun upo mkoani Jilin, kwenye sehemu ya kaskazini mashariki ya China, ambako katika majira ya siku za baridi halijoto ya sehemu hiyo ina wastani wa nyuzi chini ya sifuri. Mkoa huo wa Jilin ni mmoja kati ya mikoa yenye halijoto ya chini kuliko mingine ya China.
v Wageni wanaopenda kuishi vichochoroni mwa Beijing 2006/12/21
Wageni wengi kutoka ng'ambo wanaofanya utalii au kuja kufanya kazi mjini Beijing hupenda kutembelea vichochoro vya Beijing, baadhi yao hata wanapenda kuishi katika nyumba za kupanga na hoteli za watu binafsi zilizoko vichochoroni. Muda si mrefu uliopita, mwandishi wetu wa habari aliwakuta wageni kadhaa wanaopenda kuishi katika nyumba za vichochorini hapa mjini Beijing.
v Bibi Katysha anayefundisha lugha ya Kirussia nchini China 2006/12/07
Bi. Katysha mwenye umri wa miaka 24 hutoka Russia, hivi sasa anafundisha lugha ya Kirussia katika chuo kimoja cha ualimu mjini Hegang, mkoani Heilongjiang, kaskazini mashariki mwa China. Kutokana na mradi wa kubadilishana walimu kati ya China na Russia, Bi. Katysha alikuja China kutoka maskani yake iliyopo mkoa wa mashariki ya mbali, nchini Russia.
v Akina Bibi waliojikita katika kutunza na kuhifadhi Mto Hanjiang 2006/11/30
Mto wa Changjiang ni mto maarufu kwa urefu kwake kuliko mingine ya China. Tawi lake kuu linaitwa mto Hanjiang. Makala hii inahusu kina Bibi wawili wanaoishi kando ya Mto Hanjiang, ambao wamejikita katika shughuli za kueneza elimu ya kutunza na kuhifadhi raslimali ya maji, na kuzuia viwanda kadhaa visitoe maji machafu mtoni.
v Panda mzee 2006/11/16
Panda ni aina ya wanyama adimu wanaoishi nchini China, kwa hiyo wanajulikana kama tunu la taifa la China. Huko Fuzhou, mji wa pwani uliopo kusini mashariki mwa China, kuna panda mmoja maarufu, anayeitwa Basi. Basi ana umri wa miaka 26, kwa mujibu wa wanasayansi mwaka mmoja wa panda unalingana na miaka minne ya binadamu, kwa hivyo hivi sasa umri wa Basi unalingana na mzee mwenye umri wa miaka zaidi ya 100.
v Ujenzi wa kituo cha mambo ya fedha  2006/11/02
Shanghai ina mfumo kamili wa soko la mambo ya fedha wenye idadi kubwa ya wataalamu na uwezo mkubwa wa kuunganisha masoko ya mambo ya fedha ya sehemu zilizoko pembezoni mwake.
v Mwimbaji wa kabila la Wauzbek anayejikita kwenye shughuli za ufadhili 2006/10/19
Mkoa unaojiendesha wa Xinjiang Uygur upo sehemu ya kaskazini magharibi mwa China, ni mkoa wanakoishi watu wa makabila mbalimbali wakiwemo Wauzbek wanaojulikana kwa uhodari wa kuimba na kucheza ngoma. Bw. Xiamili Xiakeer ni mwimbaji maarufu atokaye kabila la Wauzbek, mbali na kuwa mwanamuziki pia anajihusisha na shughuli za utoaji misaada.
v Mfaransa Bw. Le Blainvaux anayefanya kazi nchini China  2006/10/05
Kampuni ya Shenlong ni kampuni kubwa ya kutengeneza magari hapa nchini China, ambayo ilianzishwa kwa ushirikiano kati ya kampuni ya Peugeot Citroen ya Ufaransa na kampuni ya Dongfeng ya China, pia ni mradi mkubwa kuliko mingine uliowekezwa na Ufaransa nchini China.
v Mahala pa kuwapa matumaini watu walioathirika na dawa za kulevya  2006/09/21
Dawa za kulevya zinachukuliwa kama shetani aliyehatarisha jamii na maisha, na kituo cha kuwatibu watu walioathirika kutokana na matumizi ya dawa hizo, ni mahala pa kupambana na shetani huyo na kunusuru roho zilizosumbuliwa.
1 2 3 4 5 6 7 8 9 10