Spika wa Bunge la Umma la China asisitiza kuhimiza maendeleo na utawala bora kwa kutumia sheria
Spika wa Bunge la Umma la China Zhang Dejiang asisitiza umuhimu wa kuhimiza maendeleo na utawala bora kwa kutumia sheria.
Zhang alisema hayo alipotoa ripoti ya kazi ya kamati ya kudumu ya bunge kwa wabunge wote kwenye mkutano wa mwaka wa bunge hilo unaoendelea jijini Beijing.
Ripoti hiyo imeonesha kuwa kipaumbele cha kazi ya utungaji wa sheria kwa mwaka huu, ni kuharakisha kukamilisha mfumo wa sheria ili kuhimiza utekelezaji wa mtazamo mpya wa maendeleo.
|
China yapunguza lengo la ukuaji wa uchumi ili kuzidisha mageuzi Serikali ya China inalenga kasi ya ukuaji wa uchumi ya kati ya asilimia 6.5 hadi asilimia 7 kwa mwaka katika miaka mitano ijayo. Kasi hiyo itakuwa cha chini zaidi katika miongo tatu iliyopita. Hata hivyo, muundo wa uchumi wa China umeendelea kuboreshwa, ambapo sekta ya huduma imechukua zaidi ya asilimia 50 ya pato la jumla la taifa GDP kwa mara ya kwanza na uvumbuzi umekuwa injini mpya ya uchumi.
|
Wajumbe wa mikutano miwili ya China wajadili namna ya kutekeleza mkakati wa kuondoa umaskini kwa hatua madhubuti Kwa mujibu wa mpango uliowekwa wa kutekeleza mkakati wa kuondoa umaskini kwa hatua madhubuti, ifikapo mwaka 2020, watu wote maskini nchini China wataondokana kabisa na umaskini. Utekelezaji wa mkakati huo umefuatiliwa sana na wajumbe wa mkutano wa baraza la mashauriano ya kisiasa la China, na mkutano wa bunge la umma la China.
|
Mkutano wa nne wa Baraza la 12 la mashauriano ya kisiasa la China wafunguliwa leo
Mkutano wa nne wa Baraza la awamu ya 12 la mashauriano ya kisiasa la China umefunguliwa leo hapa Beijing. Akifungua mkutano huo kwa kutoa ripoti ya kazi za kamati ya kudumu ya baraza hilo, mwenyekiti wa baraza hilo Bw. Yu Zhengsheng amesema, mwaka huu baraza hilo litatoa kipaumbele kwenye kazi ya kutoa ushauri na mapendekezo kuhusu utekelezaji wa mpango wa 13 wa maendeleo ya miaka mitano.
|
Masuala ya uchumi yafuatiliwa zaidi na vyombo vya habari kwenye mikutano miwili ya China itakayofanyika Mkutano wa kwanza na waandishi wa habari wa Mkutano wa nne wa Baraza la 12 la mashauriano ya kisiasa la China umefanyika leo hapa Beijing. Msemaji wa mkutano huo Bw. Wang Guoqing amefahamisha kuhusu ajenda ya mkutano huo na kujibu maswali ya waandishi wa habari, ambayo mengi yanafuatilia maendeleo ya uchumi wa China.
|
China ina imani ya kudumisha utulivu wa hali ya ajira mwaka huu Waziri wa raslimali watu na uhakikisho wa kijamii wa China Bw. Yin Weimin leo amesema, mwaka huu China inakabiliwa na ugumu mkubwa kwenye suala la ajira, kwa kuwa hatua za kudhibiti sekta ambazo uzalishaji umezidi mahitaji ya sokoni, zitapunguza idadi ya wafanyakazi kwenye sekta hizo.
|
Mageuzi ya kina yanasaidia kubadili maisha ya watu wa kawaida nchini China Takwimu zilizotolewa na wizara ya elimu ya China zinaonyesha kuwa, zaidi ya wanafunzi elfu 69 kutoka familia maskini vijijini wanafurahia sera mpya ya kujisajili vyuo vikuu iliyoanza kutekelezwa mwaka 2014.
|
China kuongeza nguvu ya kudhibiti uchafuzi wa hewa Katika miaka miwili iliyopita, uchafuzi wa hewa umekuwa tishio kwa afya ya wakazi wa sehemu nyingi nchini China, ingawa idara za kuhifadhi mazingira zimetekeleza hatua mbalimbali za usimamizi na kupata maendeleo kiasi, kutatua kabisa tatizo la uchafuzi wa hewa kunahitaji juhudi kubwa za pamoja kwenye jamii.
|
Serikali ya China yasema ina uwezo wa kudumisha utulivu wa kiwango cha ubadilishaji cha RMB Msemaji wa kamati ya maendeleo na mageuzi ya China Bw. Zhao Chenxin amesema, China ina uwezo wa kudumisha utulivu wa kiwango cha ubadilishaji cha RMB, na kwamba hatua za kudhibiti uzalishaji kwenye sekta ambazo uzalishaji wake umezidi mahitaji ya soko hazitasababisha mkondo mkubwa wa kupunguza wafanyakazi katika sekta hizo.
|
China yahimiza uvumbuzi wa kisayansi uhudumie mageuzi ya kiuchumi Viongozi wa idara za serikali ya China leo wamesema, China inajitahidi kuhimiza uvumbuzi wa sayansi na teknolojia uhudumie marekebisho yanayofanywa kwenye muundo wa uchumi wa China.
|
More>> |