• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Msanii Mashuhuri Bw. Jin Lisheng wa mchezo wa sanaa wa Pingtan
  •  2010-01-11

    Pingtan ni aina ya usanii wa kusimulia hadithi kwa kuimba na kuongea kwa lahaja ya mji wa Suzhou, usanii huu umeenea katika mikoa ya Jiangsu na Zhejiang, kusini mwa China. Usanii huo umewekwa na serikali katika orodha ya urithi wa utamaduni usioonekana wa China.
  • Msanii anayechora Picha kwa Sindano badala ya Brashi Bw. Gu Yuchun
  •  2009-12-28

    Bw. Guyuchun mwenye umri wa miaka 55 alikulia huko Nanchang, mji mkuu wa mkoa wa Jiangxi. Katika miaka ya 80 ya karne iliyopita, alikwenda mji wa Yangzhou mkoani Jiangsu kumfanyia tambiko babu yake, siku alipokuwa huko aliambiwa kwamba babu zake wote walikuwa mafundi wa kazi ya utarizi, hivyo akavutiwa sana na ufundi huo.
  • "Urithi wa Utamaduni Usioonekana wa China"-Opera ya Su
  •  2009-12-21

    Opera ya Su ni mchezo wa sanaa unaoenea katika mikoa ya Jiangsu na Zhejiang, katika sehemu ya kusini mwa Mto Changjiang nchini China. Mwaka 1941 Kundi la Opera ya Su ya Guofeng ambalo ni la kwanza kabisa la opera hiyo, liliundwa katika mji wa Shanghai, hii ilikuwa na maana ya kuanza rasmi kwa opera hiyo nchini China.
  • Shi Zhangyuan, Mwanamuziki Mkulima aliyetunga Nyimbo Zaidi ya 2000
  •  2009-12-07

    Katika wilaya ya Xiyang mkoani Shanxi, kaskazini mwa China, kuna mzee mmoja anayeitwa Shi Zhangyuan. Mzee huyo mwenye umri wa miaka 90, hafahamu namna ya kuonesha sauti kwenye mistari mitano ya kuandikia noti, kwa kuwa katika maisha yake yote anaishi vijijini, lakini kutokana na kupenda maisha na uzalendo alionao, katika muda wa miaka hamsini iliyopita ametunga nyimbo zaidi ya 2000.
  • Mwanasarakasi Mashuhuri wa China Bibi Deng Baojin
  •  2009-11-30

    Bibi Deng Baojin mwenye umri wa miaka 51 amefanya maonesho ya sarakasi kwa miaka zaidi ya 30 nchini China na nchi za nje. Licha ya kuwa amepata tuzo nyingi za dhahabu katika mashindano mengi ya kimataifa na kupewa heshima ya daima ya mafanikio katika michezo ya sarakasi na serikali ya China, pia alikuwa mjumbe wa Bunge la Umma la China katika vipindi vitatu mfululizo na sasa anapewa ruzuku maalum na serikali ya China.
  • Ngoma ya Afrika Yavuma Mjini Beijing
  •  2009-11-26

    Katika sehemu ya katikati ya mji wa Beijing kuna ziwa moja linaloitwa Houhai, sehemu lilipo ziwa hilo inavutia watu wengi kutokana na kuwepo kwa mikahawa ya kila aina na mazingira ya mkusanyiko wa tamaduni tofauti. Kila Jumapili alasiri wanaopenda kupiga ngoma za Afrika wanakusanyika huko na kufundishwa kupiga ngoma hizo na mwalimu wao anayeitwa Liu Yong. Wapita njia wengi wanavutiwa na kusimama huko kuangalia.
  • Mchoraji anayechangia maingiliano ya utamaduni kati ya China na nchi za nje Bw. Wang Peidong
  •  2009-11-23

    Bw. Wang Peidong wa wilaya ya Wuyang ya mkoa wa Henan ni mchoraji mahiri wa picha za maua na ndege kwa mtindo wa jadi wa Kichina, picha zilizochorwa naye mara nyingi zilipata tuzo kubwa nchini China na nchi za nje. Mwaka 2007 alichaguliwa kuwa ni mmoja kati ya wachoraji 30 wa picha zinazonunuliwa sana nchini China katiza zama za hivi leo. Bwana huyo pia ni mwanaharakati wa maingiliano ya utamaduni kati ya China na nchi za nje.
  • Michezo bora kabisa ya sanaa katika Tamasha la Kimataifa la michezo ya sanaa la Shanghai, China
  •  2009-11-16

    Tamasha la Kimataifa la 11 la michezo ya sanaa lilifanyika mwezi Oktoba mjini Shanghai, China. Tamasha hilo lilifunguliwa kwa mchezo wa ballet wa hadithi ya kale ya China iitwayo "Wang Zhaojun". Wasanii kutoka nchi 23 walikusanyika katika tamasha hilo na michezo mingi kama vile mchezo wa ballet wa "Wang Zhaojun" uliooneshwa na Kundi la Ballet la Mkoa wa Hubei na mchezo wa ballet wa "Dansi ya Wanawake Machoni mwa Wanaume" uliooneshwa na Kundi la Ballet la Monte-Carlo la Monaco
  • "Urithi wa Utamaduni Usioonekana wa China"-Usanii wa Nanqu wa Kabila la Watujia, China
  •  2009-11-09

    Nanqu ni usanii wa muziki unaochanganya kuimba na kuongea katika wilaya inayojiendesha ya Changyang ya kabila la Watujia, kusini magharibi mwa mkoa wa Hubei China. Usanii wa Nanqu unavutia kutokana na sauti yake inayoeleza hisia.
  • "Urithi wa Utamaduni Usioonekana wa China" Nyimbo za Jadi katika Kijiji cha Lujiahe
  •  2009-10-19

    Kijiji cha Lujiahe mkoani Hubei kinasifiwa kuwa ni "kijiji cha kwanza cha nyimbo za jadi za kabila la Wahan" nchini China. Kutokana na kufundishana nyimbo hizo wenyewe kwa wenyewe, wenyeji wa kijiji hicho wamehifadhi nyimbo za jadi zaidi ya elfu tano, sauti mbalimbali za nyimbo hizo zinafika 79.
    prev 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 next
    SearchYYMMDD  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako