• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tamasha kubwa la televisheni la Afrika la DISCOP lafanyika Afrika Kusini
  •  2015-11-13

    Tamasha kubwa la televisheni la Afrika la DISCOP limemalizika Jumatano wiki iliyopita mjini Johanesburg Afrika kusini. Katika kipindi cha leo, tutazungumzia tamasha hilo kubwa la televisheni barani Afrika.
  • Sanaa ya uchongaji wa mawe ya Soapstone huko Kisii, magharibi mwa Kenya
  •  2015-10-21

    Mawe ya Sopestone pia yanaitwa mawe ya Kisii, ambapo jina hilo linatokana na jina la kabila la Kisii linaloishi kwenye eneo la milima ya Tabaka, magharibi mwa Kenya. Watu wa kabila hilo wameanza kutumia mawe hayo mapema, na katika miaka ya karibuni tu wameanza kuchonga mawe hayo kwa ajili ya biashara. Ustadi hodari wa kuchonga wa wasanii wa Kisii umesaidia sana kujenga umaarufu wa vinyago vya Soapstone.
  • Maonesho ya 18 ya vitabu ya kimataifa ya Nairobi yafanyika
  •  2015-09-25

    Kauli mbiu ya maonesho hayo yaliyoandaliwa na Shirikisho la uchapishaji la Kenya ni "Twende Digital". Katika zama za leo, Digital ikiwa ni mwelekeo wa kisasa, imeibua mageuzi makubwa kwenye sekta zote zinazohusiana na mawasiliano na upashanaji habari, ikiwemo uchapishaji vitabu.
  • Tibet, chimbuko la Dansi ya Shon na nyimbo za mishale za Kongpo
  •  2015-09-18

    Kaunti ya Zanda iko kaskazini magharibi mwa mkoa unaojiendesha wa Tibet, watalii wengi kutoka nchini na nchi mbalimbali duniani hwenda kwenye kaunti hiyo kuona mandhari ya kushangaza ya kijiografia iitwayo misitu ya udongo au kwa kiingereza "Soil forest", pamoja na mabaki ya kale ya enzi ya mfalme Gurge iliyoanzia karne ya 10 na kudidimia ghafla baada ya miaka 700. Lakini kwa Bi. Ren Yunjuan aliyetembelea kaunti ya Zanda mara nyingi, ardhi hiyo ina mvuto mwingine maalum.
  • Utenzi wa mfalme Gesar, ensaiklopidia ya utamaduni wa Tibet
  •  2015-09-11

    Utenzi wa mfalme Gesar ni shairi la kughani linalojumuisha historia, mashairi, mithiolojia, methali na hekaya za Tibet ya kale. Kutokana na kufariki kwa waimbaji wazee, usanii wa kughani shairi hilo unakaribia kutoweka. Bw. Buqiong ni mmoja wa wasanii wachache vijana wanaoweza kughani shairi hilo. Katika kipindi cha leo, tutazungumzia hadithi za mwimbaji huyo Buqiong pamoja na utenzi wa Gesar.
  • Maonesho ya kimataifa ya vitabu ya Beijing ya mwaka 2015
  •  2015-08-28

    Maonesho ya kimataifa ya vitabu ya Beijing yanafanyika kuanzia Jumatano hadi Jumapili wiki hapa Beijing. Mashirika 2,270 kutoka nchi na sehemu 82 yanashiriki kwenye maonesho hayo, ambayo ni maonesho makubwa ya pili duniani.
  • Watu wa jamii ya Bushmen
  •  2015-08-21

    Jangwa la Kalahari lililoko nchini Botswana, kusini mwa Afrika, siku zote lina ukame na ukosefu wa mvua, lakini hapa ni nyumbani kwa watu wa jamii ya Bushmen ambao wana asili ya Afrika Kusini na nchi jirani za Botswana na Namibia. Katika jangwa hilo, watu wa jamii ya Bushmen wanasifiwa kama wataalamu wa mimea, udaktari na uwindaji.
  • Chakula cha kichina chatarajia kuorodheshwa kuwa urithi wa kiutamaduni duniani
  •  2015-08-14

    Mwaka huu ni mwaka wa tano tangu China ijiandae kutoa ombi la kuorodhesha mapishi ya kichina kuwa urithi wa kiutamaduni duniani. Kwa hiyo katika kipindi cha leo tutazungumzia maendeleo ya kazi hii pamoja na hali ya vitoweo vya kichina katika nchi za nje, haswa Afrika.
  • Mahojiano na Mwenyekiti wa Shirikisho la Filamu Tanzania Bw. Simon Mwakifwamba
  •  2015-08-07

    Tamasha la 18 la filamu la kimataifa la Zanzibar ZIFF limefanyika hivi karibuni huko Zanzibar, Tanzania. ZIFF ni tamasha kubwa zaidi la filamu, muziki na sanaa katika Afrika Mashariki, na linashirikisha wasanii wapya kutoka nchi mbalimbali duniani. Katika kipindi cha leo, tumefanya fursa ya kufanya mahojiano na mwenyekiti wa Shirikisho la Filamu Tanzania Bw. Simon Mwakifwamba.
  • Tamasha la 18 la Filamu la Zanzibar lafungwa
  •  2015-07-31

    Tamasha la 18 la filamu la kimataifa la Zanzibar ZIFF limefanyika hivi karibuni huko Zanzibar, Tanzania. ZIFF ni tamasha kubwa zaidi la filamu, muziki na sanaa katika Afrika Mashariki, na linashirikisha wasanii wapya kutoka nchi mbalimbali duniani.Kila mwaka, baadhi ya filamu nzuri zaidi kutoka Afrika na sehemu nyingine duniani zinaoneshwa kisiwani Zanzibar. Kutoka filamu za kimataifa na filamu fupi za kienyeji zote zinaoneshwa, tamasha hilo lina historia ndefu ya kuonesha filamu zenye sifa nzuri kutoka nchi mbalimbali duniani. Filamu zinafuata kaulimbiu ya mwaka, ambayo kwa mwaka huu ni "Mawimbi na njozi ya matumaini", na kuingia katika mashindano ya tuzo za aina tofauti. Usiku wa siku ya mwisho ya tamasha hilo ni usiku wa kutoa tuzo.
    prev 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 next
    SearchYYMMDD  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako