• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tamasha la 18 la Filamu la Zanzibar
  •  2015-07-24

  • Utamaduni wa harusi za wachina wabadilika kwa kuendana na wakati
  •  2015-07-16

    Harusi ni moja ya sherehe muhimu katika maisha ya karibu watu wote duniani, ambayo inaonesha mapenzi kati ya wanandoa na pia kuthibitisha wajibu na majukumu yao katika ndoa. Kila nchi na taifa lina utamaduni wake wa jadi kuhusu harusi, lakini mila na desturi hizo pia zinabadilika kwa kuendana na wakati.
  • Vichochoro ya Hutong ni alama ya kiutamaduni kwa wenyeji wa Beijing
  •  2015-07-07

    Hutong, ni vichochoro au mitaa miembamba inayozunguka kasri la kifalme yaani the Forbbiden City, ambavyo vinaunganisha makazi ya watu wa kawaida. Hutong imekuwa na historia ndefu, na tunaweza kusema ni moja ya sehemu muhimu zinazohifadhi utamaduni wa Beijing ya kale.
  • Tamasha la 6 la opera ya Nanluoguxiang
  •  2015-07-06

    Hivi karibuni tamasha la 6 la opera ya Nanluoguxiang limefanyika hapa Beijing. Nanluoguxiang ni eneo la makazi ya zamani kwenye kitovu cha Beijing, ambako kuna makazi ya mtindo wa jadi wa Beijing na vichochoro. Mchezaji dansi kutoka Cameroon Simon Abbe amealikwa kuja kutumbuiza katika tamasha hilo. Abbe na kundi lake la wachezaji dansi walifanya maonesho yanayoitwa "Uwezo unaosahaulika". Maonesho hayo yanalenga kuwakumbusha watu uwezo uliofichika ndani yao, na kuwaambia watu kuwa wasisahau uwezo wa kiasili katika jamii ya kisasa.
  • Sanaa ya kuchorachora na zentangle
  •  2015-07-06

    Leo hii katika kipindi hiki tutakuelezea kuhusu sanaa ya kuchorachora ambayo inapendwa na watu wengi zaidi. Watu wengi wanapenda kuchorachora wakati wanapoongea na simu, kukaa kwenye mkutano au kusikiliza wanachofundishwa darasani. Hivi sasa kuchorachora kunachukuliwa kama mtindo wa sanaa unaopendwa na watu wengi.
  • Kabila la mbilikimo barani Afrika liko hatarini kutoweka
  •  2015-06-11

    Kabila la mbilikimo ni kabila la watu wafupi barani Afrika, pia kwa kiingereza wanaitwa kabila la Nigrillo, kwa wastani watu wazima wa kabila hilo wana urefu wa mita 1.3 hadi 1.4. Utafiti wa kianthropolojia umethibitisha kuwa watu wa kabila la mbilikimo ni warithi wa ustaarabu wa Sangha uliokuwepo kabla ya historia ya binadamu. Ingawa mbilikimo ni wafupi, lakini wana nguvu kubwa na wote ni wawindaji hodari na kujiita kuwa "watoto wa misitu".
  • Sanaa ya michoro ya Tingatinga yahitaji kutangazwa zaidi ili kupanua soko lake duniani
  •  2015-06-03

    Michoro ya Tingatinga huchorwa kwa kutumia rangi mbalimbali ang'avu zinazovutia macho, kutokana na wasanii wa Afrika kuwa na upendeleo huo maalumu wa rangi, Tingatinga inachukuliwa kuwa ni moja ya sanaa zinazowakilisha mitindo ya uchoraji ya kiafrika.
  • Tamasha la 15 la sanaa la kimataifa la Meet In Beijing lamalizika
  •  2015-05-28

    Tamasha la sanaa la kimataifa Meet in Beijing ni moja ya matamasha makubwa ya sanaa nchini China, ambalo kila mwaka wasanii kutoka nchi na sehemu mbalimbali duniani hualikwa kuonyesha utamaduni wao wa kipekee hapa Beijing katika kipindi cha mwezi mmoja hivi, na tamasha hilo litakalomalizika kesho ni la awamu ya 15. Tamasha la mwaka huu limeshuhudia makundi 42 ya wasanii na bendi 104 za muziki kutoka nchi na sehemu 25 duniani zikifanya maonesho zaidi ya 100 ndani ya kumbi mbalimbali na mengine 50 kwenye viwanja vya wazi.
  • Siku ya kimataifa ya jumba la makumbusho
  •  2015-05-22

    Msikilizaji mpendwa, karibu katika kipindi cha Utamaduni Wetu. Mei 18 ni maadhimisho ya 39 ya kimataifa ya jumba la makumbusho. Kaulimbiu ya mwaka huu ni "Jumba la Makumbusho linafanya juhudi ya kuhimiza maendeleo endelevu ya jamii". Majumba ya makumbusho nchini China yaliandaa shughuli mbalimbali zilizowavutia watazamaji wengi wakiwemo wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.
  • Duka la vitabu la Sanlian linalofunguliwa saa 24 kwa siku
  •  2015-05-22

     Kuna mikahawa na maduka mengi yanayofunguliwa saa 24 kila siku katika sehemu mbalimbali duniani, lakini maduka ya vitabu ya saa 24 sio mengi sana. Mwezi Aprili mwaka jana, duka la vitabu la Sanlian Taofen la Beijing lilianza kufunguliwa saa 24 kwa siku, na limekuwa duka la vitabu la kwanza linalokuwa wazi siku nzima jijini Beijing. Baada ya mwaka mmoja, duka hilo limefungua tawi lake katika eneo lenye vyuo vikuu vingi jijini Beijing, ambalo pia liko wazi saa 24. Kutokana na mafanikio ya duka hilo, maduka mengine mawili pia yameamua kujiunga na kundi la maduka ya vitabu ya saa 24. Je, ama kweli watu wanakwenda duka la vitabu usiku wa manane? Na baada ya mwaka mmoja, uendeshaji wa duka la vitabu la Sanlian linalofunguliwa saa 24 inakuwaje? Wasomaji wana maoni gani kuhusu duka hilo?
    prev 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 next
    SearchYYMMDD  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako